Naomba Jamii Forums msaidie kupaza sauti ya huyu mzee apate msaada, tumemkuta anaishi chini ya hili jiwe, anadai yupo hapo tangu Mwaka 2011 baada ya CDA Dodoma kuvunja nyumba yake aliyojengewa kwa msaada na Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma.
Eneo hili ni ITEGA, Mzee mwenyewe anadai ofisi ya Mwenyekiti wa Mtaa haijamsaidia kabisa.
Nyumba ilivunjwa kupisha bomba la maji na hakupewa mbadala wa maisha yake na hana ndugu kabisa
Busara ilikuwa kwa hao waliomjengea ya awali wamjengee tena au wampe hifadhi maana ndiyo wanafahamu situation yake nje ndani hata kabla ya hili la bomba.
Au anahitaji msaada wa kisheria apate fidia ya kubomolewa nyumba yake?
Kwa huu mfumo wetu wa utoaji haki,anawezajikuta anasota miaka 10 mingine chini ya jiwe huku jamaa wakikata rufaa tu hata kama atashinda kesi.
Kwa muda wote huo kashindwa kuboresha Hilo eneo hata kwa miti tu na tope na jiwe likatumika kama bati..?? Miaka 13 anakula nini na anaishi vip anafanya kazi gani
Mfano. Angeamua kwenda Kijiji Fulani akaomba shamba akawa analima (wengi wanafanya hili) angekua na hali gani kwa sasa....