Mambo yanayozuia mafanikio yako

Mambo yanayozuia mafanikio yako

Joined
Feb 20, 2018
Posts
28
Reaction score
14
Kila mmoja kwenye maisha anataka mafanikio maana mafanikio yako ndio yatakayokufanya ushi maisha ya kifahari, uweze kumilijiki majumba pamoja na magari ya kifahari.

Lakini umetamani sana kutafuta mafanikio bila kuyapata na hujui ni jambo gani lililokufanya umeshindwa kuyaona mafanikio yako. Huenda ipo sehemu uliokosea ila hukulitambua hilo basi leo nakuletea mambo ambayo yapaswa uyaache ili uweze kufanikiwa katika maisha yako.

01. Kukata tamaa unapokutana na kikwazo kidogo.

Wengi huwa tunatabia moja, pale tunapoianza safari ya kutafuta mafanikio na katika safari hiyo tukakutana na kikwazo chochote tunakata tamaa. Ukiwa mtu wa kukata tamaa kila mara basi inakupasa uyasahau mafanikio kabisa.

Kuna kinajana mmoja ambaye alitaka sana kufanikiwa kwenye maisha yake hivyo alitafuta fursa yeyote ile ili aweze kufanikiwa. Hivyo aliamua kuanza kujishughulisha na kilimo. Kilikuwa kinamlipa vyema ila siku moja akiwa shambani wakiwa wanalima waliweza kupata madini ya dhahabu na walipoanza kuyachimba walipata kiasi na waliamua kuomba msaada kwa wanakijiji ili waweze kununua mashine ya kuchimba madini yale.

Walifanikiwa na lilikuwa ni jambo rahisi sana kwani alikuwa akiaminika sana na wanakijiji. Hivyo baada ya kuchimba madini yale ilifika mahali wakachimba kwa urefu mkubwa sana bila kupata chochote hivyo walihisi madini yale yalikuwa yameisha. Kwakuwa shamba lile lishaharibiwa kwa shughuli za madini aliamua kuliuza kwani alikuwa ashakata tamaa.

Hivyo aliondoka na kwenda kutafuta kazi kwenye kampuni na kufanya kazi kama mwajiri akihisi pale atafanikiwa zaidi. Baada ya mda kidogo kupita yule aliyenunua shamba lile aliamua kumleta mtaalamu wa kuchimba madini na kumwambia afanye utafiti ili kujua ni kiasi gani cha madini kilichokuepo pale au yalikuwa yameshaisha.

Mtaalamu alianza kuifanya kazi yake na mwisho wa siku alimpa taarifa kuwa madini yapo tena kwa wingi sana kwani yapo futi tatu kutoka pale wale vijana walipoachia. Yule mnunuzi wa shamba lile alifurahi sana na kumlipa ujira wake mtu yule kisha akaondoka zake.

Laiti kama kijana yule angeendelea kuchimba madini yale bila kukata tamaa hakika angeweza kutimiza malengo yake. Wengi wetu tunatabia kama hizi tunaanzisha jambo ila tunakata tamaa hata kabla hatujaona matunda. Hivyo ukiwa na tabia ya kukata tamaa ni vigumu kufanikiwa katika maisha yetu.

02. Kutoamini sehemu ulipo ni sehemu sahihi.

Ili kufanikiwa kwenye maisha lazima uwe na imani kuwa hapo ulipo upo sehemu sahihi. Inatakiwa ujiamini eneo ulilopo ndio eneo sahihi ambalo litakupa mafanikio.

Mfano: kazi uliochagua, taaluma au biashara amini ndiyo itakayokupa mafanikio na mafanikio hayawezi kuja kwa kufanya kitu ambacho huna ufanisi nacho hivyo cha zaidi ni kutia juhudi utayaona mafanikio yake. Kulikuwa na mzee mmoja alienda kumtembelea rafiki yake na alipofika alimkuta shambani kwake amekaa kando ya mto.

