mambo ya quotations-ushauri

mama dunia

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2011
Posts
420
Reaction score
84
Hi wanajamvi, mi kuna kitu huwa kinanisumbua kwenye huu ujarisiamali, yaani utakuta mtu anakuomba quotation lakini hakupi kazi, najua sometimez unaweza ukawa higher/yani bidder wa juu kibei nk, lakini majuzi nimegundua kuwa most of them wanakuwa na watu wao tayari yaani wewe unakuwa unatoa mi-quotations weee then anakuwepo mtu wao tayari, tena mbaya zaidi sometimes ni ile call for proposal ambayo unajipinda kuandika kuweka midata nk kumbe ukija kupeleleza kuna mtu, sasa kwakweli inakatisha tamaa, lakini sasa utajuaje kama hii sehemu ni yakupeleka quotation na hii sio, mi napenda sana changamoto yani kushindana kwa vigezo nk lakini ndo hivyo tena, utakuta kuna mtu/ofc anaweza akakusumbua hadi ukampatia ukijua may be utapata lakini hola, tena saa ingine mnakuwa bidder wawili tu!, kuna rafiki yangu yeye alishaniambia hafanyi mambo ya kupeleka hizi quotes yeye anasubiria kazi tu, hapotezi mda kuandaa quotes, kuna mwingine pia aliniambia yeye na tender za serikalini hataki kusikia, ingawa ni kweli serikalini kupata napo shughuli mhh..hebu wekeni mawazo maana tunakoelekea watz na hizi 10 % ni noma-maana mtu anatoa kwanza ndo kupata job na kama hujulikani ndo balaa zaidi....
 
Haya mambo yako sana, wewe huoni hata Kule Alibaba wachina wanavyo pata shida? wanaweza chati na mtu na wakamtumia Proformer Invoice ila jamaa mwisho wa siku anaingia mitini, na vile vile ni sawa na ukienda Dukani unalizia kitu and then baadae unawaambia utarudi halafu ndo kimoja,

Kuna changamoto ila wewe kama mjasirimali ni kukaa chini na kuja solution
 
ni kweli juu ya hayo unayoongea,nimeshafanya kazi sehemu kama tau kwenye kitengo cha manunuzi,quotation mara nyingi hutolewa kwa watu wanaowajua au wale wenye kutoa ten pasenti,so ni ngumu sana kwa mtu usio na watu unaowafahamu.
 
ni kweli juu ya hayo unayoongea,nimeshafanya kazi sehemu kama tau kwenye kitengo cha manunuzi,quotation mara nyingi hutolewa kwa watu wanaowajua au wale wenye kutoa ten pasenti,so ni ngumu sana kwa mtu usio na watu unaowafahamu.
Hiyo ipo sana, na nyie wengine mnawekwa pale kuisindikiza quotation ya jamaa tu... Maana walio wengi wanataka quotations tatu, ya wanayemtaka ndo itapita..
 
yeah kweli ipo kazi! kuchange hii kasumba ni ngumu sana wajameni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…