SoC04 Mambo yatakayochochea ukuaji katika sekta ya utalii

SoC04 Mambo yatakayochochea ukuaji katika sekta ya utalii

Tanzania Tuitakayo competition threads

Joseph Nyoni

Member
Joined
Apr 21, 2024
Posts
5
Reaction score
2
Na Joseph Nyoni

Tunapozungumzia utalii nchini tunazungumzia Taifa linalopata watalii kati ya milioni 1.5 hadi milioni 2 kwa mwaka.

Na tunapozungumzia Afrika katika mataifa yanayoongoza katika sekta ya utalii tunazungumzia mataifa matatu ambayo yanafanya vizuri kwa miaka kadhaa mfululizo yaani Misri (Egypt) Morocco pamoja na Afrika Kusini(South Africa) Hawa ndiyo wafalme katika sekta hii wakitembelewa na watalii wasiopungua milioni 10 kwa mwaka. Kabla ya Korona Misri( Egypt) Ilikuwa imekwisha tembelewa na watalii wasiopungua milioni 13 yaani mwaka 2019 huku wakiwa wameweka malengo ya kutembelewa na watalii milioni 15 mwaka 2020 kama kusingekuwa na tatizo la ugonjwa wa Korona.

Huku bara la Afrika likitajwa kama bara la pili kwa maendeleo ya haraka katika sekta y utalii Duniani baada ya bara la Asia. Vyombo vikubwa vya habari Duniani kama CNN pamoja na ripoti mbalimbali ikiwemo ile ya Global Spa and wellness monitor wameeleza hilo kwa kina na kuonyesha kushangazwa.

Zipo jitihada ambazo zimefanywa na serikali za awamu mbalimbali na zinaendelea kufanywa sasa hapa nchini ikiwemo kuboresha viwanja vya ndege na kununua ndege kwaajili ya kurahisisha safari za watalii kitu ambacho kilifanywa pia na serikali ya Misri miaka ya nyuma na hata kuweka mkazo zaidi mwaka 2018 ambapo waliongeza ujenzi wa viwanja kadhaa vya ndege lengo likiwa ni kurahisisha safari za watalii na kuwavuta nchini mwao ili wapate urahisi wa kwenda kutembelea nchini mwao wapatapo nafasi. Hili siyo la kuumiza vichwa nchini Tanzania kwani tayari linatiliwa mkazo lakini changamoto kubwa imekuwa katika kuongeza idadi ya watalii. Wakati umefika tuwe na lengo la kuingiza watalii milioni 5 baadala ya milioni 1.5 hadi 2.

Hivi juzijuzi mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan aliamua kurekodi kipindi akilenga kutangaza utalii nchini kama sehemu ya jitihada zake kuweza kuwavuta watalii wa mataifa mbalimbali nchini.

Basi ikiwa uimarishaji wa miundombinu kama viwanja vya ndege umeandaa mazingira mazuri ya kupeleka watalii sehemu mbalimbali nchini bado changamoto kubwa tuliyonayo ni idadi ya watalii hivyo yatupasa kufanya pia mambo mengine ili kuchochea utalii walau tupate watalii milioni tano kwa kipindi kifupi cha chini ya miaka 5. Basi tukifanya yafuatayo tunaweza tukafanikiwa kutangaza zaidi vivutio na kujikuta tunafanikiwa haraka.

1. Ukiitazama Misri utagundua imefanikiwa kujitangaza kupitia dini tatu zenye chimbuko lake katika eneo hilo na maeneo yanayozunguka taifa hilo yaani Ukristo, Uislamu na Uyahudi kitu kinachopelekea wengi kupenda kutembelea taifa hilo. Pia swala lingine ni historia yake, hiki kipo pia katika eneo la Zanzibar nchini Tanzania yaani historia yake inafungamana sana na Oman hivyo kufanya watalii wengi kutembelea zaidi Zanzibar ili waweze kujifunza mambo ya kihistoria yaani kuhusu utawala wa kisultani na mengine.