Walianza mazungumzo ya hapa na pale na yule mzee akamwambia rafiki yake "kwenye hii dunia ukifanikiwa kupata almasi inayolingana na jiwe kama hili (akimuonyesha jiwe alilokuwa ameshika mkononi kati ya matatu aliyokuwa nayo ambayo yalikuwa na ukubwa tofauti) hakika utaweza kumili nyumba nzuri na magari ya kifahari maisha yako yote.

Kisha akaendelea kumwambia na ukifanikiwa kupata alimasi ambayo inalingana na jiwe hili (akimuonyesha jiwe la pili) hakika utakuwa na uwezo wa kuimiliki nchi hii. Na ukifanikiwa kuwa na almasi yenye ukubwa kama jiwe hili (akimuonyesha jiwe la tatu) hakika utainunua dunia yote hii na kuwa mali yako.

Yule rafiki wa yule mzee alimuona yule mzee kaongea maneno yenye hekima hivyo alijawa na shauku ya kutaka kuipata almasi. Hivyo baada ya kushawishika na maneno yale aliuza shamba lake na kuanza kuizunguka dunia kuitafuta almasi. Alizunguka Afrika nzima hakufanikiwa kuipata hakukata tamaa akaendelea ulaya hata Amerika ila hakufanikiwa kuipata.

Hela alizokuwa nazo ambazo alizipata kutokana na shamba alilouza zilianza kuisha na hivyo hakuwa na hela ya kuuzunguka ulimwengu tena. Yule aliyeuziwa shamba aliendelea na kilimo na siku moja akiwa mtoni ambao upo pembeni ya shamba lake aliona jiwe moja linalongaa sana.

Aliamua kuchukua jiwe lile na kwenda kulieka nyumbani kama urembo maana alikuwa hajui ni jiwe gani ila alilipenda tu kwa mng'ao wake. Siku moja yule mzee alikuja kumtembelea yule mwenye shamba na kuliona lile jiwe. Kwa tahamaki alimuuliza yule mwenye shamba "hii almasi umeipata wapi" yule mwenyeshamba alimcheka sana na kumwambia "tokea lini almasi ikakaa mtoni?

Hili jiwe nimeliokota mtoni nikaamua kulichukua kwa sababu ya mng'ao wake" yule mzee alilisogelea na kulikagua ndipo alipogundua kua ni almasi. Hivyo alianza kumsikitikia sana yule rafiki yake. Huwa kwenye maisha tunaamini kwamba ukitoka sehemu uliyopo na kwenda sehemu nyingine ndipo utakapopata mafanikio.

Kama unadhana kama hiyo hakika umekosea. Amini hapo ulipo ni sehemu sahihi kinachohitaji ni kutia bidii na kutumia fursa ambazo zinapatikana eneo hilo na hakika utaona mafanikio yake.

03. Kuiga alichokifanya/anachokifanya mwenzako.
Ni sawa tunaweza kusema kwenye zama hizi huwezi kuanzisha biashara ambayo hajaifanya mwenzako. Lakini kosa ni pale unapoiga na kufanya kama mwenzako anavyofanya huwa wengi wanasema kukopi na kupesti (copy and paste).

Hakika kwa kufanya hivyo ni vigumu sana kufanikiwa cha kufanya unaweza kufanya kitu sawa na mwenzako ila ukakifanya kwa njia tofauti na kikakupa mafanikio makubwa. Watu waliofanikiwa sio kwamba wanafanya vitu tofauti la hasha! ni vilevile ambayo tunavifanya kila siku kwenye maisha yetu ila wakavifanya kwa njia tofauti na kuwaletea mafanikio walionayo siku ya leo (they do the same thing in a different ways).

Ili ufanikiwe inabidi uwe mbunifu tengeneza njia ambayo itawashawishi mteja wako. Na ukifanikiwa akinunua leo bidhaa kwako na akaridhika kesho atarudi. Swali la kujiuliza kama huduma ninayoitoa mimi ni sawa na anayotoa mwingine je mteja uliyemhudumia leo atarudi tena kesho? Ukiweza kupata jibu na kulifanyia kazi jibu hilo hakika utaona mafanikio yake.

