Mambo yanayochangia mume kutembea na hausigeli

Mambo yanayochangia mume kutembea na hausigeli

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
attachment.php

NI siku nyingine tulivu kabisa tunakutana tena kupitia safu hii nikiamini umzima bukheri wa afya na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku.
Mimi nitakuwa mchoyo wa shukurani kama sitachukua nafasi hii kumshukuru Mungu kwa mema ambayo amekuwa akinitendea katika kila siku ya maisha yangu.

Ndugu zangu, malalamiko ya baadhi ya mabinti wanaofanya kazi za ndani ‘mahausigeli’ kuwazidi kete baadhi ya wanawake kwa kuwachukulia waume zao yamekuwa yakiripotiwa kila mara.
Si ajabu hata wewe unayesoma makala haya aidha umeshawahi kumsikia rafiki kama siyo jirani yako akikorofishana na hausigeli wake au kushuhudia hausigeli akifumaniwa na bosi wake.

Hakika ni matukio ya aibu sana. Inafika wakati unajiuliza inakuwaje mume anamtongoza na hatimaye kutembea na hausigeli wake? Ameshawishiwa na kitu gani au amekosa nini kwa mkewe mpaka anafikia uamuzi huo?
Kimsingi linapotokea tukio kama hili, wengi hujiuliza maswali mengi sana na majibu yake huwa ni magumu kupatikana. Hii ni kwa sababu ni jambo lisilotarajiwa kufanywa na mtu aliyestaarabika. Hata hivyo, tuna kila sababu ya kujua chanzo cha tatizo hili.
Nitajaribu kuzungumzia kipengele kimoja baada ya kingine kuhusiana na yapi yanayotajwa kuwasukuma baadhi ya wanaume kutembea na mahausigeli wao.

Wanawake wanajitakia
Ni jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa sana na baadhi ya watu kuwa, inakuwaje hausigeli anapewa majukumu ya kumhudumia mume wakati mke yupo?
Ni ukweli usiofichika kwamba, kuna baadhi ya wanawake ni malimbukeni wasiojua jinsi ya kuitunza ndoa. Hawajui namna ya kumshika mume na kumuepusha na vishawishi vinavyoweza kumfanya akamsaliti.
Ndugu zangu, kitendo cha mke kumruhusu hausigeli amfulie mumewe nguo zake za ndani, amuandalie chakula, ampelekee maji ya kuoga na mambo mengine kama hayo ndivyo vimekuwa vikichochea usaliti huu.
Kama mke hataki kusalitiwa kirahisi basi ajitahidi sana kuchukua jukumu la kufanya yale ambayo kwa kiasi kikubwa yakifanywa na hausigeli huweza kujenga ukaribu wa kimapenzi kwa mumewe. Kamwe usibweteke, ukibweteka hausigeli wako atakupindua na itakuwa ni aibu kwako.

Mahausigeli micharuko
Hivi inaingiaje akilini mke kuridhia kumuajiri hausigeli ambaye kwa macho tu anaonekana hajatulia? Unamuajiri hausigeli ambaye siku ya kwanza tu anataka umpe sehemu ya mshahara wake akafanye ‘shopping’ halafu unakubali, unajitaka kweli?
 
Attachments

  • MAHABA.jpg
    MAHABA.jpg
    48.5 KB · Views: 3,301
MAMBO YANAYOCHANGIA MUME KUTEMBEA NA HAUSIGELI-2

Utakumbuka nilianza kuzungumzia mambo yanayotajwa kuchangia baadhi ya wanaume kutembea na wafanyakazi wao wa ndani ‘mahausigeli’.

Ni mada iliyoonekana kuwagusa wengi na huenda ni kutokana na ukweli kwamba, matukio ya baba kufumaniwa akifanya dhambi na hausigeli wake yamekuwa yakishamiri sana huko mtaani.
Wapo walionipigia simu na kuniambia si kwa wanaume tu bali kuna wake za watu nao wamekuwa wakifanya mapenzi na ‘mashamba boy’ wao, hilo

nalo tutalizungumzia siku zijazo ila kwa leo tumalizie kwanza yale ambayo huwafanya waume za watu kutembea na mahausigeli wao.

