Uchaguzi 2020 Mambo yanayotafakarisha kuelekea Uchaguzi Mkuu

Uchaguzi 2020 Mambo yanayotafakarisha kuelekea Uchaguzi Mkuu

sammosses

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2011
Posts
1,687
Reaction score
1,111
Tanzania ipo kwenye kipindi kigumu sana kuelekea uchaguzi mkuu, ni kipindi cha dola kuwa chama cha siasa na chama cha siasa kuwa chama dola zaidi.

Naiona hofu ya uchaguzi iliyobebwa na ulimbukeni wa kimamlaka. Hii ni hatari sana kwa karne hii ya 21. Katiba ya Jamhuri ya Muungano ina kanyagwa hadharani.

Mamlaka ya kikatiba inayotoa haki mbalimbali inaporwa, ndiyo maana leo katika CCM ile ile ya mwaka 1961 iliyopendwa na kila Mtanzania ina chukiwa na kila Mtanzania wa miaka ya 2015/2020.

Eti kuimba wimbo wa Taifa ukiwa umebeba bendera ya chama cha siasa ni haramu lakini kuimba ukiwa umebeba mpira au vifaa vya michezo ruksa!

Kwa mara ya kwanza Mwenyekiti wa chama cha siasa ana agiza jeshi la polisi kumpa shortlist ya wagombea wa upinzani.

Mamlaka hii kaitoa wapi, hivi kweli Watanzania wamekuwa wajinga wasiojua separation of power maanake nini

Mbona kila inapoelekea uchaguzi kuna kuwa na mambo ya ajabu yasiyo zingatia sheria, au hamjui Tanzania ni nchi yetu sote!

Jaji Mkuu alisema kuwa ipo haja ya kuziangalia sheria kandamizi zinazo pora haki,uhuru na usawa kwa wananchi, lakini hatujiulizi ni lini mtu mmoja ataendelea kuwa na mamlaka hata yasiyo ya kikatiba kwa maslahi binafsi!

Tunapoelekea kwenye siasa za uchaguzi tujifunze kuielewa katiba yetu kwa kuitumia ibara ya 8 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano ipasavyo kwa kuwa mamlaka na madaraka ya serikali yanatoka kwetu.

Tukiendeleza kanuni ya uoga kwa unyenyekevu bandia tutaumiza future za vizazi vyetu, lakini tutarudisha utumwa rasmi usio zingatia haki za binadamu.

Ukielewa haki na thamani ya kura yako kwa kusikiliza sera shindanishi hakika utaijuwa thamani na mamlaka yako kikatiba, Mtanzania amka sasa saa ya maamuzi sahihi imefika.
 
Natamani watanzania wangekuwa wanaelewa kama wewe. Kweli tunaharibu taifa letu sana kwa mambo haya ya kishabiki na unafiki wenye lengo la kujipatia upendeleo wa kisiasa. Udikteta unaendelea ukikubalika zaidi nchini, kufanya mambo bila kufuata sheria imekuwa ni ugonjwa mbaya unaokuwa kila siku.
 
Back
Top Bottom