Mamlaka inayosimamia ‘parking’ za gari iwajulishe Wateja kuhusu Madeni ya miaka ya nyuma na siyo kuwashtukiza na kutaka walipe papohapo

Mamlaka inayosimamia ‘parking’ za gari iwajulishe Wateja kuhusu Madeni ya miaka ya nyuma na siyo kuwashtukiza na kutaka walipe papohapo

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Miezi kadhaa iliyopita kuliibuka Watu waliokuwa wanakamata magari Jijini Dar es Salaam kwa wale ambao hawakuwa wamelipia ada za maegesho.

Kuliibuka usumbufu mkubwa kwa kuwa watu waliokuwa wakikamatwa walikutwa na madeni ya miaka ya nyuma ambayo hata wengine hawayajui au hawayakumbuki.

Mamlaka zikajitokeza kufafanua kuwa madeni hayo hayakulipwa kwa sababu za kimfumo, sikumbuki vizuri wao wenyewe wanajua walichokisema, hoja yangu ni kuwa usumbufu huo unaendelea na wahusika wengi hawajui madeni yao hali inayosababisha usumbufu kwa kiasi kikubwa.

Kwa sasa nimesikia kuwa mfumo huo wa madeni upo chini ya TAMISEMI, kama ni kweli kwa nini wasitume ujumbe kwa wale wanaodaiwa kwenye namba za simu kwa wahusika wenye magari.

Inawezekana wasifikiwe wote kwa kuwa wengine walishabadilisha namba za simu, waliuza magari, au hawana tena hayo magari kwa namna yoyote, lakini hii tabia ya kumsapraizi mtu kumwambia anadaiwa kisha ukamtaka alipe papo kwa hapo, haijakaa sawa.

Juzi nimekamatwa maeneo flani na hao wanaotoza malipo ya parking wakaniambia nilipe elfu 50 na kama sina salio basi niendelee kubaki nao hadi jioni, hivi hii ni sawa?

Hapo mimi nina nafuu kuna mwamba aliambiwa anadaiwa zaidi ya 200,000 akatakiwa kuilipa papo hapo, akasema hiyo gari aliinunua kwa mtu hakujua kama ina deni kubwa hivyo.

Hivyo, wito wangu kwa Serikali kutafuta namna ya kuwafikishia ujumbe wanaodaiwa hata kama ni kwa njia ya sms kwa kuwa madeni ni ya miaka ya nyumba, sio rahisi mtu kukumbuka na kuwa na gari haimaanishi wewe unatakiwa kutembea na hela nyingi muda wote.

Pia soma:
~
Wanaohusika kudai fedha za ‘parking’ kwa kusimamisha magari barabarani, wamekuwa kero kwa Wananchi!
~ TAMISEMI: Mfumo wa kusoma madeni ya parking ulipata hitilafu ukashindwa kutuma ujumbe kwa wenye magari
 
kwa walio dar es salaam ikiwa unaweka mashaka juu ya deni la parking nenda pale anatouglou utapatiwa ufumbuzi maana kwa mfumo walionao wanaona kila kitu kwa picha mnato.

tamisemi wakiweza kuuboresha mfumo wao ili mteja aweze patiwa 'access' ya kuona kwa picha kila siku aliyotumia parking za umma ingepunguza kama si kuondoa kabisa malalamiko juu ya kubambikiwa madeni ya parking.
 
Unamix kaka.

Ili deni la trafiki sio la parking.
Nimeelekeza yote pia aweza download app ya serikali ya GePG ina kila kitu humo mambo ya madeni ya traffic ,mambo ya parking fees nk unaona madeni yote ya nyuma ya gari
 
Yaani unaibiwa mchana kweupeeeeeee
Kuna mmoja humu aliwahi sema amelipa hela ya mwezi na bado akakuta deni lipo tu

Kwa tafsiri nyepesi na ya haraka ni wizziiiii wiziiiii wiziiiiii
 
Yaani unaibiwa mchana kweupeeeeeee
Kuna mmoja humu aliwahi sema amelipa hela ya mwezi na bado akakuta deni lipo tu

Kwa tafsiri nyepesi na ya haraka ni wizziiiii wiziiiii wiziiiiii
Kila ukilipa baada muda ukicheki unakuta kuna deni tena!!
 
Huduma nyingi za kimfumo zinazotolewa na tamisemi ni mbovu mnoo,,hiii wizara ina mambo yakikoloni mnoo
 
Back
Top Bottom