04. Kutoweka malengo na kuhakikisha yanatimia.
Ili ufanikiwe kwenye maisha ni lazima kuwa na malengo. Kunatofauti kati ya malengo na shauku/tamaa. Shauku au tamaa ni kutamani kuwa mtu flani au kumiliki kitu flani. Mfano kumiliki magari ya kifahari, nyumba, kampuni n.k. na siku zote tamaa haiwezi kutimia bila kuwa na malengo.

Malengo ndio yanakufanya uwe na mikakati kwenye maisha yako. Mfano mtu atasema ndani ya mwaka hadi kufikia mwezi wa nane lazima niwe nimeanzisha biashara flani. Mtu huyo lazima atajiuliza je nitapata wapi mtaji wa kuanzisha biashara yangu? Maana bila mtaji hataweza kuanzisha biashara na lengo lake halitatimia.

Hivyo lazima atanza kuweka mikakati ambayo itamfanya apate mtaji wa kuanzisha biashara yake. Hakikisha ukieka malengo lazima uweke na mda wa kukamilisha malengo yale na hakikisha yanatimia kwa mda muafaka. Mtu ambaye hana malengo ni sawa na mtu ambaye hajui anakoelekea.

Mfano. Kulikuwa na mwanume mmoja aliyekuwa amesimama njia panda na kumuuliza mpita njia mmoja ambaye alikuwa ni mzee wa makamo hii barabara inaelekea wapi? Naye yule mzee akamuuliza unataka kwenda wapi? Yule mwanaume akajibu “sijui ninakoelekea” kisha yule mzee akamwambia basi pita barabara yeyote ile tu, kwani kunautofauti gani hadi uulize?

Mfano huu unamaanisha nini? Tukiwa hatujui tunaelekea wapi barabara yeyote ile hutufikisha. Ukiwa haujaeka malengo kwenye maisha yako ni sawa na mtu ambaye hajui anapoelekea. Watu wengi wanakuwa na shauku ya kufanya jambo flani maishani au kutimiza jambo flani kwa siku.

Ila hawajaeka maelengo hivyo kusababisha kupoteza muelekeo na hatimaye siku au miaka itasonga na hujafanya chochote. Hivyo shauku bila malengo ni sawa na mtu yule aliyesimama njia panda.

05. Kutojali afya yako.

Ninaposema kutojali afya mawazo ya wengi huenda moja kwa moja kwenye chakula. Ni sawa upo sahihi ila tambua kuwa sio chakula pekee kinachoufanya mwili kuwa na afya. Yapo mazoezi pia kutumia njia yeyote ile kujikinga na maradhi.

Tuzungumzie maradhi, kwa kipindi hiki cha sasa kumekuwa na maradhi mengi ambayo yanaifanya afya yako kudhoofika. Mfano kuna malaria na ukimwi. Vijana wengi wa siku hizi na baadhi ya wazee wanaendekeza sana ngono na wengi wao huishia kufanya ngono zisizo salama.

Ni sawa sijakataa vishawishi vipo lakini kumbuka kama wewe ni kijana na unatamani sana kufanikiwa ukiendekeza sana ngono basi tambua fika kuwa hutafanikiwa kwenye malengo yako.

Dunia ya sasa wengi wameambukizwa na gonjwa hatari la ukimwi na wengi wao huwa hawakuambii na huwezi kugundua kwa macho ila wengi tunalipuuza kwa kuendekeza ule msemo vijana wengi wanaopenda kutumia “ukimwi ni sawa na malaria” nawe ukiwa na mawazo kama hayo hautafanikiwa kamwe.

Pia maradhi hupunguza nguvu kazi ukiwa kama mtu anayetafuta mafanikio tambua siku moja ni muhimu sana na hutakiwi kuipoteza kirahisi maana hutaweza kuifidia kamwe. Hivyo jikinge na magonjwa ili kuepuka kupoteza siku nyingi kwa kulazwa kitandani hakika ukizingatia hilo utaona matunda yake.
 
