Mamlaka ya Mapato - TRA, Nasema Nanyi

Mamlaka ya Mapato - TRA, Nasema Nanyi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
MAMLAKA YA MAPATO- TRA, NASEMA NANYI

Na, Robert Heriel

Kumekuwa na malalamiko yanayoelekezwa Mamlaka ya Mapato - TRA. Malalamiko ya wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo dhidi ya TRA yamekuwa kama sehemu ya wimbo katika taifa hili. Hii imepelekea baadhi ya wanasiasa kujipatia ujiko kwa kupata tawi la kudandia kama nyani katika kipengele hichi.

Tangu niko mdogo nikiwa nakua malalamiko haya nayasikia. Mara TRA waonevu, mara TRA hawajali wafanyabiashara, Mara TRA wanadhulumu watu basi maneno ya kila namna yanatolewa dhidi ya TRA.

Malalamiko haya hayapaswi kupuuzwa, serikali lazima itafuta namna bora ya kusaidia wananchi wake hasa Wafanyabiashara na wajasiriamali wanaolalamika.

Nafahamu moyo wa nchi upo TRA, Mamlaka ya Mapato ni kama moyo unaosukuma damu sehemu zote za mwili. Kupitia Mamlaka ya Mapato serikali inajipatia kodi zinazoendesha shughuli za kiserikali. Kama TRA ni moyo wa serikali hatuna budi kuhakikisha unadunda vizuri na kusukuma damu vyema. Tunafahamu kama Moyo unamatatizo lazima mwili uhangaike, upate shida na ulalame.

TRA ni Kama Moyo. Kuna mishipa inayoingiza damu na inayotoa damu kwenye moyo kwenda/kutoka mwilini. Mishipa hiyo hufahamika kama ATERI na VENA. Ateri ni mishipa inayopeleka damu kutoka moyoni kwenda mwilini. Vena ni mishipa inayopeleka damu kuingia moyoni kutoka mwilini. Ateri huwa ni mishipa myembamba inaotoa damu kutoka moyoni kwenda mwilini, ni myembamba ili kufanya damu ipite kwa kasi ikielekea mwilini. Wakati Vena inakuwa na mishipa mipana hasa karibu na moyo ilikupunguza kasi ya damu inayoingia moyoni. Somo la moyo nimechomekea tuu,

TRA Lazima ihakikishe kuwa viingizi vya mapato viwe ni vipana kama mishipa ya Vena iliyokaribu na moyo, Kusudi kuiingiza mapato polepole ndani ya TRA. Kufanya viingizi vya mapato kuwa vyembamba ni kupoteza mapato, ni kutaka kuupasua moyo au mishipa ya damu na kufanya damu ivuje na kusababisha mtu kufarikia(Mamlaka kupata hitilafu)

Moyo/TRA haiwezi kupokea damu inayokuja kwa kasi kwenye mishipa myembamba. Moyo unaweza kupasuka au kusimama kwa kuzidiwa uwezo, au mishipa kupasuka.

TRA ndio moyo
Walipa Kodi ndio Oragan za Mwili na viungo vyake
Vyanzo vya Mapato ndio Mishipa ya damu.

TRA Lazima itafute namna bora ya kukusanya mapato bila kuumiza watu. TRA lazima itafute namna bora ya kuwafanya wananchi wote wenye umri wa kulipa kodi walipe bila ya wao kuhisi kuonewa.

MBINU ZA KUKUSANYA KODI BILA KUBUGHUZI RAIA

1. KANUNI YA FUNGU LA KUMI (10% PERCENT PRINCIPLE)

Kanuni hii imegawanyika sehemu mbili
1.1. 10% ya makato ya Pango
1.2. 10% ya makato ya faida

1.1. 10% YA MAKATO YA PANGO

Hapa zipo makato yawepo ya aina mbili;
1.1.1. 10% makato ya mpangishaji
1.1.2. 10% Makato ya mpangaji

TRA waunde utaratibu wa kukata 10% ya Hela ya pango ambayo mfanyabiashara anaitoa kulipia Fremu ya Biashara.

Mfano 01. Pango la bei ya 50,000/= kwa mwezi
10% ya 50,000/= ni 5,000/=
Hivyo mfanyabiashara atatoa 55,000/=, ambapo 5000/= itaenda serikalini kwa mwezi.
Kisha Mpangishaji, yaani mwenye Fremu naye atalipia 5000/= itaenda serikalini na kufanya jumla ya 10,000/= kwa Fremu moja kwenda serikalini yenye pango la bei ya 50,000/= kwa mwezi.
Mpangishaji yaani mwenye Fremu atabaki na 45,000/=

Hii ni kusema, kama Fremu za biashara ambazo zinapangishwa kwa 50,000/= kwa mwezi zipo 10,000/= Tanzania nzima. Hesabu itakuwa hivi;

Mpangishaji tumpe herufi = MP
Mfanyabiashara(mpangaji) = MF

MF= 5,000/=
MP= 5,000/=
Kwa pango la 50,000/= Kwa mwezi

MP + MF = Mapato ya TRA (M-TRA)
5,000 + 5,000= 10,000/= Kwa Fremu moja.