Kama uko sambamba na mimi utakumbuka niliishia pale ambapo niliwataja mahausigeli mcharuko. Wapo mabiniti ambao walianza kujihusisha na vitendo vya ngono tangu walipokuwa wadogo.

Kuna ambao walipitia biashara ya uchangudoa na baada ya kushindwa huko wakaingia mtaani na kuanza kutafuta kazi za ndani.
Ukijichanganya na ukakutana na kabinti kazuri ambako kalipitia uchangudoa na ukaamua kukaajiri kama kahausigeli kako, mambo hayawezi kuwa sawa. Mumeo atategwa na mwisho atashawishiwa kukusaliti.

Sasa inaingiaje akilini mke kuridhia kumuajiri ‘hausigeli’ ambaye kwa macho tu anaonekana hajatulia? Unamuajiri hausigei ambaye siku ya kwanza tu anataka umpe sehemu ya mshahara wake akafanye ‘shopping’ halafu unakubali, unajitaka kweli?
Hujiulizi ana sababu gani ya kununua lotion, pafyumu na nguo tena za kimitego wakati ndiyo kwanza anaanza kazi? Anataka ampendezee nani kama siyo kumtega mumeo?
Kimsingi kuna hawa wafanyakazi ambao ukikubali wawe wasaidizi wako ndani ya nyumba watakusaidia hadi ‘kumhudumia’ mumeo. Kikubwa ni kuangalia yupi ana vigezo vya kuwa hausigeli wako na yupi hafai.

Mke kutojali
Kuna wanawake wengine naweza kusema hawajali, yaani hata wakiona dalili za wazi kwamba wanachukuliwa waume zao, wanachukulia poa tu. Hivi utakuwa ni mke makini kweli kama utamruhusu hausigeli wako akae akiangalia TV sebuleni na mumeo wewe ukiwa chumbani umelala?
Ni sahihi kweli mke kusafiri na kumuacha mumewe na hausigeli, wawili tu ndani ya nyumba ambayo si ya kupanga? Je, ni sahihi mume kwenda ‘out’ na hausigeli huku mke akibaki nyumbani?
Kwa mke makini hawezi kukubaliana na mazingira hayo lakini kama hujui wapo wanawake wa ajabu ambao wala hawaoni hatari kuwaachia waume zao kuwa na ukaribu huo na wafanyakazi wao wa ndani. Sasa katika mazingira hayo unatarajia nini?

Wanaume ambao hawajatulia
Kuna waume za watu wengine wamekuwa na tamaa za kijinga sana kiasi cha kufikia kuwashawishi mahausigeli wao wawape penzi. Hili limekuwa ni tatizo kubwa na kimsingi mke anapobaini kuwa mumewe anamsumbua mfanyakazi wao, hatua za haraka zichukuliwe.

Nimeimaliza mada hiyo, tukutane tena wiki ijayo kwa mada nyingine.

kweli mwanaume anaetembea na hauz girl.huyo siyo mwanaume original au wa kweli bali ni mwanaume jina tuu.ni mwanaume kwajili anavaa suruale.hata kama ni mke mzembe.au ana shida zake bora utafute.mwanamke aliye mbali na mtaani kwako.kwani hauz gel lazima ijulikane cku moja.mbona kuna wanawake kila kona?hauz gerl kujizalilisha na kuzalilisha mkeo na familia.kama ni kubadili mapishi nenda hata kwenye danguro lipia gonga then chapa mwendo hapo hakuna deni.ila hauz gel hapo utachonga mzinga.na mwanaume wa kweli hachongi mzinga ni kugonga na kuchapa mwendo.
 
Ndugu zangu, kitendo cha mke kumruhusu hausigeli amfulie mumewe nguo zake za ndani, amuandalie chakula, ampelekee maji ya kuoga na mambo mengine kama hayo ndivyo vimekuwa vikichochea usaliti huu.

Mzizi, hizo sababu nilizo-highlight hapo juu sijawahi kukubaliana nazo na sitegemei kubadilisha huo msimamo kwa sababu sio sababu za msingi.
Ni kweli si sawa kwa housegirl kukufulia nguo zako za ndani, lakini inakuwaje mwanaume uache shuguhli za msingi na kuanza kufatilia nani anaefua nguo zako? Je, kwa yeye kufua kunaamsha vipi hisia zako za mapenzi? Akikuwekea maji bafuni (lazima itakuwa bafu za nje) hilo linachangia vp?

