Mamlaka ya Hali ya hewa Kenya yadai mvua inayotakiwa kunyesha nchini humo imekwama Tanzania

Venus Star

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
26,519
Reaction score
78,311
Mamlaka ya hali ya hewa Kenya imetoa malalakiko kuwa mvua ayake imezuiliwa Tanzania.
Hivi ni mwendelezo wa vituko vya wakenya. Uwezo wa wakenya kufikiri kadili ya siku zinavyoenda unazidi kudidimia na kuisakizia Tanzania kila jambo baya linalowatokea.

Idara ya hali ya hewa Kenya: Mvua imekwama Tanzania

Idara ya hali ya anga nchini Kenya inasema kuwa kiangazi kitaendelea hadi mwisho wa mwezi huu huku upepo wa mvua ukisalia nchini Tanzania kutokana na kiwango cha chini cha upepo.

Mvua ndefu itaanza kunyesha katika maeneo mengi ya Kenya ifikiapo miwsho wa mwezi huu, wataalam wa hali ya anga wamesema.

Kaimu mkurugenzi wa shirika la hali ya anga nchini Kenya Stella Aura alielezea kwamba upepo wenye mvua umekwama nchini Tanzania kutokana na shinikizo ya kiwango cha chini ambayo haiwezi kuisukuma mvua hiyo kuelekea kaskazini mwa Kenya.

Mwezi Aprili ndio mwezi wa mvua ndefu nchini Kenya na onyo limetolewa katika maeneo kadhaa ya Kenya kuhusu kuchelewa kwake.

''Mvua ya msimu husababishwa na upepo wa mvua unaoelekea kaskazini lakini kufikia sasa upepeo huo haujaelekea kaskazini'', aliambia vyomb vya habari.

''Mvua imekwama nchini Tanzania, mifumo ya upepo iliopo kusini haijashikamana kuweza kusukuma mawingu hivyobasi mvua itachelewa , lakini mvua itaanza kunyesha mwisho wa mwezi huu'', alisema.

Mvua Ndefu
Hatahivyo amesema kuwa mvua ndefu imeanza lakini kwa kiwango kidogo katika maeneo mbalimbali.

Mvua ndefu hunyesha miezi ya Machi, Aprili, na Mei hususan katika eneo la magharibi , bonde la Ufa na mkoa wa kati na ni muhimu sana katika sekta ya kilimo hatua inayosababisha kuwepo kwa chakula cha kutosha.

Idara hiyo imewashauri wakulima kupanda mimea inayokuwa kwa haraka na ile isiotegemea maji kwa kuwa mvua hiyo huenda isinyeshe kwa muda mrefu.

Mafuriko
Wale wanaoishi katika maeneo ya nyanja za chini ikiwemo miji midogo isio na mitaro ya kusafirisha maji walionywa kwamba watarajie mafuriko.

Magharibi mwa Kenya, visa vya radi vinatarajiwa kuongezeka huku maporomoko yakitarajiwa kufanyika katika maeneo ya juu ikiwemo Murang'a na Meru miongoni mwa mengine.

Maporomoko pia yanatarajiwa kuathiri maeneo ya magharibi na mkoa wa Bonde la Ufa.

''Mikakati inafaa kuwekwa ili kuzuia maafo yoyote'' ,ilishauri idara hiyo.
 
Katika hali isiyo ya kawaida, mamlaka ya hali ya hewa ya Kenya imesema kuwa mawingu yenye mvua yamekwama Tanzania.Habari zaidi tembelea Bbcswahili.

Sent from my TA-1024 using Tapatalk

=====

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu tuna njaa kali ya kodi,halafu Kenya wanaleta mzaha.Watamjua Magu haki ya nani.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my TA-1024 using Tapatalk
 
hahajaja yalikuwa yanaenda Kenya kwa usafiri gani?
je? ni lini watatuma wataalamu kuyakwamua mawingu haya (mwandishi ilitakiwa ahoji)

sema kiswahili kinazingua itakuwa alikuwa na maana kwamba mawingu ya kuleta mvua yameishia Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…