Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
1. Biashara holela ya bunduki kwa raia
Hizi taarifa za kupigana sana risasi hovyo hovyo kila siku kwa sababu ya biashara holela ya silaha isiyo na udhabiti mpana kama mataifa mengine ya West na yaliyoendelea zinasikitisha na kutia doa sana Marekani. Kifo cha risasi kwa watoto ndicho chanzo kinachoongoza kwa sasa. Nafikiri sio sahihi kabisa, na ni wendawazimu wa hali ya juu kuruhusu bunduki za kila aina kuuzwa kama bidhaa nyingine ambapo mtu yeyote hata mwenye matatizo ya akili, umri mdogo au mhalifu anaweza kununua bunduki kirahisi kama bidhaa nyingine yoyote.
2. Wafahidhina/Conservatives hasa MAGA Republicans
Hawa watu nawaona wa ajabu sana katika sera na misimamo yao. Hawataki sheria zozote ngumu kuhusu umilikaji bunduki, hawapendi sana msaada wa serikali kwa watu masikini, ukiwa kinyume na Democrats wewe ni rafiki yao na wataungana na wewe, wamejaa conspiracy theories za kila aina. Ni tofauti sana na conservatives wengine wa West na nchi zilizoendelea ambao wana make sense kwa mambo mengi.
3. Ughali wa huduma za matibabu na dawa sekta ya afya
Marekani ni taifa ambalo gharama za kila matibabu ziko juu na dawa zinauzwa ghali sana tofauti na kwingine duniani. Sekta ya afya ni mojawapo ya sekta zenye mzozo mkali sana katika siasa za hii nchi .Upande mmoja wa Democrats wakitaka udhibiti, usaidizi na ufadhili zaidi wa serikali kupitia bima na sheria na upande mwingine wa Republicans ukitaka biashara huria zaidi ambapo makampuni ya dawa, bima, hospitali na wateja wao ndio watakuwa na maamuzi yao makubwa zaidi ya kibinafsi.