Mamlaka kuchelewa kuzichukulia hatua kwa wakati 'kampuni bubu za upatu', Je wanachelewa kupata taarifa au?

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
Katika kipindi ambacho teknolojia inaendelea kukua kumekuwepo na ongezeko la michezo mingi ya upatu hasa kupitia mitandao (digital platforms), katika michezo hiyo kumekuwepo na ugumu wa kutambua ni kampuni zipi zenye usajili halali jambo ambalo limekuwa gumu kuwaondoa watu wengi kwenye mtego wa kutapeliwa.

Katika udadisi, inabainika vijana wengi kutokana na kukabiliwa na hali ngumu ya kimaisha inayochangiwa na changamoto ya ukosefu wa ajira wamejikuta kwenye mtego wa kutapeliwa kirahisi huku wakibakia kujifuta machozi.

Ni kwa mara kadhaa imekuwa ikiibuka michezo ya upatu au kamali inayochezwa kwa njia za Mtandao, ambapo tumekuwa tukiona watu wengi wakiwekeza fedha zao na muda wao mwingi huku michezo hiyo ikiendeshwa kama michezo halali bila kificho.

Kutokana na kufanyika kwenye mazingira ya uwazi hali hiyo imekuwa kichocheo cha wengi kuingia kwenye mnyororo huo, ambapo hilo limechangia hamasa kuwa michezo hiyo imepewa uhalali na mamlaka.

Hata hivyo inashangaza katika baadhi ya michezo ya upatu inaweza kuendeshwa hata kwa zaidi ya miezi mitatu bila kificho huku mamlaka za kisheria zikiwa kimya bila kuchukua hatua za wazi, jambo hilo linanifanya nijiulize kwamba wanakuwa hawana taarifa za mambo yanayoendelea kwa Wananchi wake licha ya kufanyika kwa uwazi?

Mfano kwa mara kadhaa tumeona mamlaka zinachukua hatua baada ya muda kupita, nyakati ambazo watu wengi wanakuwa tayari wametapeliwa huku hatma ya fedha yao inakuwa haijulikani, mfano juzi tumesikia kwamba mamlaka zimewakamata baadhi ya Maafisa wa LBL kwa kuendesha mchezo wa upatu bila kuwa na kibali kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kama sheria zinavyoelekeza, lakini tujiuluize kampuni hiyo bubu imeanza kuendesha michezo hiyo kwa muda gani?

Huo ni mfano tu, pia tumewahi kuona hilo pia kwa Qnet na kampuni bubu nyingine zikichukuliwa hatua baada ya kundi kubwa la watu kupingwa pesa zao licha ya kuwepo kwa uwezekano wa kuthibiti tatizo hilo kabla halijawa kubwa.
photo_2025-02-25_16-53-36.jpg
Mantiki kubwa ya andiko hili ni kuhoji juu ya uwajibikaji wa mamlaka zilizopewa dhamana, je, zimeshindwa kuwa na vyanzo muhimu vya kubaini mtandao unaoendesha michezo hiyo kinyume na Sheria mapema kabisa kabla wananchi wengi hawajalizwa!

Inaibua mashaka kwa vyombo vyetu au mamlaka kuchelewa kuchukua hatu juu ya vitendo vya uvunjifu wa Sheria ambavyo viko wazi na matokeo yake yanaathiri kundi kubwa la watu katika jamii, hususani kundi la vijana ambao kilio chao kikubwa ni ugumu wa maisha.

Uenda lawama zikaelekezwa pia kwa Wananchi ambao wamekuwa waathirika, lakini mamlaka zimepewa jukumu la kusimamia uzingatiwaji wa Sheria, hivyo wapo Wananchi wanaoweza kuaminishwa kwa uwazi unaokuwepo kwamba baadhi ya michezo inayoendeshwa inazingatia misingi ya Sheria na taratibu, licha ya kuwa mwisho wa siku wanaangukia kwenye mikono ya kutapeliwa.

Wito wangu kwa mamlaka ni vyema kusimamia vyema Sheria na kuwajibika kwa wakati kuwaepusha watu wengi kuingia kwenye mitego ya kutapeliwa, kinyume na hivyo inaibua hisia za mashaka ya wao pia kujitenga na mnyororo wa mtandao huo ambao umekuwa ukiwanyonya wananchi.

Pia, suala hili linaweza kutoa taswira hasi juu ya mamlaka zetu za kiusalama namna zilivyowekeza katika kupambana na uharifu wa kimtandao. Ni muhimu eneo hilo likapewa nguvu ili kuweza kubaini mapema kuthibiti uharifu na utapeli ambao umekuwa ukielekezwa huko kwa kuzingatia Sheria.

Lakini yawekwe mazingira na vithibitisho vya wazi vinavyoweza kumfanya mwananchi kubaini uhalali wa kampuni zinazoendesha upatu ili kuwanasua wengi kwenye mtego wa utapeli, pia hatua hiyo itasaidia kulinda hadhi ya taasisi zenye uhalali huku pia mbinu hiyo ikiongeza nafasi ya mamlaka kupata taarifa zaidi.

Hata hivyo licha ya kusisitiza hayo na kutoa wito, nikumbushe kuwa kampuni hizo bubu zimekuwa zikihusika kukusanya taarifa za watu, je taarifa hizo zinakuwa salama kama sheria zinavyoelekeza.
 
Uzi mrefu mno, ungeandika tu serikali ilikuwa wapi hadi LBL ikaoparate siku zote hizo?
 
Ni ''mamlaka'' gani unazungumzia ewe mdanganyika? Kweli mnachekesha. Nchi wewe unaona ina viongozi wanajua ni nini maana ya kuongoza?
 
Uzi mrefu mno, ungeandika tu serikali ilikuwa wapi hadi LBL ikaoparate siku zote hizo?
Serikali isihusishwe na hao wapumbavu wanaochukua hela zao wenyewe ambazo walitakiwa kulipa ada za shule na kuwapelekea hao matapeli kila mara. Pyramid schemes nyingi zimetapeli watu mkiambiwa hao matapeli mnawatuka wanaowakatazq kupeleka hela "zenu".
 
Akili kumkichwa usitegeme mamlaka I've ikuokoe

Ova
 
Serikali isihusishwe na hao wapumbavu wanaochukua hela zao wenyewe ambazo walitakiwa kulipa ada za shule na kuwapelekea hao matapeli kila mara. Pyramid schemes nyingi zimetapeli watu mkiambiwa hao matapeli mnawatuka wanaowakatazq kupeleka hela "zenu".
Wajinga kabisa

Ova
 
Back
Top Bottom