KERO Mamlaka ya Maji Mhanuzi - Meatu Mkoani Simiyu inatuhudumia maji yenye tope, ni kweli hakuna chujio?

KERO Mamlaka ya Maji Mhanuzi - Meatu Mkoani Simiyu inatuhudumia maji yenye tope, ni kweli hakuna chujio?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

KwetuKwanza

Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
82
Reaction score
150
Mimi ni mdau natokea Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, naishi hapa makao makuu ya Wilaya, Mjini Mhanuzi.

Sisi Wananchi wa makao makuu ya Wilaya hapa Meatu Mjini Mhanuzi, tunayo mashaka makubwa na haya maji ambayo tunatumia.

Maji haya ambayo yanatolewa kama huduma na Mamlaka ya Maji na usafiri wa Mazingira Mhanuzi (MWANHUWSSA), kila siku yanatoka yakiwa na tope, maji meusi sana.

Ukichota maji ukaweka kwenye ndoo, yanakuwa meusi, tunaomba kujua kama haya maji ni safi na Salama.

Tetesi zilizopo ni kuwa Mamlaka hii haina chujio la kuchuja maji, hivyo hali hii huwa inatokea hasa wakati huu wa kiangazi, maji yanapopungua, inaponyesha mvua yanakungana na tope kisha Mamlaka inaweka dawa na yanakuja kwetu yakiwa na tope kama unavyonionea kwenye video.

Tunalipa bili kila mwezi, lakini hii Mamlaka imeshindwa kabisa kuchuja haya maji, mpaka itusambazie maji ya tope? Kwanza ukioga yanawasha.

Maji yamejaa tope, watu tunalipa hela zetu kupata maji ya tope? Tunaomba mtusaidie wananchi wa Meatu Mhanuzi kwa haya maji meusi yenye tope.

Hapa ni Mjini tunapata maji ya tope, tena ni makao Makuu ya Wilaya, ambapo anaishi mwakilishi wa Rais na vyombo vyote vya ulinzi na usalama.

Wakati nyie viongozi mkioga maji meupe sisi huku Meatu Mhanuzi, maji yetu ni meusi yamejaa tope, alafu ni maji yanatolewa na chombo cha serikali na wanayalipisha bili.

Kinachonishangaza ni mamlaka kabisa ambayo ina Mkurugenzi na Watendaji na wanalipwa hela, lakini wanatoa huduma ya maji yenye tope na maji ni meusi sana.

Hapa chini nimeweka video mbili, angalieni maji tunayotumia wananchi wa Mhanuzi Meatu, Makao Makuu ya Wilaya.

Je, ni kweli mamlaka haina chujio?



 
Fedha zimeenda Taifa Stars ndiyo watu muhimu. Nyie huko hata mkinywa tope mna hasara gani kwa nchi?
 
Pole mdau . Nadhani watalifanyia kazi kwa kuliweka hapa jukwaani. Ila mdau vipi shule yangu bado ipo ya meatu sekondari?2016-2018.
 
Back
Top Bottom