mimiamadiwenani
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 5,718
- 7,784
Habari za muda huu, tena.
Leo nitaongelea na hili pia. Nina uzoefu mkubwa mno wa kuwa karibu na Watanzania wa hadhi mbali mbali, hivyo mengi nimeyaona na kuyafahamu.
Kwa Tanzania, hususani DSM(ingawa mpaka mikoani hii naona inaelekea), watu wanaishi kwa makundi na wengi hufanya vitu vya kuigana igana, ni kama nyumbu(siyo tusi, nimetumia kama mfano tu).
Kuna vitu karne hii ambavyo vina tija sana, ila ukivifanya au ukiwa navyo, Wa-TZ walio wengi watakuita mshamba, na ikibidi hata kutengwa utatengwa.
1. Kujishusha na kuomba samahani.
Siku za hivi karibuni, kujishusha na kusema neno 'samahani' imeonekana kuwa ni ushamba hasa kwa jamii za Wa-TZ, wakati ni habit bora kabisa. Muungwana akivuliwa nguo huchutama. Ukizingua, omba msamaha.
2. Kuto bet.
Leo hii kwenye kundi la Wa-TZ nane au zaidi, ukisema hu bet, basi wengi kama siyo wote, watakuelekezea macho na kukuita 'wa kuja', 'mshamba', na kila jina la fedheha, wakiona wao ndiyo wajanja. Halafu hapo ukitazama kwa makini, hao wajanja hakun hata mwenye ka-ist au akiba ya angalau 500K bank. Yaani ufahari wa kuitwa mjanja ilhali ikitakiwa 200K ya haraka unaanza kulia lia kwa watu.
3. Kuwa na mwenza mmoja.
Dunia hii, hasa kwa TZ, kwa uzoefu wangu mkubwa till this age, mtu akisema ana mpenzi mmoja watu wanamuona mshamba na wa kuja tu. Na ukizingatia wengi wanavyopenda kuishi kwa kushikiana akili, basi kila mmoja anaepuka kuonekana ana mpenzi mmoja. Sababu? Ili aonekane mjanja.
4. Kusimamia principles zako.
Ukiwa enforcer wa kanuni zako, Wa-TZ wengi watakuita mshamba. Watasema maneno kama, una ukoloni mwingi, mlugha lugha nk, ili kukudhoofisha.
5. Kutowajua kwa usahihi wanamuziki wa ndani na wa nje.
Limenitokea sana na zaidi kuliko yote. Si-dedicate my time mostly searching about lives and trends of the local and cross-border artists. Kwa nini? Kwa sababu hakuna faida yoyote niliyoi project. To me, it's some sort of wastage of time. Kuwahukumu watu kwa kuwaita wa kuja, kisa hawawajui artists wengi, siyo jambo jema.
6. Kuwa na company ndogo ya marafiki, au kutokuwa nayo kabisa.
Wengine wameumbwa hivyo, wanafurahi kuwa alone kuliko kujichanganya sana na watu. Jamii kubwa ya TZ ina uelewa mdogo wa hiki kitu. Ukisema mbele za watu huna marafiki, au una marafiki wachache, watakuita mshamba, wa kuja n.k, kitu ambacho siyo sawa. Ni bullying.
7. Kuvaa kawaida.
Leo hii ukivaa simple pasipo mikogo mingi, utabatizwa jina la mshamba. Ukivaa sendo, kaptura na T shirt ukazama kitaa, watasema ni mshamba. Kwa nini? Kwa sababu wanajua una vihela hivyo hutakiwi kuvaa simple. Nunua raba kali, nenda salon za 40k, vaa chains, vaa jeans kali n.k!
8. Kutosikiliza muziki.
Hili ndilo kabisa, binafsi limenikumba, kwa sababu sina muziki wowote kwenye simu yangu, na sisikilizi miziki kwa earphone. Not interested in music. Why niitwe mshamba?
9. Kutokuwa na kundi.
Kama nilivyosema awali, mjini hasa Dar, wengi wanaishi kwa makundi. Ukiwa alone na usiye na makuu, utaitwa mshamba. Makundi yanamaliza pesa, mostly. Hakuna faida yoyote ya msingi ya kuwa kwenye makundi.
10. Usipopeleka mtoto private.
Wa-TZ wengi ni duni mno kichwani. Ukiwa na uwezo na mwanao akasoma shule za serikali, watakuita siyo mjanja, yaani mshamba, wa kuja nk. Watanzania wengi ni kama wanajaribu ku programme maisha ya watu, kwamba yaende kama wanavyotaka wao. Watoto wengi tu wanasoma 'kayumba' na wazazi wana uwezo, na wanafanya vizuri.
11. Kutoshabikia mpira.
Hili sina haja ya kulieleza.
Hao watu wote, kiuhalisia si high minded, ni low IQ'd.
Ulaji wa ugali ni tatizo kwenye nchi yetu? Hali ngumu ya maisha? Elimu duni? Shida ni nini? Shida ni sumu kuvu?