Mambo yanayofanana kuhusu maisha ya Marais wa Marekani Abraham Lincoln na John Kennedy: Je, haya yalitokea kwa bahati tu au kuna jambo tofauti?

Mambo yanayofanana kuhusu maisha ya Marais wa Marekani Abraham Lincoln na John Kennedy: Je, haya yalitokea kwa bahati tu au kuna jambo tofauti?

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Ni hivi, watu hawa wawili ni miongoni mwa viongozi maarufu zaidi katika orodha ya Marais wa Marekani. Abraham Lincoln na John F. Kennedy kila mmoja aliongoza Marekani na kupitia baadhi ya misukosuko mikubwa katika historia za uongozi wao. Mauaji yao yalitikisa siyo tu Marekani, bali dunia mzima.

Hapa nakupa baadhi tu ya mambo mengi yaliyowakuta Lincoln na Kennedy ambayo watu wengi wanazungumza kwamba yanafanana kwa namna ya kushangaza.

Mnamo Agosti 1964, Jarida la Kamati ya Wabunge wa Chama cha Republican lilichapisha orodha ya kile ambacho Time magazine ilikiita "mkusanyiko wa mambo ya kushangaza" katika maisha na vifo vya Abraham Lincoln na John F. Kennedy

Matukio mengi yanayofanana kati ya Lincoln na Kennedy yanahusu herufi na namba. Kwa mfano, majina Lincoln na Kennedy kila moja lina herufi saba. Na walichaguliwa kwanza kuwa wabunge kisha kuwa marais kwa tofauti ya karne moja kamili: Lincoln mnamo 1846 na 1860, Kennedy mnamo 1946 na 1960.

Wote wawili walipigwa risasi kichwani kutokea kwa nyuma siku ya Ijumaa, na wote walifariki kutokana na majeraha yao. Na haya matukio yote haya mawili yalitokea katika sehemu zinazohusiana na herufi "PH," yaani Petersen House kwa Lincoln na Parkland Hospital kwa Kennedy.

Unaweza kufuatilia visa vya maisha yao kisha ukatupa mtazamo wako kuhusu matukio ya maisha yao. Unadhani yaliyotokea ni bahati tu au kuna jambo tofauti?

 
Back
Top Bottom