Mambo yanayo kufanya uwe mswahili...

Gudboy

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2009
Posts
867
Reaction score
82
1.Unamwita mtu usiyemjua(wala kukutana nae kabla)aunt au anco.
2.Asilimia 90 ya CD pamoja na cassete za muziki ulizonazo nyumbani ni feki (sio original copies).
3.Stooyako imejaa vitu (makorokoro) kwa kuwa hutupi kwa kuamini kuwa ipo siku utayahitaji kwa mfano karpet ukilitoa hulitupi n.k.
4.Una machupa ya maji matupu ya shampoo perfume pamoja na vipodozi vingine umeweka tuu wala huna shughuli navyo.
5.Watoto wako wote wana majina ya utani mfano babu ali,chidi,mamu,dida n.k.
6.Hakuna mtu katika familia yako anayetoa taarifa kwako anapo kuja kukutembelea mfano kaka,shangazi n.k.
7.Mifuko yako imejaa vitu kama vile vijiti vya kusafishia meno,tissue n.k ulivyochukua sehemu kama vile mgahawani.
8.Mama yako anamigogoro na ndugu na hawazungumzi kwa muda wa siku 10au zaidi.
9.Hupigi simu isipokuwa katika
muda ambao gharama za kupiga ni nafuu(mfano usiku sana )na mara nyingi huwa una beep
tu.

10.Ulipokua mdogo nguo unazonunuliwa pamoja na viatu ni vikubwa mara mbili ili uweze kuvivaa muda mrefu zaidi.
11.Wakati ukisafiri na ndege unabeba mzigo wa uzito mkubwa kuliko inavyoruhusiwa.
12.Unapomsaidia mtu na akafanikiwa basi utakuwa unasema kama sio mimi asingekuwa vile yule.
ila kuna ka ukweli jamani
 
Kuanzisha THREAD yenye 'taarifa za uswahili'
 
Ha ha ha ha nimecheka mpaka basi,halafu ni kweli tupu,ingawa in touch
 
Haaaaa ! hii kweli kabisa
bado moja " unapoulizwa swali nawe unauliza badala ya kujibu au kusema sijaelewa"
 
Kuna mengi umesahau;

* unapenda kujua mambo ya wengine yasiokuhusu a.k.a umbeya
* unaeneza mambo/tambala au habari ambazo si za kweli
* unakwenda kwa watu bila kukaribishwa (haswa wakati wa mlo)
* unapenda kusema kuwa huna pesa wakati unazo
 
pindi unapojisikia maumivu unapenda kunywa dawa bila kupata ushauri wa daktari
 
  • kuongea kwa sauti kubwa katika daladala mambo yako binafsi.
  • kuimba wimbo kwa sauti ya juu ili wengine waone unauelewa sana.
  • kuwatangazia watu kwamba umejenga (hukai nyumba ya kupanga).
  • kuweka kandambili mlango wa ******.
  • kutundika meseji za mafumbo sebuleni.
  • kuandika meseji za ajabu katika magari.
  • kuwa na madeni baaa na kwa mama ntilie.
  • kupiga mswaki hadharani huku umejifunga kijitaulo.
 
.kupenda kujua jirani yako leo kala/kapika nini.?
.kupenda vitu vya gharama kuliko uwezo wako binafsi.
 
-Kupenda kukojoa pembezoni mwa barabara
-kununua vitu njiani na kuanza kula
-kuuza biza chini na hasa pembeni mwa barabara
-kununua bidhaa sehemu zisizo rasmi
 
ukipanda daladala za uswazi kama mbagala na uko sopusopu basi unajifanya hujui vituo eti unamuuliza jirani yako 'hapa wapi?, tukifika sehemu flani nistue sikufahamu kabisa'!!.
 
badala ya kumuambia jirani karibu tule unamuambia karibu twala.
 
- Hujali usafi wa mazingira ya nyumbani kwako bali unapenda kujikwatua na kuvaa vizuri uonekane na watu hata ikibidi kuazima kuanzia nguo, viatu hadi hereni, mikufu na mapambo mengine
- Kama ni mwanamama unapenda sana kukaa barazani kuangalia wapitao
-Kuvaa khanga zenye maneno ya mipasho na kupiga miziki ya taarabu ya mipasho
 

ha ha ha ha yaani umenikumbusha mbali sana
na hiyo kupiga mswaki hadharani huku umejifunga taulo.....yaani
 
....kupenda kutazama filam za kanumba na wenzie
....kupenda kuponda watu waliokuzidi kipato
 
ukipanda daladala za uswazi kama mbagala na uko sopusopu basi unajifanya hujui vituo eti unamuuliza jirani yako 'hapa wapi?, tukifika sehemu flani nistue sikufahamu kabisa'!!.



-we nawe mswahili nani kakwambia kuuliza ni ujinga?
 
1.Kuwa na nyumba ndogo.
2.Kuwa na wivu kwa mkeo.
3.Kuweka simu kwenye silence hasa ukiwa na mkeo.
4.Kuandika majina ya uongo kwenye address book ya simu yako.
 
-Kunywa Soda/bia (chupa moja)kwa mda wa saa nzima
-Kuongea kwa sauti kubwa kwenye simu!
-Kubipu
 
*Kuangalia mwanamke ambaye si wako akipita mpaka aishie haswa wakati ana bonge law....
*Kupiga mziki kwa sauti ya juu mpaka nyumba ya nne mtaani wajue una mziki gani mtaani
*Kutamani/Kuwa na wanawake zaidi ya 3 kwa pamoja
*Wanawake kuvalia khanga zenye maneno ya kusutana hata wakati wa msiba
*Mwanamke kutaka kuhongwa hata kama yy ndie mwenye kipata zaidi.
*Hata uwe umesoma kiasi gai kukubali kuongopewa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…