SoC02 Mamlaka ya Kiserikali na Utawala wa Sheria

Stories of Change - 2022 Competition

Loyadom

Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
54
Reaction score
51
MAMLAKA YA KISERIKALI NA UTAWALA WA SHERIA.
(Governmental powers and rule of law)

UTANGULIZI.

Ni kuhusu madaraka ya serikali na utawala wa sheria je, serikali inapo telekeleza mamlaka yake inafanya hivyo kulingana na sheria au inaenda tofauti? Karibu Tujifunze..

Serikali. Ni taasisi yenye mamlaka ya kuratibu,kusimamia na kufanya maazimio kwa wote katika suala Fulani pia serikali inalo jukumu la kutunza na kutekeleza sheria, kanuni, miongozo na kuendesha shughuli muhimu za umma kwa kuzingatia utawala wa sheria.

Serikali kama taasisi ina mamlaka yake ya kusimamia na kutekeleza shughuli zake hata hivyo mamlaka hayo yanatakiwa kufanyika kwa kuzingatia Haki na usawa kwa raia wote na bila kwenda tofauti na takwa la sheria.

Utawala wa sheria, hii ina maana kua kila mtu pamoja na taasisi zote wapo chini ya sheria na hakuna alie juu ya sheria (usawa mbele ya sheria) hii imeandikwa katika sheria nyingi za kimataifa na kitaifa pia. Kwa mfano Katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, utawala wa sheria umewekewa misingi kwenye ibara ya 3, 4 na 13.

Kwa mfano, Ibara ya 13 ya katiba ya Tanzania naya Zanzibar ya mwaka 1984, kifungu cha 12 zote hizi zinatafasri na kufafanua juu ya usawa mbele ya sheria.

Hivyo basi Utawala wa sheria ni dhana inayoeleza namna mamlaka ya nchi pamoja na serikali yanavyotekelezwa kihalali iwapo tu yanafanywa/ yatafanywa kwa kufuata sheria.

Kwa maana hiyo sheria zinazoruhusu mabavu hazina nafasi katika serikali inayozingatia utawala wa sheria na mamlaka yote ya serikali yanapaswa kufanyika kwa kuzingatia utawala wa sheria.

Serikali nyingi zinajengwa/kuundwa na mihimili mitatu ambayo ni-;
Rais.

Raisi ndie mkuu wa nchi na serikali na anahusika kusimamia mambo mengi nchini ikiwepo utekelezaji wa shughuli za serikali, mamalaka ya kuteua watu kushika nafasi mbalimbali, uwezo wa kutoa msamaha kama ilivyo fafanuliwa Sura ya pili ya Katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Bunge.

Bunge lina kazi kubwa ya kutunga sheria bila kuingiliwa na yeyote ambapo wawakilishi wa bunge huchaguliwa na wananchi na sheria hizo hutumiwa na Nchi katika Nyanja mbalimbali.

Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia ibara ya 62 hadi 65 imefafanua Bunge la Tanzania na majukumu yake.

Mahakama.

Kazi yake kubwa mahakama kama muhimili unaojisimamia ni kusuruhisha na kutatua migogoro ya watu na serikali pia na ina jukumu la kuhakikisha usawa mbele ya sheria kwa watu wote bila ya kuingiliwa na yeyote na bila kujali cheo, dini au rangi ya mtu fulani.

Serikali kamili katika kutekeleza shughuli za umma ni yenye kufanya kazi zake kwa kuzingatia utawala bora ambao unazingatia utawala wa sheria ikiwa ni pamoja na kuzipa nafasi nguzo kuu (3) Tatu za serikali kufanya kazi bila kuwa na muingiliano wa aina yeyote isipo kua tu kama kuna kuangalia na usawa katika utendaji wa mihimili hiyo.

Utawala wa sheria, Huu unahitaji kila kitu kifanyike kwa mujibu wa sheria, inamaanisha kuwa pamoja na vyombo vyote vya umma viendeshwe kwa mujibu wa sheria na hakuna mtu yeyote ambaye ataathiriwa au kuaathirika au mali yake isipokua kila kitu kitafanyika kwa mujibu wa sharia.