Assume Fremu zipo 10,000 Tanzania nzima za pango la 50,000/=

Hesabu itakuwa hivi;

Jumla ya Fremu zote Tz x M-TRA ya Fremu moja kwa mwezi

10,000 x 10,000 = 100,000,000/= Kwa mwezi.

100,000,000 x 12 = 1, 200,000,000/= kwa mwaka

Bado kuna fremu za elfu 40, 30, 25 za biashara kwa mwezi

Kwenye 40,000/= kodi iwe 44,000/=
8000 iende serikalini
36000 achukue MP
Assume wenye Fremu za 44,000 wapo 5000
8000 x 5000 = 40,000,000/= kwa mwezi
40,000,000 x 12 = 480, 000,000/= kwa mwaka

MATUMIZI YA 10% YA PANGO KATI MP NA MF

1. Hiyo ndio itakuwa pesa ya leseni kwa kila mfanyabiashara.
Kazi ya serikali ni kuwabana wenye Fremu za biashara, kazi hii ifanywe na maafisa wa TRA ngazi ya Kata, au serikali ya mtaa.

Mfanyabiashara yeyote akichukua Fremu basi automatiki atakuwa ameshalipa kodi ya leseni bila kusumbuana na serikali.
Kazi ya serikali ni kuzungukia watu wote wenye Fremu na kuwapa Leseni baada ya kuonyesha mkataba wa pango.

FAIDA YA KANUNI HII
> Serikali itajipatia mapato mengi bila usumbufu kodi itakuwa inalipwa pamoja na pesa ya kodi ya Fremu.
>. Itapunguza kufungiwa kwa wafanyabiashara kisa hawana leseni.
>. Itaondoa mgogoro wa moja kwa moja baina ya wafanyabiashara na maafisa wa TRA au manispaa bali mgogoro utakuwa baina ya TRA na wamiliki wa Fremu.
> Itapunguza kusumbuka kwa maafisa wa TRA na Manispaa ambao wakipita hukuta Fremu zimefungwa ilhali zinafanya kazi, Hii ni kutokana na tabia ya walipa kodi kupeana taarifa kuwa TRA wanakuja, hivyo wanafunga Fremu chapu. Lakini kanuni hii automatiki mtu atakuwa kakata leseni bila ya kupenda

HASARA YA KANUNI HII
> Itaibua mgogoro baina ya TRA au manispaa na Wamiliki wa Fremu katika kipindi cha mwanzo lakini baadaye itazoeleka.

UTEKELEZAJI
> Iundwe sheria itakayomfanya mfanyabiashara na mmiliki wa Fremu kutoa 10% ya pesa ya pango kila mwezi kila mmoja.
> Maafisa TRA kata waongezwe ambao watadili na wamiliki wa FREMU NA sio Wafanyabiashara.
> Maafisa TRA kata wakifika kwenye Fremu wadai mkataba wa pango. Kama Mfanyabiashara amelipa kodi ya pango automatiki mmiliki anapaswa awe amaeshalipia 10%(yake na mfanyabiashara) Serikalini.

1.2. 10% Makato ya Faida
Hapa ndio utata ulipo hasa kwa wasiowaaminifu.
Mbinu ya kukadiria kodi sio nzuri kwa hapa tulipofikia.
Serikali naipongeza kwa kutoa mashine za kukatia Risiti. Ningeshauri mashine zile zitolewe bure, lakini namna zinavyofanya shughuli zake ndio ziwekewe gharama kama luku ya umeme.(Hili kidogo linahitaji maelezo marefu, ngoja likae pending)

Muhimu kila raia afundishwe kudai risiti, pia wafanyabiashara nao watoe risiti.

Iundwe sheria lkali ya kutochukua na kutoa risiti ni kosa kisheria.

Kwa Wateja wa nchi za nje, kanuni hii isitumike bali inaweza kuongezwa hata 15% au 20% kabisa

Kwa habari ya Wamachinga au watu wote wasio na Fremu

Wajumbe wa mtaa na wamiliki wa vyumba vya kupanga ni muhimu.

Mmiliki wa nyumba ya kupanga ataongeza 10% ya kodi kwa mpangaji ambaye ni machinga au asiye na Fremu ya biashara.

