Mambo yafuatayo yananifanya nione hakuna umuhimu wa katiba mpya kwa sasa

Mambo yafuatayo yananifanya nione hakuna umuhimu wa katiba mpya kwa sasa

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
2,789
Reaction score
4,951
Huu ni mtazamo wangu binafsi juu ya katiba iliyopo na umuhimu wake licha ya upinzani kuipigia kelele. Mtazamo wangu ni kwamba katiba ya JMT ni bora sana na kwa sasa ni baadhi ya vipengele tu vinahitaji kurekebishwa.

Yafuatayo ni mambo yanayofanya nione umuhimu wa katiba tuliyanyo:

I) Madaraka na mamlaka ya Rais. Siku zote ninaamini ili nchi itawalike vizuri naamnini ni lazima mamlaka na Madaraka ya Rais yawe ni makubwa. Rais anapokuwa na mamlaka makubwa juu ya utumishi, uongozi, siasa n.k inasaidia Wananchi na viongozi kuiheshimu hiyo mamlaka na ndio maana ninaona umuhimu wa katiba hii kuliko katiba mpya kwa sasa ambayo inajaribu kumuondolea Rais mamlaka aliyonayo.

ii) Katiba ya sasa inaleta utulivu mkubwa wa kisiasa hususani kwenye nafasi za kuchaguliwa. Kiongozi anapochaguliwa anapata wasaa mzuri wa kutekeleza mipango na ahadi zake.

iii)Katiba hii ya sasa inatafsiri misingi ya kijamaa ambayo ni msingi wa utaifa wetu.
 
Back
Top Bottom