Ngatele
JF-Expert Member
- Jan 25, 2011
- 808
- 704
Hapo nyuma nilikuwa na mazoea ya kwenda saloon fulani ambayo nilikuwa nimeizoea kama ilivyo kwa watu wengi. Mara zote nilipokuwa nanyolewa mashine ya kunyolea ilikuwa ikitolewa kwenye sterilizer ambayo huwa wakati wote kitaa cha ON (Chekundu) kinaonesha kuwa ipo ON na kwa hiyo ina maanisha inafanya kazi ya ku sterilize mashine inapokuwa ndani.
Hivi karibuni nilipokwenda saloon hiyo nilipata wasiwasi na hiyo sterilizer na hivyo kuamuru nitazame ndani yake kama ile taa yake ya joto inafanya kazi, alas! maajabu nilikuta ni gagali, vinyozi wanadanganya wateja kwani kitaa cha ON kinaonesha inafanya kazi lakini ile tube ya ndani kuleta joto haifanyi kazi. Niliudhika sana na kuwashangaa kwa nini wanadanganya wateja na kuhamisha mashine kutoka mteja mmoja kwenda mwingine pasipo usafi unaohitajika.
Suala hili nililikuta pia saloon nyingine ambayo inapendeza sana. Inawezekana uhuni huu unafanyika katika saloon nyingi huku watu wakilipa pesa nyingi za kunyoa nywele na ndevu huku wateja wengine wakiwa na mapele ambayo yanaweza kuleta maambukizi.
Nawaomba watu wafanye uchunguzi kwenye saloon walizozoea na baadaye walete mrejesho hapa kama uhuni huo unafanyika pia na ikibainika Mamlaka husika za Afya zijulishwe ili zifanye uchunguzi na kuchukua hatua.