Mamelod sundown watapitishwa katika tanuri la moto

Mamelod sundown watapitishwa katika tanuri la moto

mwehu ndama

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2019
Posts
630
Reaction score
2,151
Baada ya droo ya hatua ya robo fainali ya michuono ya caf champions league kufanyika hapo jana, kumekuwa na hisia mchanganyiko kuhusiana na timu zilizokutanishwa kukabiliana na wawikilishi wawili kutoka ligi ya Tanzania bara, simba na Yanga sc.

Wakati mashabiki wa Simba sc wakionekana kufurahia kukutanishwa na timu bora ya karne" Al ahly kutoka Egypt" furaha yao inaukamilisha ule msemo wa kiswahili usemao "usilolijua ni sawa na usiku wa giza" , sababu wasicbokijua mbumbumbu efusii ni kuwa wameingia katika mdomo wa mamba wakati akiwa na njaa, hakuna namna wataondokana na kipigo cha mbwa koko toka kwa mafarao hawa, kwa sababu Al ahly iko ilivyo Leo sababu ya hatua kama hizi katika michuano hii mikubwa kabisa kwa ngazi ya vilabu barani afrika.

Kwa upande mwingine timu dume na ngumu kabisa kwa sasa kutoka ukanda wa Cecafa Yanga Afrika, itakutana na mabwanyenye wa kabumbu kutoka bondeni mwa Africa katika ardhi ya madiba, naam hawa si wengine bali ni masandawana Mamelod sundown ukipenda waite the Brazilians!. Baada ya droo kuonyesha miamba hii ya soka itakutana, imepelekea uwepo wa hofu miongoni mwa mashabiki wa Yanga afrika kuelekea mchezo huu, huku mashabiki pinzani wa Yanga Afrika na wachambuzi uchwara wakionekana kufurahia mchezo huu wakiwa na imani kuwa sasa Yanga sc inaenda kukomeshwaa

Hahaha, manake hapo kwanza nchekee!!,wasilolijua mashabiki wa Mbumbumbu efusii na wachambuzi uchwara ni kuwa Yanga sc ina ubora wa daraja la juu zaidi kiwanjani na ni aina ya timu ambayo kamwe mamelodi hawatoweza kuisahau katika maisha yao baada ya mchezo husika kutamatika kwa mechi zote mbili.

Niulize kwa nini? Naam sababu ni moja tu, Yanga sc ni aina ya timu ambayo mamelod sundown hapendi kucheza nazo, Yes, offensive style ya Yanga sc ni tishio kwa timu yoyote ile barana Africa, mamelod sundown huwa anashinda mbele ya waarabu sababu ya style ya timu za kiarabu kiuchezaji, wako tactical sana, hususani wakiwa away na hata wakiwa nyumbani kuna muda huwa wanajilinda, kitu kinachowapa sana advantage mamelod, na ndicho kitu hichohicho kinachowapa sana faida yanga sc, sababu tangu wakati wa nabi, Yanga sc imekuwa ikifungua timu hata ugenini, ni either upishane nao, au upaki basi, lakini jua tu yanga sc watakushambulia bila hofu wala heshima sababu anayo quality ya kufanya hivyo.
.
Sasa basi, katika mchezo huu sio Yanga sc atakaekwenda kukutana na kipimo sahihi la hasha, bali mamelod sundown ambae anajiita timu bora Afrika ndio anakwenda kukutana na kipimo sahihi katika mchezo huu, Anakwenda kujaribiwa na Timu isiyokuwa na hofu wala adabu, anakwenda kujaribia na watu wasiokuwa na chakupoteza, yet still dangerous, anakwenda kujaribiwa na timu iliyojaa quality za kimataifa kwa ngazi ya soka la Africa, nasema hakuna namna midfield ya mamelodi itaweza kumzima pacome zouzou, naam hakuna njia wataweza kumzuia aziz ki wala aucho na maxi wasi operate katika level ya kikatili pale estadio de Benjamin mkapa.

Mamelod amazoea kuogopwa na kupakiwa basi, na wakati si timu yenye historia ya kutosha barani Africa, mara ya kwanza walitwaa hili taji mwaka 2016, pia tangu wakati huo wamefika nusu fainali mbili tu, hawa ni wakawaida, pesa haichezi mpira na ukitaka kuamini hivyo, UAE pamoja na pesa zao zote lakini timu ya ya taifa ni kishundu. Mamelod wako overrated, na niwakati sahihi Africa kuijua Yanga sc ya eng. Hersi kama timu isiyokuwa na adabu wala heshima kupitia mabwanyenye hawa.

