#COVID19 Mamilioni ya watu duniani huenda wakapoteza ajira kutokana na Corona

#COVID19 Mamilioni ya watu duniani huenda wakapoteza ajira kutokana na Corona

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Shirika la kazi duniani ILO limesema mamilioni ya watu ulimwenguni wamepoteza ajira zao au kupunguziwa muda wao wa kufanya kazi kufuatia janga la virusi vya Corona.

Katika ripoti yake ya tathmini iliyotolewa leo shirika hilo la kimataifa limeeleza kwamba, ikiwa janga hilo halitoongezeka soko la ajira linapaswa kuanza kurudi kwenye hali nzuri katika kipindi cha nusu ya pili ya mwaka.

Hata hivyo kwa mujibu wa shirika hilo katika mwaka 2020 asilimia 8.8 ya masaa ya kufanya kazi kwa watu duniani yalipotea. Watu milioni 220 duniani kote huenda wakakosa ajira mwaka huu na watu milioni 205 wakakosa ajira mwaka ujao.
 
Sasa mbona hilo shirika la kazi halitowi Muongozo, kua tutaishi vp bila kazi?
 
Naona athari za corona zimeanza kupungua sana kwa sasa.

Uchumi baadhi ya nchi umeanza kurudi na ajira zinaanza kurudi pia.
 
Hili janga sijui tuseme la asili au la kujitakia vyovyote vile tuliite lakini limetuonyesha namna mwanadamu si kitu, hivyo tusijiinue Sana kwamba tumeujua ulimwengu barabara bali Kuna vilivyo juu yetu, vikiamua tu kuonyesha uwezo wa japo kwa asilimia chache mwanadamu anabaki mdogo Sana.
 
Baba alisema lazima tujifunze kuishi nalo sasa naamini ni kweli
 
Back
Top Bottom