KERO Mamlaka Jiji la Mwanza mulikeni wavuta sigara wanakera

KERO Mamlaka Jiji la Mwanza mulikeni wavuta sigara wanakera

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

ngulyabhule

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2020
Posts
226
Reaction score
377
Juzi nilijaaliwa kuingia jijini Mwanza sasa leo nikaona nitoke nilifahamu japo kidogo jiji hili! Hakika kwa ujenzi wa SGR nimeshuhudia unaendelea lakini pia nimependa kuona ujenzi wa soko kuu japo nimeona paa lake tu but hope litakuwa soko zuri!

Sasa kilichonikera ni hii tabia ya wavuta sigara wa hili jiji hakuna nidhamu ya kujali wangine wasio vuta kwa maana maeneo niliyo jaaliwa kupita mfano dukani hata mkiwa watatu mtu ana washa sigara ilhali wengine wapo kwenye foleni anatoka na kuacha moshi wa sigara hapo dukani ukiwakera wengine hadi nikaamua kuondoka!

Mbaya zaidi ni hii tabia ndani ya soko la MLANGO MMOJA eneo hili nimeambiwa lina uongozi lakini bado watu wapo huru humo ndani kuvuta sigara hili ni eneo la mkusanyiko wa watu wa kila namna lakini wavuta sigara wanakera sana kwenye hili eneo nitoe rai kwa uongozi wa hili eneo kukomesha hii tabia.
 
Back
Top Bottom