Pre GE2025 Mambo yanazidi kunoga Majimboni, mbinu ni zilezile wadanganywa ni walewale

Pre GE2025 Mambo yanazidi kunoga Majimboni, mbinu ni zilezile wadanganywa ni walewale

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
20241009_192652.jpg


Unaweza shikwa hasira kwa mbinu zilezile zitumikazo kuwahadaa wananchi ila kila ukikumhuka wananchi wanadanganyika kama watoto wadogo kwa greda moja linalopita kwenye barabara za mitaani kiba baada ya miaka 5 kuelekea uchaguzi na halitaonekana tena mpaka baada ya miaka 5 basi unashusha pumzi unailaumu elimu wanayopewa Wananchi inayowafanya washindwe kitambua kuwa Wanadanganywa ili wawape kura

Nimeona mitaa mbalimbali barabara zikikarabatiwa kwa greda kupita kwa kweli zinavutia ila walikuwa wapi kwa miaka yote wananchi wanateseka kupita kwenyw mashimo, kwa nini sasa? Japo greda limepita ila inabidi tuwaambie wazuie mvua maana mvua ikinyesha tope lake ni hatari zaidi ya awali

Nikisema Watanzania wamerogwa nakataa kwa kuwa siamini kuhusu Ushirikina, nikisema niwaze huenda hawajitambui kulingana na Elimu ya uraina kutolewa ikiwa na Mrengo wa namna fulani naona huenda ikawa sahihi hii.

Hivi mnawezaje kukubali kudanganywa kwa miaka nenda rudi kwa uongo uleule na mkaingia kingi bila hata kuona kuwa hao ni matapeli wanahitaji madaraka kisha wanawatupa wanendelea na mishe zao?

Ole wake mtu aje kunambia nichague kisa nimepitisha greda hapo haki nitampeleka mahakamni akanieleze kwa nini ananiona mjinga.

 
View attachment 3120158Unaweza shikwa hasira kwa mbinu zilezile zitumikazo kuwahadaa wananchi ila kila ukikumhuka wananchi wanadanganyika...
barabara ikiwa mbovu mnalalamika, barabara hiyo hiyo ikijengwa mnalalamika 🤣

hiyo maana yake haijulikani hata nini kinachohitajika ndrugu zangu mlio elimika, right?🐒

ama nini mwataka?
 
Back
Top Bottom