Mmmhhh bila takwimu za watu waliofanikiwa wakiwa na afya na ambak hawakufanikiwa kisa hawana afya huu uzi wako ni mawazo yako tu ambayo yanaweza kupingwa na yeyote
 
Ni sawa sijakata hapa hatuongelei kwa kitaalamu. Utaalamu ndio unahitaji ufanye utafiti (reserch) ila mimi nawafungua tu watu mawazo mkuu. Chukulia mfano ugonjwa kama UKIMWI je hii itahitaji ufanye utafiti?
 
Kwahiyo ukimwi unazuia mafanikio?
Hakuna watu wenye ukimwi na wamefanikiwa?
 
Kama akiwa na mtazamo changa kuna wengine ambao wakiupata ugonjwa kama huu hukata tamaa na akikata tamaa safari yake ya mafanikio inakaribia kufika ukingoni. Mfano mzuri ni nikipokuwa field mwaka juzi nilikuwa kwenye kitengo cha CTC. Huwa pale kunawagonjwa ambao wanakuchua dawa hizi za kurefusha maisha na wengine huja kujua afya zao. Ukiwa kama mtoaji ushauri nasaha kuna mambo mengi utayajua ila kikubwa nilichokutana nacho ni kwamba wapo watu wanaoanza matibabu lakini hawazingati dawa zile na wengine huacha kabisa hadi aumwe ndio afike hospitalini sasa mtu kama huyo ukimuuliza anaweza kufanya kazi gani anakuambia hawezi kufanya chochote je huyo ataweza kuhangaika na purukushani za kutafuta mafanikio. Ndugu hii ni mada ndefu sana nitaielezea kiundani kama unataka kujifunza
 
Aliyelenga kufanikiwa na kuacha alama duniani atafanikiwa tu hata apatwe na ukimwi, ukimwi unazidisha mtizamo wa mtu juu ya maisha na malengo yake, huu ni msimamo wangu binafsi, kwa umri wangu nina miaka 33, nimejiapiza kufikia miaka 40 niwe huru kiuchumi na nibaki mtu wa kubuni, kupanga, kusimamia, kushawishi na kuhimiza, nikipatwa na ukimwi leo nina miaka zaidi ya 10 ya kuishi ikiwa nitafuta masharti, sasa why nibadili viapo vyangu juu ya maisha yangu na uzao wangu!?

Sio kama nawashawishi vijana wenzangu wasiwe makini na kuacha ngono zembe bali kwa atakaye jikwaa nashauli asitoke relini coz ile sio ebola.
 
Hayo mambo uliyoandika Ni basics Sana kiasi kwamba hayamfanyi mtu kufikiri Mara mbili.
 
Aliyelenga kufanikiwa na kuacha alama duniani atafanikiwa tu hata apatwe na ukimwi, ukimwi unazidisha mtizamo wa mtu juu ya maisha na malengo yake, huu ni msimamo wangu binafsi, kwa umri wangu nina miaka 33, nimejiapiza kufikia miaka 40 niwe huru kiuchumi na nibaki mtu wa kubuni, kupanga, kusimamia, kushawishi na kuhimiza, nikipatwa na ukimwi leo nina miaka zaidi ya 10 ya kuishi ikiwa nitafuta masharti, sasa why nibadili viapo vyangu juu ya maisha yangu na uzao wangu!?

Sio kama nawashawishi vijana wenzangu wasiwe makini na kuacha ngono zembe bali kwa atakaye jikwaa nashauli asitoke relini coz ile sio ebola.
Umenena vyema mhesihimiwa lakini wapo wale wanaopaniki na kuona kifo kimefika mfano wapo vijana wenye umri kuanzia miaka 22 wengi hukata tamaa na ukiwa unampima maambukizi ukimuuliza utafanya nini endapo ukigundulika umeathirika atakuambia sitakubali kufa peke yangu mtu mwenye mtazamo kama huo tayari ashapotoka na kinachobakia kwenye nafsi yake ni chuki na sio mitazamo ya kimafanikio tena.
 
Kila mmoja kwenye maisha anataka mafanikio maana mafanikio yako ndio yatakayokufanya ushi maisha ya kifahari, uweze kumilijiki majumba pamoja na magari ya kifahari.

