Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,443
- 4,006
Wakuu na mamlaka husika (Wizara Elimu na TAMISEMI)
Uzi wenye sura ya swali umeletwa jukwaani hapa baada ya kufanya jitihada za kutosha kutafuta mwongozo wa kuaminiwa kutoka serikalini , lakini imeshindikana kupata.
Taratibu za sasa katika utafutaji ajira na kujiendeleza kielimu unahitaji uwe na cheti cha 'leaving cettificate', 'academic certificate', cheti cha kuzaliwa, kitambulisha cha uraia au kura, hati ya kusafiria au leseni ya udereva kuhakiki majina, umri, uraia, sura ya muombaji na kulinganisha uelewa wa mhusika kuhusu vyeti alivoambatanisha kama kweli ni vya kwake au katengenezewa 'stationery' kwa malipo.
Zamani cheti cha 'leaving certificate' kilikuwa kinatolewa na mwalimu mkuu wa shule husika lakini siku hizi kuna utata ambao ningependa kupata ufafanuzi wa kipi ni kipi.
Je, ni kweli kuna wakati vyeti hivyo vilisitishwa kutolewa na kwa sababu gani? Kama ni kweli ilikuwa lini na iliathiri shule zipi? (Serikali/binafsi).
Ni nani kwa sasa ana mamlaka ya kutoa vyeti vya 'leaving certificate' vya shule msingi na kidato cha nne/tano?
Wadau na Serikali ninaomba ufafanuzi tafadhali.