Unajua kuna watu hawarudii nguo za ndani (so hamna kufua), wanatumia washing machines na bado hg anapigwa kawaida?

Mambo mengine huwezi kuzia ila unaweza kupunguza

1. Kwanini uchukue beki tatu Bomba Mbayaaa! Kisu cha Hatari jishepu kama Agness Masogange afu utegemee Mumeo asisababishe! Aaaaaah wappi! Ukimkabidhi Fisi bucha hata kama kashiba kuonja sunna. Chuku dada pande la mtu, mweusi tiii, Nido saa kumi jioni. Hata Hubby akimuona tu ANAREPEL! automatically.

2. Ndumbaaaaaaa! Mabeki tatu wengi sanaa wanatumia kiringe kuchukua waume za watu, akipika lazima atie black science kidogo. Utatupiwa virago hivi hivi unajiona. Au kila siku ugomvi hauishi mumeo, kitu cha Nuksi hicho ushatupiwa na beki tatu.

3.Mavazi unayomruhusu beki 3 wako. Yaani unamuachia kabisaa beki 3 apige tight, mara pensi, mara mini, inaonesha umesahau seein is believing! Hubby akiona ule mpaja umenona nona lazima abelieve there is more in there! Apige sketi za marindaaaa na tshirt.

4. Mazoea na mumeo! Yaani unaruhusu kabisa wakae wapige story, eti hela ya matumizi amuombe mumeo we mama upo tu, Alaaaaaaaaa! Humo humo kunako mazoea anachakachuaamo!

All in all kikulacho ki nguoni mwako! Na asilimia kubwa sanaa ya wanaume ni n.y.o.k.o (Take it as a compliment) vibayaaa mno, wako rijali kweli kweli! So kumfuga beki tatu bombaaa kakuzidi, afu unamruhusu apige vicataloge, afu ukete maza house gangstar mwenzio full kujicream, udi na nini lazima Mapinduzi bubu yatokee!

Nae pi mwanamke atii, she got same needs as you the wifey!!!!!!!!!!!

All im sayin is dont patronise with the enemy! You better give her prior notice that jst incase you sense she is double crossin you somebody will surely get shot! And it aint your dear husband!
 
kweli mwanaume anaetembea na hauz girl.huyo siyo mwanaume original au wa kweli bali ni mwanaume jina tuu.ni mwanaume kwajili anavaa suruale.hata kama ni mke mzembe.au ana shida zake bora utafute.mwanamke aliye mbali na mtaani kwako.kwani hauz gel lazima ijulikane cku moja.mbona kuna wanawake kila kona?hauz gerl kujizalilisha na kuzalilisha mkeo na familia.kama ni kubadili mapishi nenda hata kwenye danguro lipia gonga then chapa mwendo hapo hakuna deni.ila hauz gel hapo utachonga mzinga.na mwanaume wa kweli hachongi mzinga ni kugonga na kuchapa mwendo.

Na hawa mahauz gels wataliwazwa na nani jameni?? Maana kutwa tumewabana hawana hata off!!

Houz gel nae mtu na anahitaji kuliwazwa japo siku moja moja
 
Hii mada imekaa vizuri, inabidi isomwe na watu wote walio ndani ya ndoa na wale wanandoa watarajiwa.

Ndiyo maana huwa wasiwaelewi wanaopiga vita magazeti ya udaku halafu akasapoti mada hii, maana mimi nimekuwa nikiifuatilia toka mwanzo kupitia gazeti la AMANI, "Only God can".
 
Na hawa mahauz gels wataliwazwa na nani jameni?? Maana kutwa tumewabana hawana hata off!!

Houz gel nae mtu na anahitaji kuliwazwa japo siku moja moja
Inaonekana una huruma sana, basi mpe mwanao wa kiume la kama huna hata ndugu yako yoyote wa kiume amfariji.

Acha kupalilia Uzinzi ndani ya ndoa takatifu.
 
