Vinci Dayot Upamecano
JF-Expert Member
- Nov 11, 2020
- 524
- 1,288
Asalaam Aleykum warahmatullah wabarakatul, Ramadan Mubarak.
Penye hela nyingi hapaharibiki neno, kuna mshkaji wangu mmoja hiv ametusua bwana, sasa siku ya Jana Ijumaa alinipa mualiko kwenye Hafla fupi ya kumpongeza Binti yake wa miezi 10 kwa sasa, ameweza kutembea mwenyewe.
Kwanza sherehe ilikuwa sio baridii, Wageni walikuwa nyomi Ile mbayaa, yaani watu walikuwa ni wengi sana waliokwenda kusherehekea mtoto ameweza kutembea mwenyewe (na mimi pia ni miongoni mwao). Ilikuwa ni kama li'sherehe fulani hivi likubwa la harusi, Kuanzia muziki, vyakula, vinywaji, wageni, ukumbi, Maonyesho hadi Zawadi kumbe ni mtoto ameweza kutembea, wanangu tutafute mboga.
Jamaa ni kawaida yake tangu atusue (naongea kwa kumsifu sio kwamba nampiga madongo) amekuwa anafanya vi'event fulani hiv vyenye maudhui ya kawaida kwa gharama kubwa sana (pesa si ipo bwana). Jamaa anakwambia tangu anazaliwa mpaka mwaka juzi 2021 hakuwahi kufanyiwa Birthday Party, Sasa hiyo mwaka Jana alijifanyia Birthday Party ya kufuru, watu tulikula, kunywa na kusaza.
Mwaka Jana 2022 kafanya bonge moja la Party kuzindua nyumba yake, mwaka huohuo kamfanyia Party moja ya kutisha mtoto wa sister'ake kumpongeza kwa kuhitimu Nursery.
Bado una ule mtazamo wako kuwa "Pesa haiwezi kununua furaha"?