SoC04 Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)

Tanzania Tuitakayo competition threads

Dahaye Jr

New Member
Joined
May 2, 2019
Posts
2
Reaction score
2
Mimi nashauri MAMLAKA YA VITAMBULISHO (NIDA) kuangaliwa upya kwa maslahi mapana ya taifa letu kwa sababu zifuatazo;

1. Endapo kuna makosa yamefanyika wakati wa usajili wa mwananchi hasa makosa ya alama za vidole mfumo wa usajili Una reject application halafu inaonekama hakuna namna ya kurekebisha tatizo kama hilo katika mfumo wa usajili hivyo kuna watanzania wengi sana ambao wamekwama kupata namba ya NIDA au kitambulisho cha TAIFA.

2. Idara ya VITAMBULISHO VYA TAIFA inatumia muda mrefu sana sana kutoa namba za NIDA baada ya usajili kiasi kwamba sasa inaonekana kama si jambo la muhimu sana wakati huku mtaani kuna watu wengi wanakwama kufanikisha mambo yao mengi kwa kukosa namba ya NIDA.

3. Nashauri au napendekeza NIDA iangalie upya utaratibu wake maana kama inawezekana waanze utaratibu wa kuandikishwa mapema ikiwezekana mtoto anapoandikishwa darasa la Kwanza kwa vile lazima shule kwenye usajili itahitaji CHETI CHA KUZALIWA na kwa vile vile kiambatanisho muhimu sana cha kuandikishwa NIDA pia ni cheti hicho hicho cha kuzaliwa basi mtoto huyo baada ya kuandikishwa shule iwe sharti pia kuandikishwa kwenye vitambulisho vya taifa awe na kitambulisho chake akifikisha miaka 18 afanyiwe uhakiki tu.

Kwa kufanya utaratibu kama huo serikali itakuwa imepunguza msongamano wa kazi za usajili katika idara yake na pia hiyo itapunguza mianya ya watu kufanya udanganyifu katika taarifa zao maana kila mtu atakuwa anasomeka kwenye mfumo toka akiwa na umri wa miaka 6, atakuwa hawezi kudanganya kuanzia pale anasoma shule ya msingi, sekondari, sekondari ya juu,vyuo vya kati hadi chuo kikuu na bodi ya mikopo itapata urahisi wa kuhakiki taarifa za mwombaji maana atakuwa anasomeka kwenye mfumo wa NIDA kweye taarifa zake, za wazazi /walezi mpaka taarifa za shule alizopitia, nashukuru kupata nafasi ya kutoa ushauri wangu kwa mamlaka ya vitambulisho vya taifa maana mimi pia ni mhanga wa kutopata namba za NIDA toka nimejiandikisha mwaka 2017 miaka 7 imepita sasa sina namba za NIDA halafu tatizo langu la finger print naambiwa tusubiri mpaka muongozo mpya utakapotoka sasa haya sio mateso jamani?
 
Upvote 2
Nashauri au napendekeza NIDA iangalie upya utaratibu wake maana kama inawezekana waanze utaratibu wa kuandikishwa mapema ikiwezekana mtoto anapoandikishwa darasa la Kwanza kwa vile lazima shule kwenye usajili itahitaji CHETI CHA KUZALIWA na kwa vile vile kiambatanisho muhimu sana cha kuandikishwa NIDA pia ni cheti hicho hicho cha kuzaliwa basi mtoto huyo baada ya kuandikishwa shule iwe sharti pia kuandikishwa kwenye vitambulisho vya taifa awe na kitambulisho chake akifikisha miaka 18 afanyiwe uhakiki tu.
Hili ni jema sana, hatuhitaji mbambamba nyingi.
ushauri wangu kwa mamlaka ya vitambulisho vya taifa maana mimi pia ni mhanga wa kutopata namba za NIDA toka nimejiandikisha mwaka 2017 miaka 7 imepita sasa sina namba za NIDA halafu tatizo langu la finger print naambiwa tusubiri mpaka muongozo mpya utakapotoka sasa haya sio mateso jamani?
Daah pole sana, na asante kwa maoni.
 
