JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ibara ya 4(3) imeeleza kuwa kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za umma Katika Jamuhuri ya muungano na kwa ajili ya madaraka juu ya shughuli hizo kutakuwa na mambo ya muungano ambayo yatafanywa kwa ushirikiano kati ya Tanzania bara na Zanzibar na pia kutakuwa na mambo yasiyo ya muungano.
Mambo yote ya muungano yameorodheshwa katika Nyongeza ya Kwanza ( First Schedule) katika katiba hiyo.
Mambo hayo ni kama ifuatavyo:-
1. Katiba ya Tanzania na serikali ya Jamhuri ya Muungano.
2. Mambo ya Nchi za nje
3. Ulinzi na usalama
4. Polisi
5. Mamlaka za Juu ya mambo
yanayohusika na hali za hatari
6. Uraia
7. Uhamiaji
8. Mikopo na Biashara ya Nchi za nje
9. Utumishi katika serikali ya Jamhuri ya muungano
10. Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa Forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha
11. Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta, na simu
12. Mambo yote yanayohusika na sarafu na fedha kwa ajili ya malipo halali, mabenki na shughuli zote za mabenki, fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusika na fedha za kigeni.
13. Leseni ya viwanda na takwimu
14. Elimu ya juu
15. Maliasili ya mafuta
16. Baraza la Taifa la Mitihani ya Tanzania
17. Usafiri na usafirishaji wa Anga
18. Utafiti
19. Utabiri wa Hali ya hewa
20. Takwimu
21. Mahakama ya Rufani
22. Uandikishaji wa vyama vya siasa na mambo mengine yanayohusiana navyo.
Hivyo, mambo mengine yote ambayo hayapo katika orodha hii sio mambo ya muungano, pande zote mbili ( Tanzania Bara na Zanzibar) zinaweza kuyaendesha tofauti.
Mfano wa Mambo yasiyo ya muungano ni pamoja na Ardhi na Mazingira.
Upvote
2