Mamlaka za Afya nchini tulindeni Watanzania

Mamlaka za Afya nchini tulindeni Watanzania

Chendembe

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
444
Reaction score
488
Afya ndio msingi wa maisha yetu. Bila kuwa na afya hakuna Jambo linaweza kuwa sawa kwa mtu binafsi, familia na hata Taifa.

Kwa hali inayoendelea sasa nchini ya watu kupatwa na mafua na homa kali, nasukumwa kuziomba Mamlaka zetu kuwa Malini na kila kinachoingia nchini hususani vifaa tiba. Mamlaka msipatwe upofu wa kubaini njama mbalimbali zinazoweza kuangamiza nchi kwa sababu ya matakwa ya watu Fulani ambao hawanania njema.

Pamoja na kujumuika na juhudi za kimataifa katika maswala ya afya, tutambuwe kuwa, kunatofauti ya mazingira Kati ya nchi na nchi.

Tafadhali, Mamlaka tuchukuwe muda wa kutosha kukubaliana na mambo ya kiafya. Wenzentu waliokimbilia hatua za Afya awali, wamezitekeleza kwa muda mrefu na nadhani hawajafanikiwa Hadi sasa na tunaendelea nao katika vita hizohizo.

Ukweli utabaki ukweli, maji yataitwa maji tuu, chanjo za maradhi mbalimbali zilikuwepo, zipo na zitakuwepo. Tumezitumia, tunazitumia na tutazitumia. Lakini tahadhali muhimu.

Mwenyezimungu anatuimiza kuomba afya hapa duniani na kesho baada ya kuiacha dunia. Hatunabudi kuomba kwa pamoja nusura ya hili gonjwa.
 
Viongozi gani hao unawaomba?

Wenzio wanatamani Corona ichue Watanzania wengi waendelee kupata hela za Corona.
Wenzio wanapiga pesa ndefu za semina na makongamano ya Corona,halafu utegemee wakulinde?

RIP Jabali la Afrika.
 
Back
Top Bottom