Pre GE2025 Mambo ya msingi na muhimu Kwa Chadema kuyatekeleza kwa sasa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025

Pre GE2025 Mambo ya msingi na muhimu Kwa Chadema kuyatekeleza kwa sasa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
15,692
Reaction score
23,038
Baada ya uchaguzi huru na wa haki ulochukua siku mbili mfululizo na kutoa matokeo ambayo yameushangaza ulimwengu na kuiacha CCM hoi, kazi ilobakia kwa Chadema ni kujijenga uzuri na kuhakikisha mitambo yote yafanya kazi barabara.

Katika hotuba yake jana Makamu mwenyekiti wa CCM tayari kawapa mwanya Chadema kuzungumza na wananchi na kuwaelimisha kwanini wao wafaa kuwa mbadala na CCM.

Sasa, mimi binafsi nilitaka mabadiliko kwa Chadema ili kupata watu wapya wenye sera na mitizamo tofauti kabisa na wale walokuwepo. Nimemsikiliza Godbless Lema katika mahojiano yake na "Power Breakfast" na hakuniangusha, amesema aliongea na ndugu wote kuwapa msimamo wake kwamba amekuwa na mtizamo mwingine na aliazimia kumweleza Freeman Mbowe kwamba Chadema yachukua njia ingine na mtazamo mwingine.

Natambua kwa sasa bado mwenyekiti mpya mheshimiwa Tundu Lissu yupo ahangaika kusuka timu yake mpya ndani ya Chadema na si kusudio la mada hii kujadili hilo.

Nampa pongezi zangu Tundu Lissu na makamu wake John Heche kwa kuchaguliwa kuwa viongozi wapya wa Chadema wenye mwelekeo pya ambao ndo nimekuwa nikipigia kelele miaka kwa muda mrefu hapa JF. Na Hatimae kilio changi kimesikika na sasa ni kupiga kazi na hakuna kulala hadi kieleweke.

Hapa nipo kuzungumzia ni yepi Chadema yafaa kuyafanya kuanzia sasa hadi ufikapo uchaguzi mkuu na baada ya hapo pia.

1. Kutambulisha kaulimbiu ya chama.

Kaulimbiu ni moja ya mambo muhimu sana katika kukiweka chama karibu na wapiga kura na kuanza kuwaelimisha yae chama kimekusudia. Kwa kuwa tayari makamu mwenyekiti wa CCM mzee Wassira tayari amesema Chadema wakazungumze na wananchi, basi hakuna sababu ya Chadema kuhakikisha inawapa elimu nzuri wapiga kura wa Tanzania kuhusu masuala yote muhimu likiwemo suala la katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, kupiga vita rushwa na masuala mengine mengi tu.

2. Kutengeneza Ilani ya uchaguzi (Manifesto) mapema.

Hii itawasaidia Chadema kuwa na mwelekeo wa siasa zake na kuweka kufanyia marekebisho ilani hiyo kwa jinsi hali ya kisiasa na kisera za nchi inavyokwenda. Bila shaka Chadema itachukua mwelekeo mpya (new approach) na kueleza njia sahihi kuelekea nchi ya ahadi ikiwa katika kufaidi keki ya taifa, elimu bora, huduma za afya kwa kila mwananchi na mazingira mazuri kwa watumishi wa serikali khasa walimu ambao leo walipwa shilingi 3,000 kwa siku kwa kuhudhuria mafunzo ya muda mfupi.

3. Kupata watu wa stratejia.
Watu wa stratejia katika chama ni muhimu sana. Ili kampeni ifanikiwe uzuri ni muhimu kuwapata watu hawa ambao watakiweka chama katika taswira halisi ya chama kilicho tayari kuchukua mamlaka ya Jamhuri ya Tanganyika na ile mamlaka ya Zanzibar.

Labda nimuelezee kwa kifupi mtu wa stratejia ni mtu wa namna gani?

Huyu ni mtu maalum ambae kazi yake kubwa ni kuhakikisha wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi watengeneza stratejia nzuri za kushinda uchaguzi. Humo atafanya utafiti kwa wapiga kura, kuelewa matatizo ya wapiga kura (sio kero) na kutengeneza kauli zinoshabihiana na zile za wapiga kura.

