KERO Mamlaka ya Bodi ya Korosho wanasema pembejeo zipo za kutosha lakini huku vijijini hatupati

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
​
Ugawaji wa pembejeo za kilimo kwa zao la Korosho kuna ulakini, Mamlaka ya Bodi ya Korosho wanasema zipo za kutosha lakini huku vijijini hatupati, yaani wengine hatujapata lakini hata baadhi ya wachache waliopata pia hazikidhi mahitaji.

Soma Pia: Polisi Mtwara wakamata Viongozi AMCOS na Watumishi wa Umma kwa wizi wa Pembejeo za Korosho zaidi ya Milioni 15

Mfano, Mkulima mwenye shamba la hekali 15 anatakiwa kupata mifuko ya Salfa 15 lakini anapewa mifuko 5, tunashindwa kuelewa, mimi nipo Kijiji cha Nyengedi, Jimbo la Mtama.
 
Siasa kila mahali kiukweli misimu hii miwili pembejeo zimekuja kwa kusuasua mno na msimu huu ndipo hali imezidi,,,ila bodi ya korosho wakatoa pesa kwaajili ya kampeni za cccm Kuna muda huwa naamini kuwa mweusi ni laana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…