#COVID19 Mambo yanayofikirisha kuhusu chanjo ya UVIKO-19

#COVID19 Mambo yanayofikirisha kuhusu chanjo ya UVIKO-19

6321

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2016
Posts
649
Reaction score
1,117
Nawasalimu kwa jina la JMT.

Binafsi ni miongoni wa watu waliochoma chanjo dose ya kwanza yapata miez mi 3 sasa. Kwa upande wangu binafsi sikuwa na mategemeo ya kuchoma chanjo hii ila kulikokea push factors ikabid nichome na nategemea kabla mwaka haujaisha nimalizie dose.

Hadi leo hii sijaona side effects zozote za chanjo hii mwili uko kawaida kabisa, lakin kwa siku 3 au 4 baada ya kuchoma sikuwa na hamu ya kula, na uchovu ulikuwepo wa kiasi.

Haya twende kwenye hoja ya msingi, ambayo chanjo ya korona imefanya nianze kujitafakari juu ya hii chanjo.
1. Rafiki yangu ambae ni nutrition consultant wa org ya kimataifa kuniambia anaumwa covid lakin alikwisha choma dose zote mbili.

2. Kuvaa barakoa na kukeep distance huhali watu hao wamechoma chanjo zote mbili.

Lakin la mwisho ni hili kuhusu team ya Totenham ambayo mechi ya juzi ili post sababu ya wacheza wa 5 wa Tot wamekutwa na virusi vya korona.

Hayo ni baadhi ya mambo yanayonitafakarisha kuhusu chanjo ya korona, na inaniwia ugumu kumalizia dose japo nina deadline ya kusubmit cheti cha dose ya 2 mwaka huu.

Je ni yapi yanakutafakarisha kwenye covid vaccin?
 
Fuckin vaccin
FB_IMG_1639562436263.jpg

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
1.Ya kwamba hata ukichanja haikuzuii kuugua Covid 19
2.Kuibuka kwa variant mbalimbali za Virusi hivi!!
3.Kuwepo kwa Variant inayokwepa mishale ya chanjo!!!
4.Kwamba ukichanja lazima upate booster.
5.Ukichanja Vaa barakoa, Na usipochanja vaa barakoa.
Kwamba kuugua Covid 19 hakukusaidii kutengeneza kinga, ila sindano ndio njia pekee ya kukutengenezea kinga.
Kwa leo asubuhi hii hizi ndizo tafakuri zangu.
 
Hii chanjo ina visa sanaa, imekaa kibiashara zaid

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Tulishaambiwa tutafute namba ya kuishi na huu ugonjwa kama ilivyo mafua na malaria.

Kama watu wako fit hadi wanajiandaa na mechi ila vipimo ndio vinaonyesha wanamaambukizi ya Covid si waachwe tu!

Unafikiri tukipimwa nchi nzima sasa hivi wangapi watakutwa na maambukizi? Wengi wanamaambukizi ila madhara ya ugonjwa yamepungua nguvu sana.

Sasa hivi kinachopigiwa chapuo ni biashara tu. Zitaendelea series za jab balaa.

Kuchanjwa iendelee kuwa hiari ila uhamasishaji uendelee tusijekukosa misaada.
 
Nachojiuliza sasa kuna wimbi la nne eti, nchi yetu inapokea tu chanjo je zinasaidia kudhibiti kirusi kipya
 
Nachojiuliza sasa kuna wimbi la nne eti, nchi yetu inapokea tu chanjo je zinasaidia kudhibiti kirusi kipya
Wanasema chanjo inapunguza kutopata madhara makubwa[emoji57]
Screenshot_20211217-141114.jpg

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Attachments

  • Screenshot_20211217-141114.jpg
    Screenshot_20211217-141114.jpg
    47.5 KB · Views: 2
Back
Top Bottom