Usawa mbele ya sheria unahitaji kuwepo na sheria zinazo simamia na kulinda haki za watu, zinazosimamia utawala wa sheria na zisizo hujumu haki hizo na uhuru wa watu wenyewe. Hata hivyo, Hii haiilazimishi serikari kutekeleza Haki zote kwa raia wake kama ilivyo oneshwa kwenye katiba kuna kizuizi katika ibara ya 30 ya katiba ya jamuhuri ya muungano ya Tanzania ya mwaka 1977.

Kwa kuzingatia utawala wa sheria hapo ndipo utulivu wa watu na mali zao pia unaweza kupatikana kitu ambacho ni muhimu katika maendeleo ya Taifa, Serikali inatakiwa kuzingatia sheria za Nchi husika katika kufanya shughuli muhimu za umma na itaepusha pia migogoro kati ya serikali na raia wake.

Kutokana na sheria za Tanzania hasa sheria mama Katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania katika ibara tofauti kama tulivyo elezwa hapo juu, Serikali yetu inaongozwa kwa kuzingatia Utawala wa sheria na hivi ndivyo inatakiwa kuwa japo kuna changamoto nyingi katika utekelezaji wake.

Kuna umuhimu wa uimarishaji wa utawala wa sheria nchini kama ilivyo elezwa na Ndg George M. Masaju (DAG) Deputy attorney General (Naibu mwanasheria mkuu wa serikali) Wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria Nchini mnamo tarehe 6 februari 2013 Dar es salaam.

Nguzo muhimu za utawala wa sheria.

Katika utawala wa sheria kuna nguzo muhimu ambazo zinatakiwa kuzingatia ili kuimarisha utawala huu nguzo hizo ni-:

Kuwepo kwa uhuru wa Mahakama.
Kama ilivyo elezwa hapo juu mahakama ni muhimili wa serikali na unatakiwa kufanya kazi zake bila kuingiliwa na muhimili mwingine isipokuwa kama kuna kuangalia utendaji wake, Mahakama itahitaji kua huru katika utoaji wa haki na ni chombo chenye mamlaka na kauli ya mwisho ya utoaji wa haki nchini pia inatakiwa kutenda haki kwa wote bila ya kujali hali ya mtu kiuchumi au kijamii, hii ni kama ilivyo elezwa ibara ya 107A ya Katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Dhana ya kuchukuliwa kutokuwa na hatia (Presumption of innocence).
Kila mtu anadhaniwa kua hana hatia mpaka pale vyombo husika vitakapo baini hatia ya mtu Fulani hii yote ni kuhakikisha haki na usawa kwa wote, Kama shauri la mtuhumiwa bado linachunguzwa hairuhusiwi kumuhukumu mpaka pale itakapo thibitishwa baada ya uchunguzi hii pia imeelezwa katika ibara ya 13(6) b ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Mgawanyo wa madaraka (separation of powers).
Hii ndio inakua ngumu kuitekeleza katika utendaji wa kazi sheria inahitaji mgawanyo uwepo kati ya Utawala (executive), Bunge na Mahakama Lengo ni kuzuia muhimili mmoja kua na madaraka makubwa na kua na nguvu kuzidi mingine ambayo imeelezwa pia katika ibara ya 4 ya katiba inaainisha utekelezaji wa shughuli za mamlaka.

Zipo nguzo nyingi na hizo ni baadhi tu tukiangalia kwa hizo chache ni nguzo baadhi tu ndizo hutekelezwa kama sheria inavyo eleza nguzo zingine hazitekelezwi kwa usahihi hasa mgawanyo wa madaraka kuna uhitaji wa uimarishaji wa nguzo hii ili tuwe na utawala bora wa sheria nchini.

IMEANDALIWA NAMI: Chades.
Email. chadesluckius@gmail.com
 
Upvote 2

Na
 
Naomba unipigie kura ukimaliza kusoma kwa kubonyeza alama ^ hapo chini baada ya story.
 
2. Acha niisome kwa utulivu afu nije na hoja
 
Back
Top Bottom