KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 82
- 150
Ni kama Mamlaka zinazohusika na utunzaji wa mazingira katika Wilaya ya Bariadi, zimeruhusu uharibifu huu wa mazingira unaofanya kwenye vyanzo vya maji. "Uchimbaji wa mchanga katikati ya mito".
Uharibifu huu umeanza muda mrefu lakini hakua hatua zinazochukuliwa, wachimbaji wa mchanga wenyewe wanasema serikali imeruhusu maana kila siku inawatoza ushuru.
Ukitembelea mito yote ambayo inazungumka mji wa Bariadi, yote inachimbwa mchanga ambao unatumika katika shughuli za ujenzi, na wachimbaji wanachimba katikati kabisa ya mito hiyo na kwingine wameanzia kwenye kingo za mito wakielekea katikakati ya mto wenyewe.
Asilimia zaidi ya 90 ya mito hiyo ndiyo tegemeo kwa Mamlaka ya maji Bariadi (BARUWASA), kwani visima vyake vingi virefu vimechimbwa kandokando ya mito hiyo.
Mamlaka kundelea kuruhusu uharibifu huu wa mazingira, ni kuhatarisha maisha ya wananchi wa mji wa Bariadi.
Lakini pia ni kushindwa kutimiza wajibu, kwani sheria zipo wazi na zinaeleza kuwa ndani ya mita 60 ya chanzo chochote cha maji hakuna shughuli yeyote ya kiuchumi inatakiwa kufanyika.
Mara kadhaa Rais Dkt Samia na Makamu wa Rais, wamekuwa wakikemea uvamizi wa vyanzo vya maji na wameagiza mara kwa mara mamlaka zilinde hivi vyanzo, lakn Bariadi wahusika wameshindwa kutii maagizo ya viongozi.