Mambo ya mila yananinyima usingizi....


Tawire mkuu, kuna jamaa mmoja alitaka kuoa binti mmoja wazee including baba yake wakamkatalia katu katu na hakuna sababu ya maana wanampa, kijana akagangamala akao, baadae akagundua kumbe baba yake alizaa na shangaza wa yule binti aliyeoa. Wazee hawakuipenda ile picha, kijana yuko na mkewe mpaka leo.
 
Zungumza na familia yako kijiti kizima! Naamini watakuelewa kuliko kuchukua drastic sana Kama kupata uja uzito kwanza
 
wanameremetaaaaaaaaaaa........wanameremetaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!
ryeeeeeeeeeeeeeryeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!
 
Waelimishe wazee wako watakuelewa hizi mila hazina maana, eti msioane kwa sababu mnatoka sehemu moja haiingii akilini!
 
Angalia hapo kwenye bold dada!
Wewe umetuambia una miaka nane hujaonana naye afu hata kwa sasa mnakaa mabara tofauti,kuna uwezekano mkubwa kuwa hayo mapungufu wanayokuambia ndugu zako ni ya kweli.Be careful sometimes love can make you BLIND...

Asante sana Gwamahala
Nitalifanyia kazi swala hilo, ingawa wanaosema hivo wako Tanzania, huyo kijana yuko bara lingine, nami bara lingine (mabara matatu tofauti)
 
Jamani tusiangalie mila tu, lazima kuna mambo mengi ya kufanyia kazi hata kabla hujaanzana urafiki wowote na mtu. Kwanza kabisa huyu dada alipaswa kuwaza kwa nini wazazi waseme mila na desturi, may be there was problem wanashindwa kuisema wanaamua kusema hivyo. Cha kufanya kwa muda huu wabane wazazi wakwambie ukweli wakati ukifanyia uchunguzi wa familia ha bwana yako. Hata yeye aisibweteke ascan life style yenu ili ajue atakaaje na wewe.

Nakushauri binti fanya uchuguzi usijeolewa kwenye famila ya waanguka kifafa, walevi, waasherati, vichaa. hayo ni mambo ya kuangalia kabla ya kuolewa au kuoa. Samahani sina dharau kwa magonjwa niliyoandika ila ni vizuri ukiyajua ili hata baadae ukayahimili othewise ndoa itakufa within a year.
 

Ni kweli katika maisha kuna mambo mengi sana watu wanayaficha , embu fikiria kuwa unazaa na mke wa mtu mtoto wa kiume, halafu baadaye inatokea kuwa mtoto huyo huyo wa kiume anataka kuja kuoa nyumbani kwako!! Halafu cha kufuraisha huyo uliyezaa naye ni mke wa rafiki yako mpenzi, na yeye anaona kuoa hapo ni kudumisha urafiki, kumbe anayetaka kumuoa na dada yake kiaina!!! Kuna Ndoa hapo kweli??? KILA SABABU ITATOLEWA Ili pasioleke.
 




ikiwa bado yanaendelea kukunyima usingizi hayo mambo ya mila ngoja nikupe formula nyengine ikifika saa moja jioni hakikisha umekula umeshiba vizuri kisha meza valium 8 utalala mpaka kesho yake saa 6 mchanga utarudia hivyo hivyo kwa muda wa siku 7 nadhani mawazo yataisha. au hao wazee wavutie mjani halafu ukawaropokee wakome.
 

Hapo kwenye blue... Nikilala hivo masomo yatakula kwangu
Nyekundu ndo hatari kabisa... Siwezi maadili hayaruhusu kabisaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…