Mambo yakufanya Mwanaume unapokuwa likizo ya Uzazi (Paternity Leave)

Mambo yakufanya Mwanaume unapokuwa likizo ya Uzazi (Paternity Leave)

Status
Not open for further replies.

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
0001-18715954880_20210323_132801_0000.png


Kuwa karibu sana na Mama wa Mtoto(Mzazi) msaidie na toa muongozo sehemu inayoweza au unayotakiwa kufanya hivyo

Lazima uwe umejiandaa kumpokea Mtoto onesha kumuunga mkono Mama wa Mtoto na si kumshangaa Mtoto pekee na kumsahau Mama yake (usihamishe mapenzi kwa Mtoto na kumsahau Mama yake)

Wajibika katika malezi ya Mtoto, wengi huacha kila kitu kwa Mama au Mama Mkwe. Mhudumie Mkeo/Mzazi mwenzio kwa ukaribu zaidi

Muweke Mzazi mwenzio kwenye ulinzi wa hali ya juu na hakikisha upatikanaji wa mahitaji kwa wakati
 
Upvote 1
Mmh kumbe kuna likizo ya uzazi kwa mwanaume?! Inakuwa ya muda gani na kipindi gani cha uzaz?! Ni yenye malipo?!
 
Akizaa mapacha sasa ndio inakua poa, munagawana kila mtu wake, wakati wa kunyonya tu munabadilishana
 
Mmh kumbe kuna likizo ya uzazi kwa mwanaume?! Inakuwa ya muda gani na kipindi gani cha uzaz?! Ni yenye malipo?!
Inatolewa hasa kwenye mashirika ya kimataifa.Inakuwa ya siku 30 tu na inatakiwa ichukuliwe kabla mtoto hajatimiza umri wa mwaka mmoja.Ni likizo ya malipo na haiathiri siku za likizo ya kawaida.
 
Inatolewa hasa kwenye mashirika ya kimataifa. Inakuwa ya siku 30 tu na inatakiwa ichukuliwe kabla mtoto hajatimiza umri wa mwaka mmoja.Ni likizo ya malipo na haiathiri siku za likizo ya kawaida.
Mmh kumbe kuna likizo ya uzazi kwa mwanaume?!
Kwa watumishi wa uma/ serikalini,Baba Mwajiriwa, utapewa siku tatu za likizo ya uzazi.

Zaidi pitia hii nukuu

"
Likizo ya uzazi kwa baba mwajiriwa. Sheria ya ajira inampa likizo ya siku zisizopungua tatu zenye malipo baba wa mtoto aliyezaliwa. Kwamba siku hizo zichukuliwe katika muda wa wiki moja ya kwanza tangu kuzaliwa kwa mtoto. Kwa kawaida likizo hiyo ya siku 3 hutolewa mara moja tu katika mzunguko wa likizo ya mwaka bila ya kujali idadi ya watoto watakaozaliwa katika kipindi hicho. Yaani likizo hii hutoka mara moja tu kila mwaka hata kama baba ana watoto alowapata zaidi ya mara moja katika mwaka husika.


Likizo inampa baba fursa ya kumhudumia mama na mtoto, kumsaidia mama kujenga msingi mzuri wa kumlisha mtoto na pia kutafuta mahitaji ya familia. Baba wa mtoto aliyezaliwa anaweza pia kupewa likizo isiyopungua siku 4 yenye malipo, wakati wa kuuguliwa na mtoto, kifo cha mtoto au kifo cha mwenzi wake. Likizo hiyo ya siku 4 hutolewa mara moja katika kipindi cha mzunguko wa likizo ya mwaka bila kujali idadi ya matukio yaliyojitokeza katika kipindi hicho. Hata hivyo, mwajiri anaweza kuidhinisha mwajiriwa kuchukua siku zaidi zisizo na malipo kulingana na tatizo alilopata.
"

1616511301123.png
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom