JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Mambo yanayotakiwa Kufanywa na Vyama vya Siasa Mambo yanayotakiwa kufanyika wakati wa upigaji kura mpaka kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi ni pamoja na-
(a) vyama vya siasa na wagombea kuhakikisha kuwa mawakala wao wanakula kiapo cha kutunza siri siku saba kabla ya upigaji kura;
(b) mawakala wa vyama vya siasa, vyama vya siasa, wagombea na watendaji wa uchaguzi wanashirikiana katika vituo vya kupigia kura kwa kuzingatia sheria, kanuni na maelekezo ya Tume.
Hii, itawezesha zoezi la upigaji kura kuendeshwa kwa amani na utulivu;
(c) viongozi wa vyama vya siasa watawaelimisha na kuwasisitiza wanachama wao kuwa, mara wanapomaliza kupiga kura waondoke vituoni ili kuepusha msongamano na vitendo vinavyoweza kuchochea uvunjifu wa amani;
(d) mawakala wa vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi kuruhusiwa kusindikiza masanduku ya kura
hadi kufikishwa mahali pa kujumlishia kura kwa kuzingatia maelekezo ya Tume; na
(e) kila chama cha siasa kinachoshiriki katika uchaguzi kitafuata na kutekeleza maamuzi na maelekezo ya Tume pamoja na kuyakubali na kuyaheshimu matokeo ya uchaguzi. Aidha. malalamiko yoyote yatafikishwa kwenye mamlaka inayohusika kwa utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria.
Mambo yasiyotakiwa kufanyika na Vyama vya Siasa.
Mambo yasiyotakiwa kufanyika wakati wa upigaji kura mpaka kutangazwa kwa matokeo ya kuchaguzi ni pamoja na-
(a) vyama vya siasa, wagombea na wafuasi wao katika siku ya kupiga kura kufanya kampeni ya aina yoyote ikiwa ni pamoja na kuvaa vazi lolote au kuwa na kitu chochote kinachoashiria kushawishi watu kumpigia kura mgombea fulani. Hii, ni pamoja na matumizi ya vyombo vya usafiri vilivyokuwa vinatumika wakati wa kampeni vinavyoashiria utambuzi wa chama fulani;
(b) viongozi wa vyama vya siasa, wagombea au wafuasi wao kufanya vitendo vinavyoweza kusababisha fujo vurugu katika vituo vya kupigia, kuhesabia na kujumlishia kura;
(c) mtu yeyote kutumia simu ya kiganjani ndani ya kituo cha kupigia, kuhesabia au kujumlishia kura isipokuwa msimamizi wa kituo, wasaidizi wake na mlinzi wa kituo cha kupigia kura ambao watatumia simu zao pale itakapobidi kwa shughuli za uchaguzi tu na simu hizo wakati wote ziwe zimaondolewanmlio na ziwe kwenye mtetemo (vibration);
(d) kiongozi, mgombea au mtendaji wa chama cha siasa, mwanachama au mfuasi kujihusisha na vitendo vifuatavyo-
(i) kuwahamasisha wanachama au wafuasi kupiga kura zaidi ya mara moja katika uchaguzi mmoja; na
(ii) kununua kadi ya mpiga kura, kununua kura au kutoa hongo, zawadi, shukrani au aina yoyote ya malipo ya fedha au vifaa kwa mpiga kura au mtendaji wa uchaguzi; na
(e) kiongozi, mgombea au mtendaji yeyote wa chama cha siasa kutoa lugha ya matusi kwa mtendaji wa uchaguzi.
Endapo kuna changamoto au lalamiko lolote kuhusiana na mchakato au taratibu za uchaguzi katika kituo cha kupigia kura, changamoto hizo zitawasilishwa kwa maandishi kwa msimamizi wa kituo kupitia kwa wakala.
(f) kiongozi au mtendaji wa chama cha siasa, mwanachama au mfuasi kuvamia au kukaa kwa nguvu ndani ya kituo cha kupigia, kuhesabia au kujumlishia kura.
(a) kutoa fursa sawa kwa wadau wote wa uchaguzi, husudan, vyama vya siasa ili kuendesha shughuli zao za kisiasa kwa uhuru na kwa kuzingatia sheria za nchi;
(b) kuendelea kuwahudumia wananchi kwa usawa bila kujali uanachama au imani yao kwa vyama vya
siasa;
(c) kuhakikisha kuwa kama hali ya usalama, amani na utulivu katika kipindi chote cha uchaguzi. Aidha, vyombo vyake vya usalama vitoe ulinzi wakati wa mikutano ya kampeni na wakati wa uchaguzi ili kuhakikisha usalalma, amani na utulivu unakuwepo. Vyombo hivyo vizingatie mahitaji na usalama wa makundi maalum ikiwa ni pamoja na watu wenye ulemavu, wanawake, wazee, wajawazito na wapiga kura wenye watoto wachanga;
(d) kutoa fursa sawa kwa vyama vya siasa vyenye wagombea wa Urais na Umakamu wa Rais kutumia vyombo vya habari na utangazaji vinavyomilikiwa na Serikali ili kutangaza sera zao; na
(e) kuhakikisha kuwa viongozi na watendaji wake wanazingatia ipasavyo ukomo wa mamlaka na madaraka yao katika shughuli za uchaguzi.
Yasiyotakiwa kufanywa na Serikali
Mambo yasiyotakiwa kufanywa na Serikali wakati wa uchaguzi ni pamoja na-
(a) kuingilia au kuzuia isivyo halali mikutano iliyoitishwa na vyama vya siasa au wagombea kwa mujibu wa ratiba za uchaguzi;
(b) vyombo vya ulinzi na usalama kutumia madaraka yao kukandamiza wagombea, wafuasi au chama chochote cha siasa. Aidha, vyombo hivyo vitekeleze majukumu yeke kwa weledi; na
(c) kumhamisha mtumishi yeyote wa Serikali anayehusika na shughuli za uchaguzi mpaka mchakato wa uchaguzi ukamilike. Endapo Serikali itaona kuna ulazima wa kumhamisha mtumishi kama huyo ni lazima ishauriane na Tume.
Mambo yasiyotakiwa kufanywa na watendaji wa Serikali wakati wa uchaguzi ni pamoja na-
(a) Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuchanganya ziara za kikazi na shughuli za kiuchaguzi na kutumia vyombo au watendaji wa Serikali katika shughuli za uchaguzi kwa manufaa yao;
(b) kuanzia kipindi cha kampeni za uchaguzi mpaka kutangazwa kwa matokeo Mawaziri hawaruhusiwi-
(i) kutangaza katika vyombo vya habari au kwa namna yoyote misaada au ahadi ya aina yoyote;
(ii) kutoa ahadi za shughuli za maendeleo ya jamii kwa mfano, kujenga barabara, kusambaza maji na mambo mengine kama hayo kwa lengo la kuungwa mkono kisiasa; na
(iii) kutumia madaraka au rasilimali za Serikali kwa shughuli za kampeni za uchaguzi kwa manufaa ya
chama chochote au mgombea yeyote;
(c) Waziri au afisa mwandamizi yeyote wa Serikali kumwita Msimamizi wa Uchaguzi kwa lengo la kujadili masuala ya uchaguzi kuanzia kipindi cha kampeni mpaka kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi; na
(d) Mawaziri, wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na viongozi wengine wa Serikali kuingia katika vituo vya kupigia, kuhesabia au kujumlishia kura. Isipokuwa kwamba Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na viongozi wengine wa Serikali wanaruhusiwa kuingia katika kituo cha kupigia kura kwa madhumuni ya kupiga kura tu.
Upvote
3