Manyata kunambi
New Member
- Jul 19, 2022
- 3
- 0
Muhtasari wa somo ni kitabu ambacho kinamuelekeza mwalimu jinsi ya kufundisha mada husika,njia ambazo mwalimu anatakiwa kuzitumia wakati wa ufundishaji ,dhana au vifaa ambavyo vinahitajika wakati wa ufundishaji.
Muhtasari wa somo uthibiti kiwango Cha elimu kinachotolewa na kuhakikisha kwamba kile kinachofundishwa kinaendana na kiwango Cha mwanafunzi.
Mada ambazo hupatikana katika mihtasari wa masomo zimepangiliwa kuanzia mada sahili kwenda mada tata.
Kinachotiliwa manani katika muhtasari wa somo ni ujuzi ambao mwanafunzi amepata kutoka kwa mwalimu .
Mihtasari ya masomo katika shule za sekondari inatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo;
Kwanza, Muhtasari wa somo unatakiwa kuzingatia maswala ya utendaji zaidi na wala si kinadharia.
Kwa mfano katika somo la Jografia kuna baadhi ya mada kama vile KILIMO, UVUVI, UFUGAJI , hizi ni mada ambazo wanatakiwa kuzisoma kiutendaji zaidi lakini kilichopo au kinachofanyika mashuleni ni nadharia tu , kwa mfano wanafunzi wanapaswa kusoma njia mbalimbali za Uvuvi Kama zile njia za zamani ikiwemo matumizi ya ndoano na nyavu lakini wanasoma kinadharia na mwisho mwanafunzi anatoka aelewi nini maana ya ndoano , Wala kutozifahamu njia nyingine ambazo hutumik katika uvuvi.
Kama muhtasari wa somo utazingatia zaidi maswala ya kiutendaji na Wala si kinadharia kwa sababu elimu inayotolewa kwa wanafunzi ni inalenga kutoa ujuzi kwa kila mwanafunzi na huo ujuzi unategemea zaidi maswala ya utendaji pindi wakiwa katika masomo na Wala si kinadharia.
Moja ya matokeo ya elimu ya kinadharia ni kuzalisha wimbi la wanafunzi ambao wanakosa ujuzi juu ya maswala flani ambapo hupelekea serikari kutumia zaidi fedha kuwaajili wataalamu kutoka nnje kuendesha maswala flani na hiyo inasababishwa na muhtasari wa masomo yetu kuwa kinadharia zaidi.
Pili,mihtasari ya masomo inatakiwa kuzingatia muda wa kutosha kuzishughulikia mada , mihtasari ya masomo hama kwa hakika imetoa muda mchache juu ya kushughulikia mada flani kwa mfano katika somo la kiswahili Kuna mgawanyo flani juu ya ufundishaji wa somo la kiswahil na imeelekezwa Kama ifuatavyo
" Muhtasari huu unafundishika kwa vipindi vitatu(3) kwa wiki.kila kipindi kina dakika 40.katika mwaka Kuna siku 194 za masomo ambapo katika wiki Kuna siku tano (5) za masomo, kwa hiyo wiki za masomo hubaki kuwa 36 tu kwa mwaka.kwa kuwa kila wiki ina vipindi vitatu vya somo la kiswahili kwa mwaka Kuna jumla ya vipindi 108"
Chanzo: Muhtasari wa somo la kiswahili (1997).
Kwa idadi ya vipindi vinavyotolewa ni vigumu kushughulikia mada husika kwa mfano katika " MJENGO WA TUNGO " muhtasari umeeleza mada hiyo itafundishwa kwa vipindi vinne(4), lakini pia mada ndogo ya "UFAFANUZI WA AINA ZA TUNGO" itafundishwa kwa vipindi kumi na sita (16) , na wakati huo huo kuna shughuli mbalimbali ambazo Zita adhiri idadi ya vipindi.
Kiuhalisia muda au idadi ya vipindi katika kushughulikia mada flani bado ni mchache kwahiyo inakuwa ni vigumu kwa mwalimu kuzifundisha mada husika kwa undani na kwa ufasaha.
Tatu, kuzingatia njia za upimaji:
Kwa mujibu wa muhtasari wa somo la kiswahili (1997) ,unaelekeza kwamba upimaji ni safu yenye maswali inayomwongoza mwalimu kupima Kama malengo mahususi yamefikiwa.
Upimaji uzingatia njia mbalimbali ambazo mwalimu anatakiwa kuzitumia Kama kutumia maswali mbalimbali au kutumia mazoezi ambayo mwalimu anayatoa baada kumaliza mada au sehemu ya mada flani.
Katika mihtasari ya masomo katika sehemu hii haijatendewa haki kwa sababu kwa jinsi ilivyoelekezwa katika mihtasari aionyeshi ni njia ipi ambayo imetumika katika upimaji kwa mfano katika mihtasari safu hii imeelezwa kama:
"Je mwanafunzi ameweza kufupisha habari aliyeisoma"

Kwa ujumla safu hii inapaswa kueleza njia ambazo zitatumika katika upimaji kwa mfano " kwa njia ya maswali mwanafunzi ameweza kubainisha kifungu cha habari aliyeisoma."
Utofauti wa hoja ya kwanza na ya pili ni kwamba hoja yakwanza imeulizwa kama swali lakini hoja ya pili ni maelezo ambayo yanajitosheleza na siyo swali ,kwa hiyo katika safu hiyo ya upimaji si sahihi kuweza kuulizwa Kama swali bali lazima iwe Kama sehemu ambayo inayojitosheleza na iweze kuonesha njia ambazo mwalimu anatumia kuweza kupima upimaji wa mwanafunzi.
Nne, kuzingatia shughuli nyingine :
Pia muhtasari wa somo unatakiwa kuzingatia shughuli nyingine Kama vile shughuli za michezo mashuleni ili kuweza kuzalisha zaidi vipaji kutoka katika sehemu mbalimbali kwani kila mwanafunzi anakuwa na malengo yake na saingine hata hayaingiliani na masomo hivyo lazima swala la michezo kuzingatia kwa sababu taifa la wasomi pekee sio taifa ila taifa lenye mchanganyiko wa watu ndio taifa hivyo lazima kuzingatia shughuli nyingine.
Hivyo basi, mihtasari ya masomo iliyopoo kiukweli imejikita zaidi kinadharia juu ya ufundishaji wa mada mbalimbali , na hupelekea ugumu kwa walimu juu ya ufundishaji wao, pia ugawajwi wa vipindi vilivyomo katika mihtasari wa masomo unatia ugumu haswa kwa walimu pindi wakija katika swala la uandaaji wa maazimio ya kazi kwa sababu kiuhalisia muda au vipindi vilivyomo ni vichache mno na si rahisi kwa ufundishaji wa mada zote.
Ukweli usiopingika kwamba maandalizi ya maazimio ya kazi yanahiti taarifa kutoka katika mihtasari wa masomo Sasa inapelekea kutoa taarifa ya uongo haswa kwenye idadi za vipindi kwani muhtasari wa somo na azimio la kazi ni Kama pande mbili za shilingi hutegemeana na ukamilishana.

Upvote
0