Rashidi Muya
New Member
- Jun 10, 2023
- 4
- 1
Kutokana na takwimu za sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2022 imeonesha kuwa Tanzania ina watu wapatao milioni 60+ ikiwa ni ongezeko la watu milioni 20+ kutoka sensa ya mwaka 2012, kwa mustakabari huo ongezeko la idadi ya watu linaenda sambamba na ongezeko la shughuri za kibinadamu katika mazingira yanayotuzunguuka ikiwemo kilimo, uvuvi, ufugaji, biashara pamoja na makazi. Vyote hivi kwa pamoja huathiri mazingira yetu kwasababu watu watalazimika kutumia ardhi iliyopo kwa ajili ya kufanyia shughuri zao ambapo sasa rasilimali miti hukatwa na uoto wa asili hupotea pamoja na viumbe hai vingine kutoweka katika mazingira hayo.
Kuongezeka kwa shughuri za kibinadamu hupelekea mabadiriko ya tabia nchi na kijiografia hasa kuwa na vipindi virefu vya jua na kusababisha ukame katika baadhi ya maeneo na hii ni kutokana na ukataji wa miti na kuchoma mkaa ili kupata nishati ya kupikia majumbani, kukata miti na kufyeka vichaka kwa ajili ya kupata maeneo ya kilimo yatakayo wafanya wazalishe mazao kwa lengo la kujipatia chakula na kipato ili kumudu gharama nyingine za maisha.
Kuongezeka kwa idadi ya watu na makazi hasa katika maeneo ya miji mikubwa imepelekea kuwe na ongezeko kubwa la uzalishaji wa taka ambazo zimekua zikitupwa hovyo na kuzagaa katika makazi ya watu na kuchafua mazingira kutokana na kukosa mpangilio sahihi wa sehemu za kuhifadhiwa kitu ambacho huzifanya kipindi cha mvua kusombwa na maji na kutupwa mitaroni na kisha huziba mitaro hiyo na kusababisha maji kukosa njia na kutapakaa katika makazi ya watu na kuleta adha kwa wananchi.
Katika mikakati ya kuijenga Tanzania tuitakayo kwa miaka inayokuja serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanatakiwa kushirikiana na kushikamana katika suala la kuyaweka mazingira katika hali iliyo salama kitu ambacho kitasaidia kupungua kwa majanga ya kijiografia ambayo baadhi yao husababishwa na shughuri za kibinadamu.
Ili tuijenge Tanzania tuitakayo mambo yafuatayo yanapaswa kutiliwa mkazo na kupewa kipaumbele;
1: Serikali ikishirikiana na wadau wengine wapenda maendeleo wanatakiwa kuweka kipaumbele suala la elimu ya mazingira na umuhimu wa utunzaji wa mazingira na elimu hii itolewe kwa watanzania wote wa mijini na vijijini kwasababu ukosefu wa elimu ya kutosha kuhusu mazingira na umuhimu wake katika maisha yetu ya kila siku ndio husababisha wananchi kutozingatia au kutoyapa kipaumbele mazingira yetu na kujikuta wakitupa taka hovyo, wakikata miti na kufyeka vichaka ili kuchoma mkaa na kutengeneza maeneo ya kilimo pamoja na makazi pasipo kujua wanaharibu bionuai ya kijiografia na kupoteza makazi ya viumbe hai vingineo. Kwahiyo elimu inapaswa kutolewa ili watu watunze mazingira na kuacha shughuri za ukataji miti hovyo.
2: Serikali imekua ikijitahidi kuhimiza matumizi ya nishati safi ya gesi katika shughuri za majumbani lakini jitihada hizi zitachukua muda mrefu kufanikiwa katika maeneo mengi ya vijijini ambako matumizi ya kuni na mkaa yamekua makubwa sana kwasababu misitu na miti ipo karibu hivyo haiwahitaji kutumia gharama yoyote kupata nishati hiyo, hivyo basi ili juhudi hizi za serikali ziweze kufikia malengo serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya wizara ya nishati inapaswa kukaa na wadau wanaosambaza nishati ya gesi waone ni kwa namna gani wanaweza kupunguza gharama za gesi kitu ambacho kitaongeza uhitaji wa nishati hii kwa wananchi na hata yule mtanzania wa hali chini atashawishika kununua na kutumia nishati ya gesi na kuachana na matumizi ya mkaa na kuni ili tuweze kutunza mazingira.
3: Serikali kwa kushirikiana na washirika wengine katika ngazi za mkoa na wilaya wanatakiwa kutenga bajeti ya fedha kwa ajili ya vitalu vya kuoteshea miti ya aina tofauti tofauti ambayo itagawiwa kwa wananchi mbalimbali kwa ajili ya kupanda kwenye maeneo yao lengo ni kuongeza idadi ya miti katika mazingira ambayo itasaidia suala la kutunza mazingira yetu lakini pia serikali kwa kushirikiana na hao washirika wanapaswa kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya kupandia miti hiyo lengo ni kuendeleza misitu ya kupanda ambayo itasaidia katika suala la uboreshaji wa mazingira yetu.
4: Katika suala la uzalishaji taka pamoja na kuzagaa kwa taka hovyo hapa serikali inayo majukumu makubwa sana ya kufanya ili kuwez kukabiliana na tatizo hili ambalo ni kero katika mazingira, serikali inapaswa kuja na sheria kali zitazotekelezwa kwa wote watakaokiuka maagizo ya namna ya utupaji wa taka hizo, serikali inapaswa kuja na mifumo maalumu ya ukususanyaji wa taka hizo kabla ya kupitiwa na gari la taka na kwenda kutupwa sehemu zilizotengwa kwa ajili ya utupaji taka na katika hiyo mifumo sasa inapaswa kuwa ya matenki makubwa (dustbins) yatakayotengwa kwenye maeneo ya makazi ya watu hasa barabarani ili watembezi kuweza kutupa taka zao humo na sio kuzitupa kiholela na matenki hayo yanapaswa kufuatilia kila mwisho wa wiki ili taka zilizomo zitolewe na kuweka nafasi ya nyingine kukusanywa huku utaratibu wa magari ya taka kupita majumbani kwa watu kukusanya taka ukitakiwa kutiliwa mkazo kwasababu kumekua na tabia ya magari kupitisha hadi miezi miwili pasipo kupita kuchukua taka. Lakini pia serikali inatakiwa kuja na mkakati bora wa kuona ni namna gani taka zinazowezwa kubadirishwa matumizi basi zibadirishwe hata kama ni kutengeneza mbolea za mashambani kwa zile zinazowezekana lengo ni kupunguza mrundikano wa taka katika maeneo yaliyotengwa kutupia taka.

Upvote
1