Mambo yaiva ujio wa ndege tano zilizonunuliwa na serikali

kalacha mateo

Senior Member
Joined
Sep 27, 2021
Posts
119
Reaction score
240
Ndege mpya moja kati ya tano ambazo serikali iliahidi itazinunua, inatarajia kuwasili nchini Machi au Aprili, huku nyingine nne zilizobaki zikitegemewa kuwasili nchini kwa nyakati tofauti mwaka huu. Aidha John Nzulule, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) anasema maendeleo ya matengenezo ya ndege hizo yanaendelea vizuri.

Juni mwaka 2022 katika hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba wakati akiwasilisha bungeni bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2022/23 alisema serikali imeshanya malipo ya awali ya ununuzi wa ndege mpya tano.

Katika ndege hizo tano moja ni ya abiria ya masafa marefu yenye uwezo wa kubeba abiria kuanzia 26, nyingine ya mizigo ya masafa marefu itakatotumika kusafirisha mizigo mbalimbali. Ndege nyingine mbili zitakua za masafa ya kati zenye uwezo wa kubeba abiria kati ya 160 hadi 170 na moja itakua ya kubeba abiria kati ya 76.

"Tunashukuru Rais kwa kuidhinisha ununuzi wa ndege hizo, zikfika zitaongeza connrctivity (safari za kuungsnisha ndege) na zitainua uchumi wetu." alisema John Nzulule

3f8534dfae37498a4e718d6d08fd831ba08cc81e.jpg
 
Hovyo kabisa!. Kati ya ndege nne aina ya Airbus 220-300 zilizodaiwa kununuliwa "Cash" na Serikali ni moja tu inayoonekana kuruka tena kwa machale sana. Moja imehifadhiwa Uholanzi na nyingine mbili hazijulikani zilipo.

Kuna sababu gani ya kuendelea kutumia vibaya pesa za walipa kodi kununua ndege tano zaidi wakati tatu hazifanyi kazi iliyokusudiwa? Mwenendo wa kampuni ya ndege ya Tanzania itakayo kabidhiwa hizo ndege inapaswa kuchunguzwa hasa kwenye "Ticketing" kuna ubadhirifu unafanywa na wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Mkurugenzi mkuu wa Air Tanzania anapaswa kuwachunguza wafanyakazi wake kwa umakini mkubwa, vinginevyo atavuna mabua na mapato ya kampuni yataendelea kuingia kwenye mifuko ya wafanyakazi janja janja wanaocheza na mifumo ya kidigitali......
 
Wanasema ni wa humuhumu ndani
Ni mtu fulani wa biashara anataka asafirishie mizigo yake.
CHADEMA wanajua ila kwa Sasa wameonesha wazi wao ni mpango wa kando wa CCM na sio wapinzani.
 
Hovyo kabisa!. Kati ya ndege nne aina ya Airbus 220-300 zilizodaiwa kununuliwa "Cash" na Serikali ni moja tu inayoonekana kuruka tena kwa machale sana. Moja imehifadhiwa Uholanzi na nyingine mbili hazijulikani zilipo.

Kuna sababu gani ya kuendelea kutumia vibaya pesa za walipa kodi kununua ndege tano zaidi wakati tatu hazifanyi kazi iliyokusudiwa? Mwenendo wa kampuni ya ndege ya Tanzania itakayo kabidhiwa hizo ndege inapaswa kuchunguzwa hasa kwenye "Ticketing" kuna ubadhirifu unafanywa na wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Mkurugenzi mkuu wa Air Tanzania anapaswa kuwachunguza wafanyakazi wake kwa umakini mkubwa, vinginevyo atavuna mabua na mapato ya kampuni yataendelea kuingia kwenye mifuko ya wafanyakazi janja janja wanaocheza na mifumo ya kidigitali......
Mkuu kwani parking shed zimejaa?
 
Poor strategy, Ethiopia wanasifika kwa plane za abiria, sisi tulipaswa tusifike kwa cargo plane of various sizes!, na tuwe na za ukubwa wa wastani za kwenda mikoani na kuzunguka kwa majirani zetu, lakini toka base kwenye cargo plane!
 
Jiwe alishavuta tenpasenti, na amekufa hajatumia hata mia.

Wapambe wake walikuwa wanakomaa za Stiglers na reli zilipwe haraka kwa kuwa Wana vikampuni vyao huko, akina polepole Humphrey,

Mama Ana yeye ana tenda ya kulisha watumishi huko Stiglers
 
Ndege mpya moja kati ya tano ambazo serikali iliahidi itazinunua, inatarajia kuwasili nchini Machi au Aprili, huku nyingine nne zilizobaki zikitegemewa kuwasili nchini kwa nyakati tofauti mwaka huu. Aidha John Nzulule, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) anasema maendeleo ya matengenezo ya ndege hizo yanaendelea vizuri.

Juni mwaka 2022 katika hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba wakati akiwasilisha bungeni bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2022/23 alisema serikali imeshanya malipo ya awali ya ununuzi wa ndege mpya tano.

Katika ndege hizo tano moja ni ya abiria ya masafa marefu yenye uwezo wa kubeba abiria kuanzia 26, nyingine ya mizigo ya masafa marefu itakatotumika kusafirisha mizigo mbalimbali. Ndege nyingine mbili zitakua za masafa ya kati zenye uwezo wa kubeba abiria kati ya 160 hadi 170 na moja itakua ya kubeba abiria kati ya 76.

"Tunashukuru Rais kwa kuidhinisha ununuzi wa ndege hizo, zikfika zitaongeza connrctivity (safari za kuungsnisha ndege) na zitainua uchumi wetu." alisema John Nzulule

3f8534dfae37498a4e718d6d08fd831ba08cc81e.jpg
Tengenezeni zile zilizokufa kwanza, pili tatuteni masoko, ndege sio kwa ajili ya kupaki viwanjani jamani.
 
Back
Top Bottom