Mambo ya Tupac Amaru Shakur (1971-1996)

Mambo ya Tupac Amaru Shakur (1971-1996)

Dogoli kinyamkela

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
618
Reaction score
1,440
MAMBO YA TUPAC AMARU SHAKUR (1971-1996)
1732375283182.jpg
Watu timamu wanaulizana...Ilikuwaje na ni kwa namna gani Tupac Amaru Shakur, kijana wa Marekani mwenye asili ya Kiafrika kufanya mengi na kupandikiza itikadi ama legacy kubwa mno pamoja na kuacha historia ndefu mno na alifariki akiwa na miaka 25 tuu😃...Alizaliwa 1971 na akauwawa 1996 kwa kupigwa risasi,huko Marekani!!
Mambo mengi hususani kwenye muziki wake aliyafanya kwa muda wa miaka 3-5 katika kipindi cha umaarufu wake ingawa muziki aliuanza akiwa shuleni akiwa na miaka 17+ alipojiunga na kikundi cha muziki kiitwacho Digital Underground mwaka 1989...Aliishi katika kundi hilo hadi kutoa Albamu (Solo Album) yake ya kwanza ya 2Pacalypse mwaka 1991 ambayo ilitambulika na kusikilizwa kimataifa😃
Tupac ana albamu nne ambazo nyingine alizitoa wakati wa uhai wake na nyingine 7 zilitolewa baada ya kifo chake...
Enzi ya uhai wake alitoa albamu nne tuu ambazo ni 2Pacalypse Now (1991), Strictly 4 My N.I.G.G.A.Z. (1993), Me Against the World (1995), All Eyez on Me (1996) na nyingine zipatazo 7 zilitolewa baada ya kifo chake!!...
Nyimbo zake nyingi alijikita katika kusawiri maudhui na maudhui yake yalikuwa na mchanganyiko wa maumivu ya kibinafsi, changamoto za kijamii, na harakati za kupigania haki, haswa haki za Wamarekani weusi (Negroes/Nigga) dhidi ya madhalimu ya Wazungu huko Amerika!!
Kiujumla ni kuwa, Kipindi alichoishi ni kifupi sana ukilinganisha na mambo mengi sana aliyofanya pamoja na itikadi pia na historia aliyoiacha!!
Huyu alikuwa ni Icon katika mziki wa Hip Hop ila hakuwahi shinda grammy sasa sijui ilikuwaje🙄

Tujaribu ku-share historia yake tuisome tuone ni mbinu gani alizitumia licha ya kuwa ana kipaji...Ila ni wangapi walikuwa na vipaji na wakaishi miaka zaidi ya 30 ila hawajaacha legacy kubwa kama yake🙄
Hebu tujaribu ku-share mawazo hapo kwenye comments...ALIFANYAJE KUFIKIA HATUA ALIYOFIKA!?
Ni mimi ndugu mwandishi Dogoli kinyamkela
 
Kwa miaka michache aliyofanya muziki na kumbukumbu nzito ya kazi kubwa, inamfanya aonekane ni moja ya watu bora waliopata kupita duniani.. Vipi angeishi mpaka 40+

Umauti ni zaidi ya ukuta kwenye maisha ya mwanadamu...
Lakini ndio haukwepeki.
 
Bora 2Pac ambaye umaarufu wake umeongezwa na kifo chake. Ila mimi huwa namshangaa zaidi Bob Marley na utitiri wa watoto aliouacha.
Ulitakiwa umshangae Tupac imekuaje hakuacha hata mtoto pamoja na umaarufu na utajiri wake?.. Bob katuachia kina Ziggy na wenzake , huyo 2pac alitumia muda wake kutukana na kugombana na wanaume wenzake bila sababu za maana... hopeless kabisa yule...
 
Back
Top Bottom