Mamlaka za Afya nchini tulindeni Watanzania

Mamlaka za Afya nchini tulindeni Watanzania

Chendembe

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
444
Reaction score
488
Afya ndio msingi wa maisha yetu. Bila kuwa na afya hakuna Jambo linaweza kuwa sawa kwa mtu binafsi, familia na hata Taifa.

Kwa hali inayoendelea sasa nchini ya watu kupatwa na mafua na homa kali, nasukumwa kuziomba Mamlaka zetu kuwa Malini na kila kinachoingia nchini hususani vifaa tiba. Mamlaka msipatwe upofu wa kubaini njama mbalimbali zinazoweza kuangamiza nchi kwa sababu ya matakwa ya watu Fulani ambao hawanania njema.

Pamoja na kujumuika na juhudi za kimataifa katika maswala ya afya, tutambuwe kuwa, kunatofauti ya mazingira Kati ya nchi na nchi.

Tafadhali, Mamlaka tuchukuwe muda wa kutosha kukubaliana na mambo ya kiafya. Wenzentu waliokimbilia hatua za Afya awali, wamezitekeleza kwa muda mrefu na nadhani hawajafanikiwa Hadi sasa na tunaendelea nao katika vita hizohizo.

Ukweli utabaki ukweli, maji yataitwa maji tuu, chanjo za maradhi mbalimbali zilikuwepo, zipo na zitakuwepo. Tumezitumia, tunazitumia na tutazitumia. Lakini tahadhali muhimu.

Mwenyezimungu anatuimiza kuomba afya hapa duniani na kesho baada ya kuiacha dunia. Hatunabudi kuomba kwa pamoja nusura ya hili gonjwa.
 
Ten hours ago lakini no even a single comment!

Dah! Kweli kuna nyuzi na watu wao na kuna watu na nyuzi zao
 
Kila utapopiga simu habari ni homa kali ya KICHWA NA MAFUA halafu mwisho au kupona kwa viwili hivyo ndo kunakuja vikolombwezo vinginevyo ambapo hutofautiana kwa mtu na mtu

Kwamfano mimi mwenyewe ninayeandika hapa goma limenizukia ghafla tu nashangaa kichwa na mafua kwambali mara dakika kadhaa mafua hasa na kichwa haswa baada ya kula dawa3 na coldril ya chenga ikawa ndo afadhali ila dude limebaki kwenye kukohoa sana (hacking cough), kichefuchefu baadhi ya nyakati lakini bila kutapika, mara kizunguzungu kwa mbali, mara uchovu na maumivu ya viungo, kukosa hamu/ladha ya chakula mara...

Wenzangu wengine wanasema wanahisi miguu inauma na kulegea, kusikia nyela masikioni, mara baridi wakati jua ni kalisaa 8 mchana, mara... yaani ilimradi tu

Sasa yote hayo cha ajabu sisikii viongozi wa afya wakitoa neno, sisikii hatua yoyote ikichukuliwa (tofauti na zile za uviko- maana hii hatujathibitishiwa kama ni uviko bado) wala sisikii kwa watu juu ya tafiti au hatua za kufanya utafiti wowote juu ya jambo hili geni

WHY?
 
Back
Top Bottom