Kwa kifupi mamelod wameyakanyaga na tanuru watakalo pitishwa ndani ya dakika 180 za dsm na kule Pretoria zitawaachia kidondo cha milele. Niko nimekaa paleeeee
 
Raisi wenu ulimsikia karata yake aliyoitoa kwa timu zitazocheza fainali?

Hersi alisema fainali itakuwa kati ya Mamelody na Al Ahly.

Wakati anasema maneno hayo ukumbuke timu yake bado ipo kwenye michuano haijatolewa.

Kwa hiyo mtu wa kwanza kabisa kuwakatia tamaa ni Raisi wenu mwenyewe.

Kabla hata sisi tusioipenda Yanga hatujatoa ya moyoni, tayari Injinia Hersi ametuwahi.
 
Raisi wenu ulimsikia karata yake aliyoitoa kwa timu zitazocheza fainali?

Hersi alisema fainali itakuwa kati ya Mamelody na Al Ahly...
Mpira ni mchezo wa dakika tisini, Kwani ukiwa na mke ndani inakuzuia kuona uzuri wa wanawake wengine nje? Swali itakuwa kama mbunye zao ni tamu kama ya mkeo? na hauwezi kudhibitisha hilo bila kulala nao, mamelod kapikiwa mkongo shekhee
 
Ukishabikia sana simba na yanga nati za kichwani zinaanza kulegea kwa nguvu.

Vilabu hivi vinaongeza idadi ya wajinga na wapumbavu kwenye nchi.

Mpira wa uongo uongo, bahasha na chupli binafsi niliacha kufuatilia.
 
Mpira ni mchezo wa dakika tisini, Kwani ukiwa na mke ndani inakuzuia kuona uzuri wa wanawake wengine nje? Swali itakuwa kama mbunye zao ni tamu kama ya mkeo? na hauwezi kudhibitisha hilo bila kulala nao, mamelod kapikiwa mkongo shekhee
Ukisikia kauli za

"Mpira unadunda"

"Mpira una maajabu yake"

"Mpira ni mchezo wa dakika 90"

"Kwenye mpira lolote linaweza kutokea",

"Tuwe na akiba ya maneno"

"Mpira ni mchezo wa makosa yeyote anaweza kufungwa "

Ukuona tu hayo maneno ujue hizo ni kauli za waoga.

Huwezi kuzisikia hizo kauli ikiwa timu yao inacheza na Dodoma Jiji au Namungo.

Ukiona series ya hizo kauli ujue watu washapima mzani na kuona hawana msuli wa kupambana na mpinzani huyo.
 
Baada ya droo ya hatua ya robo fainali ya michuono ya caf champions league kufanyika hapo jana, kumekuwa na hisia mchanganyiko kuhusiana na timu zilizokutanishwa kukabiliana na wawikilishi wawili kutoka ligi ya Tanzania bara, simba na Yanga sc...
nawaonea huruma sana mama lodi...km 2001 huko walitufunga kwa agg ya 6-5 yanga hii ya 2024 mama lodi atakandwa pengine nje ndani kama asipojiheshimu
 
nawaonea huruma sana mama lodi...km 2001 huko walitufunga kwa agg ya 6-5 yanga hii ya 2024 mama lodi atakandwa pengine nje ndani kama asipojiheshimu
Na huu ndio ukweli, watu wanaichukulia Yanga sc oya oya ila Yanga sc timu wanayo af quality ni daraja la juu sana kuliko maelezo, yaan mamelod huyu wa papatu na mazembe na wale wa Mauritius ndo aje kutamba kwa mkapa... Maaanina naweka nyumba hawa maboya wanaondoka
 
cha ajabu siku hiyo watakaondwa mamelodi ila watakaojinyea makolouzdad
 
Raisi wenu ulimsikia karata yake aliyoitoa kwa timu zitazocheza fainali?

Hersi alisema fainali itakuwa kati ya Mamelody na Al Ahly.

Wakati anasema maneno hayo ukumbuke timu yake bado ipo kwenye michuano haijatolewa.

Kwa hiyo mtu wa kwanza kabisa kuwakatia tamaa ni Raisi wenu mwenyewe.

Kabla hata sisi tusioipenda Yanga hatujatoa ya moyoni, tayari Injinia Hersi ametuwahi.
Ile ni fasihi wewe mbumbumbu
 
UKISHABIKIA SANA SIMBA NA YANGA NATI ZA KICHWANI ZINAANZA KULEGEA KWA NGUVU.

Vilabu hivi vinaongeza idadi ya wajinga na wapumbavu kwenye nchi.

MPIRA WA UONGO UONGO, BAHASHA NA CHUPLI BINAFSI NILIACHA KUFUATILIA.
Naunga mkono hoja
 
Nnacho amini Kocha wetu hawezi tuangusha wanachi
 
Back
Top Bottom