Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
TAARIFA KWA UMMA: MAMEYA NA WAFANYABIASHARA COMORO KUSHIRIKI MAONESHO YA SABASABA
Kufuatia juhudi za utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi, Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) umefanikiwa kushawishi jumla ya Wafanyabiashara 42 kutoka nchini humo kushiriki maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu SABASABA. Pia, Mameya Wanane (8) wa miji mbalimbali ya kisiwa cha Anjouan nchini humo wanatarajiwa kufanya ziara kipindi hicho na watatenga muda kutembelea eneo la Maonesho.
Wafanyabiashara hao wanatoka visiwa vyote vya Comoro ambapo wanawakilisha Sekta zinazojishughulisha na Biashara ya vifaa vya ujenzi, nguo, Kampuni za maji, vinywaji, wafugaji, na vyakula vya Mifugo, pamoja na bidhaa za Kilimo hasa mazao ya mizizi.
Kwa upande wa kipekee, ushirika unaojihusisha na uzalishaji wa mazao ya Vanilla na Langilangi unatarajiwa kushiriki. Hatua hiyo inatarajiwa kutoa fursa kwa wenyeji kujionea mbinu za uzalishaji na kuongezea thamani mazao hayo. Vanilla na Langilangi ni mazao muhimu kwa Kampuni zinazotengeneza manukato.
Akizungumzia ushiriki huo, Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Mheshimiwa Saidi Yakubu alieleza kuwa idadi hiyo ni kubwa kuwahi kujitokeza kutoka Comoro na wengi wao wanakwenda kwa lengo la kuangalia vyanzo vya usambazaji wa bidhaa za Tanzania zinazohitajika Comoro. "Bidhaa za Tanzania zina soko kubwa Comoro ambapo mahitaji makuu ni pamoja na zana za Kilimo, mazao ya Kilimo, nyama na wanyama hai, vyakula vya Mifugo. Aidha, wafanyabiashara hawa wameomba pia kupata fursa ya kufanya vikao na wafanyabiashara wa Tanzania pembezoni mwa maonesho hayo" alisema Balozi Yakubu.
Biashara baina ya Comoro na Tanzania imekuwa ikiongezeka katika miaka ya hivi karibuni ambapo takriban mauzo ya kiasi cha Shilingi 148bilioni yalifanyika kwa bidhaa za Tanzania kwa mwaka 2023. Biashara kubwa inafanyika miezi ya Julai hadi Desemba kila mwaka.
Nayo Nchi ya Comoro imekuwa na mchango mkubwa katika kusaidia utekelezaji wa mikakati ya kuendeleza uchumi wa buluu kwa upande wa Tanzania. Nchi hiyo inasafirisha boti za fiber kwenda Tanzanzia. Takriban boti 100 husafirishwa kwenda Tanzania hasa Zanzibar, kila mwezi. Boti hizo zimejijengea sifa kubwa kwa watumiaji nchini Tanzania ikilinganishwa na boti kutoka Kampuni nyingine.
Wafanyabiashara wa Tanzania watakaopenda kuwasiliana na wafanyabiashara wa Comoro watoe taarifa kupitia simu namba +269 773 78 50 na Barua Pepe moroni@nje.go.tz
IMETOLEWA NA
UBALOZI WA TANZANIA - COMORO