MziziMkavu swala la kupendeza ni la kila mtu huwezi kusema housegirl anampendezeshea nani cha msingi mavazi hayo anayovaa yasiwe yakumtia mwanaume majaribuni na hili liko mikononi mwa mke usitegemee mme wako aanze kukemea mavazi kwa housegirl wakati unakenua meno kwamba akivaa tight huyo housegirl unasema anapendeza.......imenenwa "....mwanamke avae mavazi ya kusitiri..na mavazi ya kukosesha wengine ni chukizo kwa Bwana"
 
Mambo mengine huwezi kuzia ila unaweza kupunguza

1. Kwanini uchukue beki tatu Bomba Mbayaaa! Kisu cha Hatari jishepu kama Agness Masogange afu utegemee Mumeo asisababishe! Aaaaaah wappi! Ukimkabidhi Fisi bucha hata kama kashiba kuonja sunna. Chuku dada pande la mtu, mweusi tiii, Nido saa kumi jioni. Hata Hubby akimuona tu ANAREPEL! automatically.

2. Ndumbaaaaaaa! Mabeki tatu wengi sanaa wanatumia kiringe kuchukua waume za watu, akipika lazima atie black science kidogo. Utatupiwa virago hivi hivi unajiona. Au kila siku ugomvi hauishi mumeo, kitu cha Nuksi hicho ushatupiwa na beki tatu.

3.Mavazi unayomruhusu beki 3 wako. Yaani unamuachia kabisaa beki 3 apige tight, mara pensi, mara mini, inaonesha umesahau seein is believing! Hubby akiona ule mpaja umenona nona lazima abelieve there is more in there! Apige sketi za marindaaaa na tshirt.

4. Mazoea na mumeo! Yaani unaruhusu kabisa wakae wapige story, eti hela ya matumizi amuombe mumeo we mama upo tu, Alaaaaaaaaa! Humo humo kunako mazoea anachakachuaamo!

All in all kikulacho ki nguoni mwako! Na asilimia kubwa sanaa ya wanaume ni n.y.o.k.o (Take it as a compliment) vibayaaa mno, wako rijali kweli kweli! So kumfuga beki tatu bombaaa kakuzidi, afu unamruhusu apige vicataloge, afu ukete maza house gangstar mwenzio full kujicream, udi na nini lazima Mapinduzi bubu yatokee!

Nae pi mwanamke atii, she got same needs as you the wifey!!!!!!!!!!!

All im sayin is dont patronise with the enemy! You better give her prior notice that jst incase you sense she is double crossin you somebody will surely get shot! And it aint your dear husband!
Unajaribu kushindana na Ulimwengu wa roho chafu kwa kutumia silaha za kimwili, ushindi sahau..

  1. Unaweza kusema nikimleta beki tatu mbaya ndiyo hatapendwa na baba mwenye nyumba, jiulize kwani wanawake wabaya wa sura au weusi tii kama ulivyosema hawana wanaume?
  2. Hata kama ukiweka sheria za kuvaa magunia nyumbani badala ya nguo za kawaida, kama huyo beki tatu na baba mwenye nyumba hawajatulia hilo gunia la beki tatu litavuliwa tu na ndipo utakapoachwa mdomo wazi.
  3. Hata kama ukizuia mazoea ya wao kukaa pamoja na kupiga stori kama beki tatu na huyo baba mwenye nyumba wameamua kukengeuka wataweza tu, siku hizi mambo yapo kidijitali zaidi. Mume anaweza kuwa yupo kazini lakini bado akaweza kuchati na beki tatu kwa SMS. Whatup nk. Wakifika nyumbani ni kukamilisha waliyoyapanga mchana kutwa tu. Utachoka siku utakapowafuma wakila tunda wakati muda wote wakati wewe upo baba yupo siriasi na beki tatu naye anajifanya kuwa mbali na mumeo.
  4. Kumbukeni, kama huyo beki tatu ameamua kwa dhati kabisa kutumia ndumba kumnasa baba mwenye nyumba, hakuna sheria, kanuni wala taratibu za nyumba zitakazoweza kuzuia, bali ni kwa Dua na Sala siku zote tukimtegemea Mungu ambaye ndiye muasisi wa ndoa atailinda mwenyewe. Period!
 
Back
Top Bottom