Mfano 02
Chumba cha 30,000/=
Mpangaji atatoa 33,000/= elfu tatu itaenda serikalini
mwenye chumba atatoa 3,000 itaenda serikalini kwani hiyo kwake ni biashara.
Hivyo mwenye chumba atapata 27,000/= kwa mwezi.

Pesa hiyo itakusanywa na wajumbe na kupelekwa serikali ya mtaa kwa maafisa TRA au manispaa. Yaani 10% ya kodi ya chumba ya Machinga asiye na Fremu ya Biashara.

FAIDA

> Wamachinga wengi automatiki watakuwa wanalipa kodi kwenye serikali na hawataweza kukimbia ilimradi wawe wamepanga
> Mapato ya serikali yataongezeka maradufu kwani watu wengi watakuwa wanalipa kodi
> Wajumbe watakuwa wamepata ajira kwani nao kuna posho watakuwa wanagewa
>Kila mtu mtaani itakuwa rahisi kufahamu anajishughulisha na nini.
> Mgogoro wa Machinga na serikali utapungua automatiki

HASARA
> Mgogoro kati ya serikali na wenye nyumba utaibuka kipindi cha awali.
> Machinga wenye nyumba zao itakuwa ngumu kuwafuatilia
> Wapo baadhi ya machinga wanaishi zaidi ya mmoja ndani ya chumba kimoja, hivyo itakuwa mgogoro katika ya mwenye nyumba na wapangaji.

UTEKELEZAJI
> Wajumbe wapewe mamlaka ya kujua kazi za watu
> Wenyenyumba wachukue 10% ya kodi kwa kila machinga atakayekaa kwenye chumba chake, kama wapo wawili chumba kimoja basi wote watalipa 10% ya pesa ya pango wanalolipia chumba hicho. Yaani kama ni 2000, basi kila mmoja atalipa 2000 kwa mwezi.

> Pesa hiyo itolewe baada ya mpangaji kuchukua chumba. Ni wajibu wa mwenye nyumba kuuliza ni watu wangapi watakaa kwenye chumba hicho na shughuli zao. Kama ni watu watatu ambao ni machinga basi watalipia siku hiyo watakayolipia pango.

TRA isiwafunge Fremu wafanyabiashara kwani kwa kufanya hivyo inakosa mapato yo yenyewe na inawapa Wafanyabiashara wakati mgumu.

Embu fikiria, mfanyabiashara anafremu na pia amepangisha chumba.
Fremu 50,000/=
Chumba 40,000/=
Jumla 90,000/=
Kwa miezi mitatu= 270,000/=

Unapomfungia mtu Fremu unampa wakati mgumu na unatengeneza mazingira ya kumfilisi. Unafunga Fremu kisha, unampa faini 50,000/= muda huo anadaiwa kodi ya miezi mitatu ya chumba anachoishi na mke wake, muda huo huo kodi ya Fremu inaishi mwezi huu. Kama sio kumfanya afilisike ni nini.

Mambo haya nimeyaona kwa macho yangu wala sijahadithiwa, na ndio maana nikaona kwa upeo mdogo nilionao nishauri jambo hili, ili kupunguza migogoro isiyo na lazima.

Wazo hili linaweza kuongezewa nyama na wachumi, kwa maana mimi sio mchumi.

Nitaendelea siku nyingine na Kanuni ya pili na tatu ya namna TRA wanapaswa kukusanya mapato bila Bughuza.

Leo nitaishia hapa, naona andiko linakuwa refu na Ndugu zangu hawapendi maandiko marefu

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Kesho njoo ofisini TRA makao makuu, mawazo yako yanaweza kuisaidia Mamlaka
 
Njia rahisi ya utekelezaji wa hii ni 2 nionavyo mimi.
1. Kuwe na mkataba standard ( form ya TRA) wa upangishaji ambao una kipengele A...taarifa za mwenye nyumba na TIN yake.
Kipengele B iwe taarifa za mpangaji na TIN yake
Kipengele C. Bei za upangaji na makato yake
Kipengele D iwe kwa mtendaji wa mtaa / kijiji husika.
Kipengele E kiwe ni kwa TRA ya mahali husika.
Tuachane na mikataba ya sasa ya upangaji isiyozingatia sheria za upangaji wala za kodi.

Pili. Tuimarishe ofisi za serikali za mitaa kwa kuajiri wenye sifa ( sasa wasomi ni wengi) kwa kuweka sifa stahiki za anayetakiwa kuwa mtendaji wa mtaa. Sasa naona yeyote tu anaajiriwa.
Watu waliosoma utawala, sheria, na fedha.

Wapewe vitendea kazi
 
Back
Top Bottom