Mamlaka za udhibiti ni kikwazo kwa uwekezaji

GwaB

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2014
Posts
4,291
Reaction score
5,786
Mapato ya nchi hutegemea ukusanyaji wa kodi kutoka kwa wingi wa watu binafsi au kutoka kwenye faida ya mashirika na makampuni yaliyojiandikisha kwa lengo la kufanya biashara. Kwa miaka mingi sana Tanzania imekuwa ikitegemea kodi zinazokusanywa kutoka kwa wafanyakazi walioko kwenye mfumo ulio rasmi na baadhi ya wafanyabiashara wachache binafsi. Ni hivi karibuni tu kumekuwa na mwelekeo wa kupanua wigo wa walipa kodi kwa kuihusisha sekta isiyo rasmi ili ichangie ipasavyo katika mapato ya nchi.

Pamoja na nia njema ya serikali kuongeza idadi ya walipa kodi kwa kuruhusu watu kufanya biashara ni vyema serikali ikapitia upya huu mfumo wa utoaji leseni na vibali hasa kwenye biashara za kitaaluma. Kwa hali ya kawaida biashara zisizohitaji vibali hulipa ada kwa ajili ya leseni ya kufanya biashara ambayo iko kwenye TSH 70,000 kwa mwaka. Kwa biashara zinazohitaji vibali vya kitaaluma, pamoja na kulipia TSH 70,000 za leseni bado mfanyabiashara anatakiwa kulipia TSH 50,000 kwa ajili ya kibali cha kufanya biashara za kitaaluma.

Kwa mfano nilioutoa hapo juu, inaonyesha wazi kuwa mfanyabiashara anayewekeza kwenye biashara zinazohitaji vibali vya kitaaluma gharama zake zinakua juu zaidi na kupunguza kiwango cha uwekezaji kwenye mradi husika. Tozo na ada ya vibali ni kikwazo katika biashara napendekeza ufanyike utaratibu wa mamlaka za udhibiti kuchukua mgao kwenye leseni kuu za biashara.

Mamlaka za udhibiti huundwa kwa sheria zinazotungwa kwenye bunge letu, pamoja na uundwaji wake huo ni muhimu kuangalia kama mwelekeo wa sheria za usimamizi ziwe na lengo la kuwezesha biashara kushamiri na baadaye kulipa kodi na sio kukwamisha biashara zinazoanzishwa kwa gharama kubwa.
 
Bora wewe hiyo Tsh 70,000/=, ushauri wa kitaalam ada zake ni kati ya Tsh 150,000/= hadi Tsh 300,000/=. Taaluma zingine registration unalipia Tsh 345,000/= na retention fee unalipia Tsh 165,000/= kila mwaka. Then hapo bado kuna kulipia Income Tax TRA, Withholding tax, usafi/uzoaji taka, kulipia regulatory authorities mathalani TFDA, EWURA, NEMC nk. Ukiongezea mshahara wa staff wako, Bima yake ya afya, Pension yake nk aaahhhh lazima ujue kwa nini wafanyakazi wananenepa wakati boss anakonda
 
Mkuu nakubaliana na wewe 100%, hizi mamlaka za udhibiti zimejikita kwenye kuvuna mahali wasipopanda... Labda lengo likiwa ni udhibiti ili biashara za kitaaluma zisifanyike nitaweza kuelewa. Mamlaka zote zipo kisheria na kwa maana hiyo zinapaswa kupata ruzuku kutoka mfuko wa Serikali ili kujiendesha na siyo wao kujipangia kukusanya tozo kubwa kutoka kwa mfanyabiashara ambaye bado anapaswa kulipia kodi biashara yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…