Kwa maana hiyo basi tujitahidi kufungamanisha utalii na mambo ya historia ya ukoloni pia hasa kwa upande wa Tanganyika tukiweka mkazo katika mataifa yaliyotawala yaani ujerumani na uingereza hata wareno na huko mashariki ya mbali waliokuja kufanya biashara miaka mingi kabla ya ukoloni kwani kuna vitu vya kumbukumbu walifanya hapa nchini hivyo tunaweza kuweza kutangaza vivutio hivyo katika mataifa yao kwani huweza kuwavuta kutokana na mambo hayo ya kihistoria wakajja wengi kujifunza.

Kama haitoshi, sisi hatuna masinagogi kama Misri lakini kuna jambo linazungumzwa kwamba mlima Kilimanjaro una pete ya mfalme Suleiman ambapo alizikwa mtoto wa mfalme huyo aliyepotea njia akiwa na pete hiyo hivyo kuugua maradhi na kufa kisha kuzikwa mlimani hapo. Mfalme huyo ni mtu muhimu katika dini tatu zilizosambaa kote duniani na anatajwa kwenye vitabu vitakatifu vinavyotumiwa katika Ukristo, Uislam na hata Uyahudi. Basi nasi tulitangaze kwa nguvu ikiwa ni sehemu ya historia ya kale ya mlima huo na tusibaki tu kuzungumzia urefu wa mlima pekee na maajabu ya maumbile yake bali tuufungamanishe na mtu huyu mashuhuri katika dini ikiwa ni historia ya kale ya mlima huo ambayo haipo katika milima mingine mirefu duniani.

2. Tuwatumie watu maarufu Duniani kama wachezaji wa mpira kama akina Christian Ronaldo, Messi au wasanii wakubwa wanaotazamwa zaidi Duniani kama hao akina Rihanna, Jay Z, na wengine kisha tulipie vipindi katika television zinazotazamwa sana Duniani hasa katika mabara ya Ulaya na Amerika ambako utalii ni kama sehemu kubwa ya utamaduni wao.

3. Kuwe na matangazo endelevu katika runinga hizo za kimataifa ambazo hutazamwa na watazamaji wengi katika mabara hayo.

4. Matamasha makubwa kama lile la BET ambalo kuna mtanzania mmoja alikuwepo(msanii Diamond Platinums) Akiwania moja ya tuzo tusibaki tu kusema anashinda au hashindi? Kama Taifa tulitakiwa kufanya kitu pale au tufanye kitu kwa siku zijazo kwa kupenyeza matangazo yanayovutia watalii nchini kwani Dunia nzima hufuatilia yanayoendelea katika matamasha hayo ambayo wakati mwingine yanaweza hata kutuletea wawekezaji. Waonapo matangazo mengi watadadisi waijue vizuri Tanzania.

5. Mikutano mikubwa ya kimataifa( kidunia) Inaweza kutumiwa kukuza utalii kwa kuweka matangazo ya vivutio vyetu huko kama vya Mlima Kilimanjaro, mbuga na hifadhi tulizonazo achilia mbali utalii wa mambo ya kale.

6. Mashindano ya michezo kama soka, ndondi, na mengine yawe fursa kwetu kwa kupeleka matangazo.

7. Kupunguza gharama ya usafiri kwa watu wanaokuja Tanzania kwaajili ya kutalii.

8. Kufanya makubaliano na wasanii wetu wa muziki na filamu ili waweze kufanyia video zao maeneo ya utalii na hata kuandika maeneo hayo katika video zao zitazamwapo ziweze kusaidia watu wapate hamasa ya kutembelea vivutio.

9. Kushawishi taasisi mbalimbali ziweze kufanya safari kwenda kwenye maeneo ya utalii nchini, mfano wafanyakazi wa Radio na TV, benki, walimu na wanafunzi wa vyuo na shule n.k

10. Tuweke matangazo katika ndege na ikiwezekana video mbalimbali za vivutio vya utalii ziweze kuonekana katika ndege zinazoruka huko na huko hasa katika mataifa ambayo watu wake sana hupenda utalii au utalii ni utamaduni wao mkubwa kama Ufaransa, uingereza, Marekani, Kanada n.k.

" Tuweke jitihada tuweze kupata watalii walau milioni 5 kwa mwaka"

Joseph Nyoni

0766875334
 
Upvote 5
Back
Top Bottom