Ignatus Mkonga
Member
- Sep 15, 2016
- 18
- 9
Mambo yatakayokuwepo miaka 50 Baadae.
Inasikitisha kufahamu ya kwamba mambo yatakayokuwepo miaka 50 ijayo ni matokeo ya yale yanayofanyika leo. Je ni mambo yapi yatakayokuwepo miaka 50 ijayo?
Picha 📸 : Google
Habari mpendwa,
Naitwa Ignatus John Mkonga, ungana nami katika makala hii.
Dunia haitamani kumhifadhi binaadamu tena, si kwasababu tu ina urembo unaopakwa matope bali kwasababu ya kuhofia ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Iliumbwa kwa mhimili mzuri na kwa pande nne zenye kung'aa kama Almasi nayo miito na vijito vyake vilikuwa vikitiririsha maji matulivu yasiyo na mawaa.
Ilikuwa mahali pekee Mungu aliweka imani ili paweze kumhifadhi binaadamu lakini kumbe usilolijua ni sawa na usiku wa giza.
Baada ya miaka 2021 BK, Ewe Dunia, u wapi urembo wako?
1. Jamii imesahau unavyopambana kuilinda dhidi ya mionzi mikali ya jua, na kuamua kupunguza uoto kwa kilekinachoitwa shughuli za maendeleo. Uoto wako unaondolewa. Nini kitakuwepo miaka 50 ijayo?
2. Jamii imesahau maandiko ya kuijenga imani. Watu wameamua kufanya dini kuwa biashara, Zinaa makanisani pamoja na utakatishaji fedha kuliko hata Zakayo mtoza ushuru, kwanini jamii imekuwa saliti kwako kama Yuda?
3. Vijana na mabinti wanavaa nguo za kizinzi wakisema ndio "Neo Life" ukisasa umefanya binti akiwa Bikira jamii inamshangaa. Binti zako wamegeuza maeneo mbalimbali kuwa sehemu za biashara ya miili yao pengine kwasababu ya ukatili wa kimaisha. Vijana wanauana bila woga kwasababu mioyo yao haina hofu ya Mungu katika kutubu na kuirejea imani.
4. Ona sasa hadi ndoa za jinsia moja zinahalalishwa nawakuu wa dini. Mabinti wananyanyaswa kingono ili wapewe ajira au madaraja vyuoni. Ndio maana hata wengine hawavai nguo zao kwa staha. Ewe Dunia, mimi ninakwambia yatakayokutokea miaka 50 ijayo.
5. Umepewa watu kadhaa wakuongoze lakini wamekua wala Rushwa, wapenda starehe, wafujaji wa mali za umma, wanaoweza kutunga sheria na zikapita bila wao kujua, wenye shibe wakipita kusalimia maji yao. Waliokosa mipango madhubuti kuukabili umasikini, tunao wengi wenye kukosa uvumilivu wa kisiasa hadi wanawanyanyapaa wengine. Hapa si tu kwako wewe hata Zohari inaona hayo na Damu zao waliao zitakuwa juu ya wale watesao na kufurahia maisha haya mafupi.
Miaka 50 ijayo ninaona damu zikimiminika juu ya uso wa Ardhi, ninaona majeraha katika miili ya wale wanyama wenye pembe mbili za ufunuo. Hakika, ninaona watu wakitubu kuurejea ukweli na kujutia maisha waliyoyaishi ingawa wamechelewa.
Hata sasa unafanyiwajitihada za utunzaji wa mazingira lakini upeo wa kilio chako ni mkuu na hauhimiliki. Hivyo ninaona watu wakifa kwa kiu na njaa, mabinti watatembea uchi wa mnyama kama walivyozaliwa lakini asiwepo wa kuwatamani. Uraibu wa madawa ya kulevya na utazamaji wa filamu za ngono utakua umedhihirika na asiwepo wa kuona haya mbele ya walezi wake.
Maadili na upendo viwe kipaumbele chako ewe Dunia, fundisha vijana wako maadili mema, ugaidi unaoemdelea duniani umetokana na kukosa upendo kati ya kabila moja na lingine, dini moja kwa nyingine, tabaka moja na lingine. Fundisha hilo, watoto wako wanahitaji elimu mbadala badilika, vijana wanaingia mitaani kuwa wahuni kwasababu ya kukosa ajira wape elimu ya maisha ya kila siku kuokoa vizazi vijavyo. Naamini umenielewa.
Dunia najua utaharibiwa, lakini ongeza muda wako wa kuishi kwa kufuata ushauri wangu.
Miaka 50 ijayo, Ewe Dunia huenda usiione lakini kama unataka kupona, waambie watu wako wageuze vichwa vyao kuelekea magharibi, kabla Ustaarabu haujarudi mashariki wakaione ile nuru jioni. Na kamwe hawatakufa bali watakuwa hai daima.
Ahsanteni sana 🤝🏽

Upvote
2