Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Tanzania Airports Authority
Katika mitandao ya kijamii kunasambaa taarifa katika picha mjongeo kuhusu kukosekana kwa huduma yam aji katika maliwato iliyochapishwa tarehe 24 Julai, 2024 na abiria Dudubaya na Bushoke. Abiria hao walikuwa wanasafiri na ndege ya shirika la ndege ya Kenya Airways kati ya Saa 7 na Saa 9:50 usiku kupitia jengo la 3 la abiria katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Mamlaka inapenda kuufahamisha umma kuwa, tarehe 24 Julai, 2024 kulitokea “Leakage” kwenye pump moja ya maji safi katika kiwanja cha ndege cha JNIA na hivyo kutulazimu kubadili mfumo wa utoaji maji safi kwenda kwenye mfumo wa ziada wa maji safi, zoezi ambalo huchukua dakika tano kukamilika. Wakati wa utekelezaji wa zoezi hili maji yalikuwa na pressure ndogo, na baada ya zoezi kukamilika yalirudi katika pressure inayofaa.
Pia soma: Julius Kambarage Nyerere International Aiport vyooni hakuna Maji Aibu sana nchi yetu
Marekebisho na matengezo ya mifumo, mitambo na huduma kama maji, umeme, viyoyozi ni, katika jengo la 3 la abiria hurekebishwa mara moja na wataalamu wetu ambao wapo kazini masaa 24 ili kuhakikisha huduma zinatolewa katika viwango vinavyotakiwa.
Picha za marejeo zinaonyesha kuwa, abiria huyo hakupata maji hata kwa pressure ndogo kwa sababu hakufungua bomba kwa usahihi. Bomba hilo hubonyezwa kwenda chini ili kuweza kutoa maji na sio kuzungushwa. Aidha, chupa yam aji inayoonekana katika picha mjongea iliachwa na abiria mwingine na haikuwekwa na mamlaka kama mbadala wa kutopatikana kwa maji kwani maji katika jengo hili huatikana muda wote na kwamba kiwanja cha ndege cha JNIA kina maji ya akiba yenye ujazo wa lita milioni 4.7 wakati matumizi yam aji ya kiwanja kwa siku ni lita takriban laki sita.
Mamlaka inapenda kuufahamisha umma kuwa, toka kufunguliwa kwake mwaka 2019 hadi sasa, jengo la 3 la abiria halijawahi kupata changamoto yam aji na limekuwa likiendeshwa kwa kuzingatia miongozo ya kitaifa na kimataifa na lipo katika hali nadhifu wakati wote. Sep hivyo basi, taarifa ya kuwa maji katika maliwato ya jengo la 3 la abiria katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere hayatoki ni uzushi, zina lengo la kuchafua taswira ya kiwanja na kupotosha umma na hivyo zipuuzwe.