Yani hata mm mwenyewe ni muhanga wa hilo jambo ni muda sasa mambo yangu hayaendi sijajua mamlaka inampango gani na watu kama sisi
 
Mimi nashauri MAMLAKA YA VITAMBULISHO (NIDA) kuangaliwa upya kwa maslahi mapana ya taifa letu kwa sababu zifuatazo;

1. Endapo kuna makosa yamefanyika wakati wa usajili wa mwananchi hasa makosa ya alama za vidole mfumo wa usajili Una reject application halafu inaonekama hakuna namna ya kurekebisha tatizo kama hilo katika mfumo wa usajili hivyo kuna watanzania wengi sana ambao wamekwama kupata namba ya NIDA au kitambulisho cha TAIFA.

2. Idara ya VITAMBULISHO VYA TAIFA inatumia muda mrefu sana sana kutoa namba za NIDA baada ya usajili kiasi kwamba sasa inaonekana kama si jambo la muhimu sana wakati huku mtaani kuna watu wengi wanakwama kufanikisha mambo yao mengi kwa kukosa namba ya NIDA.

3. Nashauri au napendekeza NIDA iangalie upya utaratibu wake maana kama inawezekana waanze utaratibu wa kuandikishwa mapema ikiwezekana mtoto anapoandikishwa darasa la Kwanza kwa vile lazima shule kwenye usajili itahitaji CHETI CHA KUZALIWA na kwa vile vile kiambatanisho muhimu sana cha kuandikishwa NIDA pia ni cheti hicho hicho cha kuzaliwa basi mtoto huyo baada ya kuandikishwa shule iwe sharti pia kuandikishwa kwenye vitambulisho vya taifa awe na kitambulisho chake akifikisha miaka 18 afanyiwe uhakiki tu.

Kwa kufanya utaratibu kama huo serikali itakuwa imepunguza msongamano wa kazi za usajili katika idara yake na pia hiyo itapunguza mianya ya watu kufanya udanganyifu katika taarifa zao maana kila mtu atakuwa anasomeka kwenye mfumo toka akiwa na umri wa miaka 6, atakuwa hawezi kudanganya kuanzia pale anasoma shule ya msingi, sekondari, sekondari ya juu,vyuo vya kati hadi chuo kikuu na bodi ya mikopo itapata urahisi wa kuhakiki taarifa za mwombaji maana atakuwa anasomeka kwenye mfumo wa NIDA kweye taarifa zake, za wazazi /walezi mpaka taarifa za shule alizopitia, nashukuru kupata nafasi ya kutoa ushauri wangu kwa mamlaka ya vitambulisho vya taifa maana mimi pia ni mhanga wa kutopata namba za NIDA toka nimejiandikisha mwaka 2017 miaka 7 imepita sasa sina namba za NIDA halafu tatizo langu la finger print naambiwa tusubiri mpaka muongozo mpya utakapotoka sasa haya sio mateso jamani?
🙌🙌
 
Mkuu naomba utoe mrejesho hapa kama ulifanikiwa kujisajili upya cz mwenyew nna changamoto kama ya kwako
 
Shida ni sisi,nimetafuta mada za wanavyuoni kuona wanapendekeza nini kwenye research mbali mbali za vyuo hakuna nilichoona.
sasa kama wasomi hatuna mapendekezo ya kitafiti wao watajuaje?
 
Mwenzangu alifata hatua karibu zote,lkn mwisho akakwamba eti kwakukosa cheti cha darasa la saba,ambayo ndo elimu yake,jamani hii ni haki kweli, kwanini wasingetumia cheti chake kuzaliwa alichokua nacho,si kilikuwa kinatosha!!?
 
Back
Top Bottom