JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Uandishi wa kiuchunguzi ni aina ya uandishi inayohusisha utafiti wa kina na makini, ukweli, na na mahojiano ili kupata takwimu za kutosha. Pia inahusisha matumizi ya zana na teknolojia za kuvumbua mambo, kama kamera na vinasa sauti vya siri.
Ripoti ya uchunguzi inahusu kuleta ukweli mbele ya umma, ambao umma haujui.
Ripoti iliyotolewa na Tanzania Media Foundation (TMF) 2017, inaeleza changamoto zinazokabili waandishi wa habari za uchunguzi Tanzania kuwa ni pamoja na:-
Kuwepo kwa sheria zinazoharamisha kufichua maovu ya mtu au mamlaka fulani ikitajwa kuwa ni udhalilishaji na uchochezi, mfano sheria ya uhalifu wa mtandao (2015), Sheria ya Takwimu (2015) na Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari (2016) zinawabana sana waandishi wa habari za uchunguzi Tanzania.
Uandishi wa habari za uchunguzi wakati mwingine unahitaji fedha na Rasilimali nyingi na mda mrefu hutumika ili kukamilika ila ni vyombo vichache vya habari ambavyo viko tayari kumfadhili mwandishi kufanya habari hizo kutokana na uhaba wa fedha.
Uwezo wa Uandishi wa Habari, mfumo wa elimu nchini Tanzania hauandai watu wa kutosha kujiunga na taaluma hiyo. Wengi wa waandishi wa habari wana kiwango cha diploma hali inayoleta ugumu kwenye habari hizo zinazohitaji weledi wa hali ya juu.
Njia za kuondoa changamoto hizo ni pamoja na kupewa misaada ya kifedha kutoka mashirika ya kimataifa na wanafunzi kupata elimu ya kutosha kuhusu sheria zinazoongoza utendaji wao.
Upvote
0