Lakini umetamani sana kutafuta mafanikio bila kuyapata na hujui ni jambo gani lililokufanya umeshindwa kuyaona mafanikio yako. Huenda ipo sehemu uliokosea ila hukulitambua hilo basi leo nakuletea mambo ambayo yapaswa uyaache ili uweze kufanikiwa katika maisha yako.

01. Kukata tamaa unapokutana na kikwazo kidogo.

Wengi huwa tunatabia moja, pale tunapoianza safari ya kutafuta mafanikio na katika safari hiyo tukakutana na kikwazo chochote tunakata tamaa. Ukiwa mtu wa kukata tamaa kila mara basi inakupasa uyasahau mafanikio kabisa.

Kuna kinajana mmoja ambaye alitaka sana kufanikiwa kwenye maisha yake hivyo alitafuta fursa yeyote ile ili aweze kufanikiwa. Hivyo aliamua kuanza kujishughulisha na kilimo. Kilikuwa kinamlipa vyema ila siku moja akiwa shambani wakiwa wanalima waliweza kupata madini ya dhahabu na walipoanza kuyachimba walipata kiasi na waliamua kuomba msaada kwa wanakijiji ili waweze kununua mashine ya kuchimba madini yale.

Walifanikiwa na lilikuwa ni jambo rahisi sana kwani alikuwa akiaminika sana na wanakijiji. Hivyo baada ya kuchimba madini yale ilifika mahali wakachimba kwa urefu mkubwa sana bila kupata chochote hivyo walihisi madini yale yalikuwa yameisha. Kwakuwa shamba lile lishaharibiwa kwa shughuli za madini aliamua kuliuza kwani alikuwa ashakata tamaa.

Hivyo aliondoka na kwenda kutafuta kazi kwenye kampuni na kufanya kazi kama mwajiri akihisi pale atafanikiwa zaidi. Baada ya mda kidogo kupita yule aliyenunua shamba lile aliamua kumleta mtaalamu wa kuchimba madini na kumwambia afanye utafiti ili kujua ni kiasi gani cha madini kilichokuepo pale au yalikuwa yameshaisha.

Mtaalamu alianza kuifanya kazi yake na mwisho wa siku alimpa taarifa kuwa madini yapo tena kwa wingi sana kwani yapo futi tatu kutoka pale wale vijana walipoachia. Yule mnunuzi wa shamba lile alifurahi sana na kumlipa ujira wake mtu yule kisha akaondoka zake.

Laiti kama kijana yule angeendelea kuchimba madini yale bila kukata tamaa hakika angeweza kutimiza malengo yake. Wengi wetu tunatabia kama hizi tunaanzisha jambo ila tunakata tamaa hata kabla hatujaona matunda. Hivyo ukiwa na tabia ya kukata tamaa ni vigumu kufanikiwa katika maisha yetu.

02. Kutoamini sehemu ulipo ni sehemu sahihi.

Ili kufanikiwa kwenye maisha lazima uwe na imani kuwa hapo ulipo upo sehemu sahihi. Inatakiwa ujiamini eneo ulilopo ndio eneo sahihi ambalo litakupa mafanikio.

Mfano: kazi uliochagua, taaluma au biashara amini ndiyo itakayokupa mafanikio na mafanikio hayawezi kuja kwa kufanya kitu ambacho huna ufanisi nacho hivyo cha zaidi ni kutia juhudi utayaona mafanikio yake. Kulikuwa na mzee mmoja alienda kumtembelea rafiki yake na alipofika alimkuta shambani kwake amekaa kando ya mto.

Walianza mazungumzo ya hapa na pale na yule mzee akamwambia rafiki yake "kwenye hii dunia ukifanikiwa kupata almasi inayolingana na jiwe kama hili (akimuonyesha jiwe alilokuwa ameshika mkononi kati ya matatu aliyokuwa nayo ambayo yalikuwa na ukubwa tofauti) hakika utaweza kumili nyumba nzuri na magari ya kifahari maisha yako yote.