Majukumu mengine ni kuhakikisha tovuti za chama na mitandao yote ya kijamii yatumiwa vema na chama. Kwa mfano hadi sasa bado ni vigumu kwa totuti ya Chadema kupatikana mitandaoni na hiyo kasoro ni muhimu kuangaliwa.

4. Kuajiri meneja wa Kampeni.

Meneja wa kampeni ni mtu mwingine muhimu kwa chama ambae atahakikisha shughuli zote za kampeni zipo sawa. Majukumu mengine ni pamoja na kuhakikisha zinakuwepo vyanzo imara vya fedha, kuwepo kwa matangazo ya chama, kusimamia mahusiano ya chama na wadau wa nje ya chama, na kusimamia bajeti ya chama kuhakikisha malengo ya chama yapo sawa.

5. Kutengeneza mapema stratejia ya kisiasa -Political strategy.

Kwa kuwa tumezoea stratejia ya CCM katika kuwasilisha ujumbe wake wa wananchi kwamba Tanzania ni nchi ya amani na utulivu na kwamba bila amani hakuna maendeleo au sasa kuna msemo kutoka kwa makamu kwamba bila amani hakuna maridhiano.

Sanaa ya kutuma ujumbe katika stratejia ya siasa ni moja ya njia kuu kubwa na yenye nguvu sana, na imekuwa mara nyingi ikitumiwa visivyo au kutotumika kabisa. Ujumbe wa mwanasiasa huweza kubadili mawazo ya wapiga kura, hivyo ujume wa kisiasa ni lazima uwe ni ule wenye ushawishi na unolenga wapiga kura wenye kuitika na si wale wafuata upepo. Kwa mfano si kila ujumbe wa kisiasa uwe ni wa kufanya maandamano, bali Chadema chaweza kufanya mikutano mingine inofanana na ule wa Mlimani City lakini kikiwa na malengo ya kufikisha ujumbe wa waanchi wote kwa njia zote nilozitaja hapo juu.

6. Kulenga kupata wabunge wengi bungeni.

Kwa kuwa Chadema imeshindwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa, itakuwa ni vema Chadema ikalenga kupata viti vingi bungeni, jambo litowasadia kupeleka bungeni hoja kadhaa ikiwemo hoja ya tume huru ya uchaguzi na mabadiliko ya katiba. Ikumbukwe uwingi wa kura na wabunge bungeni ni silaha tosha kwa chama chochote kuwa na nguvu ya kuleta hoja kadhaa bungeni na zikapita kwa ushawishi wake.

Yapo mambo mengine mengi kama vile kutangazwa mgombea uraisi, kuundwa kwa baraza kivuli la mawaziri, idara zingine kadhaa na khasa ile ya ujasusi ambayo itakuwa na jukumu la kuchuja ni mwanachama yupi amenza kutorokea kwenye mzinga nyakati za usiku kulamba asali.

Kila la kheri Chadema chini ya Tundu Lissu na John Heche pamoja na wanachama wao.
 
Hapo kwenye kutengeza ilani ya Uchaguzi,

Dr Slaa arejeshwe haraka, akili zake Bado ni Bora sana, tuzitumie🙏
 
Lisu amesema "No Reform no Election". Sasa wataendaje kwenye huo uchaguzi bila reforms? Ungewashauri namna ya kupata hizo reforms wanazotaka.
 
Lisu amesema "No Reform no Election". Sasa wataendaje kwenye huo uchaguzi bila reforms? Ungewashauri namna ya kupata hizo reforms wanazotaka.
Hiyo ni kauli ya kawaida ya kisiasa ambayo mwanasiasa aweza kutumia kufikisha ujumbe kwa wapiga kura.

Lakini kauli hiyo haimaanishi kuwa kwa wakati huo ni kaulimbiu.

Ndo maana ni muhimu kwa sasa kutafuta kaulimbiu ingine ambayo itaendana na mazingira sasa, khasa baada ya usanii ulofanywa pale Dodoma ulishirikisha wasanii wenyewe.
 
Back
Top Bottom