A
Anonymous
Guest
Mamlaka hii inayosambaza Maji ya bomba viijiji vya Lyamungo, Umbwe, Sambarai, Manushi juu na chini, Mailisita, Kimashuku, Mbatakaero, Longoi na Kinamiri, imekuwa kero kwa miezi kadhaa Sasa.
Wateja wake tunaotegemea kupata Maji safi ya kunywa na mahitaji mengine ya msingi tumekuwa kwenye mateso tangia mwezi wa saba mwaka huu Kwani Maji yanatoka mara moja kwa mwezi na Maji yenyewe yanatoka kama mkojo wa mtoto(kidogo) na bado bili zinakuja kama kawaida.
Tatizo limekuwa kubwa zaidi maeneo ya tambararae hasa vijiji vya Longoi na Mbatakero kiasi Kwamba, wananchi tumelazimika kurudi enzi za kale kufuata Maji mto Kikavu Maji ambayo ni machafu kutokana na mwingiliano na wanyama.
Hadi muda huu ninapoandika ujumbe huu,tangia mwezi wa saba Maji yametoka si zaidi ya mara 3. Wengi tunalazimika kujisaidia porini kwa sababu hatuna Maji ya kutumika kwenye vyoo tulivyonavyo.
Kwa bahati mbaya,Kila tukipiga namba ofisi za idara zilizoko Lyamungo,tunajulishwa kuwa hakuna mgao wa Maji lakini sisi Maji hatuyaoni.
Namba ya fundi mkuu 0754 362 973 ukipiga anasema Maji yapo lakini kiuhalisia tumeteseka na tunaendelea kuteseka,ingali bili zinakuja kama kawaida.
Nimeamua kuwa sauti ya wengi wanateseka na Hali hii,pengine Viongozi wetu wa ngazi mbalimbali wataona sababu vijiji takribani 6 tatizo hili limekuwa kongwe zaidi na hakuna wa kutusemea.
Naomba wahusika kuanzia ngazi ya wizara itusaidie tuweze kupata Maji Kwani tupo jangwani ambako Maji haya yalikuwa msaada sana kwetu.