Kisha akaendelea kumwambia na ukifanikiwa kupata alimasi ambayo inalingana na jiwe hili (akimuonyesha jiwe la pili) hakika utakuwa na uwezo wa kuimiliki nchi hii. Na ukifanikiwa kuwa na almasi yenye ukubwa kama jiwe hili (akimuonyesha jiwe la tatu) hakika utainunua dunia yote hii na kuwa mali yako.

Yule rafiki wa yule mzee alimuona yule mzee kaongea maneno yenye hekima hivyo alijawa na shauku ya kutaka kuipata almasi. Hivyo baada ya kushawishika na maneno yale aliuza shamba lake na kuanza kuizunguka dunia kuitafuta almasi. Alizunguka Afrika nzima hakufanikiwa kuipata hakukata tamaa akaendelea ulaya hata Amerika ila hakufanikiwa kuipata.

Hela alizokuwa nazo ambazo alizipata kutokana na shamba alilouza zilianza kuisha na hivyo hakuwa na hela ya kuuzunguka ulimwengu tena. Yule aliyeuziwa shamba aliendelea na kilimo na siku moja akiwa mtoni ambao upo pembeni ya shamba lake aliona jiwe moja linalongaa sana.

Aliamua kuchukua jiwe lile na kwenda kulieka nyumbani kama urembo maana alikuwa hajui ni jiwe gani ila alilipenda tu kwa mng'ao wake. Siku moja yule mzee alikuja kumtembelea yule mwenye shamba na kuliona lile jiwe. Kwa tahamaki alimuuliza yule mwenye shamba "hii almasi umeipata wapi" yule mwenyeshamba alimcheka sana na kumwambia "tokea lini almasi ikakaa mtoni?

Hili jiwe nimeliokota mtoni nikaamua kulichukua kwa sababu ya mng'ao wake" yule mzee alilisogelea na kulikagua ndipo alipogundua kua ni almasi. Hivyo alianza kumsikitikia sana yule rafiki yake. Huwa kwenye maisha tunaamini kwamba ukitoka sehemu uliyopo na kwenda sehemu nyingine ndipo utakapopata mafanikio.

Kama unadhana kama hiyo hakika umekosea. Amini hapo ulipo ni sehemu sahihi kinachohitaji ni kutia bidii na kutumia fursa ambazo zinapatikana eneo hilo na hakika utaona mafanikio yake.

03. Kuiga alichokifanya/anachokifanya mwenzako.
Ni sawa tunaweza kusema kwenye zama hizi huwezi kuanzisha biashara ambayo hajaifanya mwenzako. Lakini kosa ni pale unapoiga na kufanya kama mwenzako anavyofanya huwa wengi wanasema kukopi na kupesti (copy and paste).

Hakika kwa kufanya hivyo ni vigumu sana kufanikiwa cha kufanya unaweza kufanya kitu sawa na mwenzako ila ukakifanya kwa njia tofauti na kikakupa mafanikio makubwa. Watu waliofanikiwa sio kwamba wanafanya vitu tofauti la hasha! ni vilevile ambayo tunavifanya kila siku kwenye maisha yetu ila wakavifanya kwa njia tofauti na kuwaletea mafanikio walionayo siku ya leo (they do the same thing in a different ways).

Ili ufanikiwe inabidi uwe mbunifu tengeneza njia ambayo itawashawishi mteja wako. Na ukifanikiwa akinunua leo bidhaa kwako na akaridhika kesho atarudi. Swali la kujiuliza kama huduma ninayoitoa mimi ni sawa na anayotoa mwingine je mteja uliyemhudumia leo atarudi tena kesho? Ukiweza kupata jibu na kulifanyia kazi jibu hilo hakika utaona mafanikio yake.

04. Kutoweka malengo na kuhakikisha yanatimia.
Ili ufanikiwe kwenye maisha ni lazima kuwa na malengo. Kunatofauti kati ya malengo na shauku/tamaa. Shauku au tamaa ni kutamani kuwa mtu flani au kumiliki kitu flani. Mfano kumiliki magari ya kifahari, nyumba, kampuni n.k. na siku zote tamaa haiwezi kutimia bila kuwa na malengo.

Malengo ndio yanakufanya uwe na mikakati kwenye maisha yako. Mfano mtu atasema ndani ya mwaka hadi kufikia mwezi wa nane lazima niwe nimeanzisha biashara flani. Mtu huyo lazima atajiuliza je nitapata wapi mtaji wa kuanzisha biashara yangu? Maana bila mtaji hataweza kuanzisha biashara na lengo lake halitatimia.

Hivyo lazima atanza kuweka mikakati ambayo itamfanya apate mtaji wa kuanzisha biashara yake. Hakikisha ukieka malengo lazima uweke na mda wa kukamilisha malengo yale na hakikisha yanatimia kwa mda muafaka. Mtu ambaye hana malengo ni sawa na mtu ambaye hajui anakoelekea.

Mfano. Kulikuwa na mwanume mmoja aliyekuwa amesimama njia panda na kumuuliza mpita njia mmoja ambaye alikuwa ni mzee wa makamo hii barabara inaelekea wapi? Naye yule mzee akamuuliza unataka kwenda wapi? Yule mwanaume akajibu “sijui ninakoelekea” kisha yule mzee akamwambia basi pita barabara yeyote ile tu, kwani kunautofauti gani hadi uulize?

Mfano huu unamaanisha nini? Tukiwa hatujui tunaelekea wapi barabara yeyote ile hutufikisha. Ukiwa haujaeka malengo kwenye maisha yako ni sawa na mtu ambaye hajui anapoelekea. Watu wengi wanakuwa na shauku ya kufanya jambo flani maishani au kutimiza jambo flani kwa siku.

Ila hawajaeka maelengo hivyo kusababisha kupoteza muelekeo na hatimaye siku au miaka itasonga na hujafanya chochote. Hivyo shauku bila malengo ni sawa na mtu yule aliyesimama njia panda.

05. Kutojali afya yako.

Ninaposema kutojali afya mawazo ya wengi huenda moja kwa moja kwenye chakula. Ni sawa upo sahihi ila tambua kuwa sio chakula pekee kinachoufanya mwili kuwa na afya. Yapo mazoezi pia kutumia njia yeyote ile kujikinga na maradhi.

Tuzungumzie maradhi, kwa kipindi hiki cha sasa kumekuwa na maradhi mengi ambayo yanaifanya afya yako kudhoofika. Mfano kuna malaria na ukimwi. Vijana wengi wa siku hizi na baadhi ya wazee wanaendekeza sana ngono na wengi wao huishia kufanya ngono zisizo salama.

Ni sawa sijakataa vishawishi vipo lakini kumbuka kama wewe ni kijana na unatamani sana kufanikiwa ukiendekeza sana ngono basi tambua fika kuwa hutafanikiwa kwenye malengo yako.

Dunia ya sasa wengi wameambukizwa na gonjwa hatari la ukimwi na wengi wao huwa hawakuambii na huwezi kugundua kwa macho ila wengi tunalipuuza kwa kuendekeza ule msemo vijana wengi wanaopenda kutumia “ukimwi ni sawa na malaria” nawe ukiwa na mawazo kama hayo hautafanikiwa kamwe.

Pia maradhi hupunguza nguvu kazi ukiwa kama mtu anayetafuta mafanikio tambua siku moja ni muhimu sana na hutakiwi kuipoteza kirahisi maana hutaweza kuifidia kamwe. Hivyo jikinge na magonjwa ili kuepuka kupoteza siku nyingi kwa kulazwa kitandani hakika ukizingatia hilo utaona matunda yake.
Duh! Amazing story! Isipokuwa inasikitisha maana Mungu hana nafasi kabisa katika mtu kupata mafanikio.
 
Mtu yuko kijijini anaendesha bodaboda kwa siku anapata elf 6 au asipate unasema asitoke hapo alipo kwenda mjini anakoweza kupata elfu 20 au zaidi kwa siku, hii kali
 
Back
Top Bottom