Ze burner
JF-Expert Member
- Jan 5, 2011
- 514
- 83
Leo tarehe 20.12.2020 muda huu naandika nikiwa katika chombo cha Zan Fast Ferry (Zanzibar 2) tulitaraji kuondoka majira ya saa 10.15 jioni kwa mujibu wa ticket zetu ila katika hali isiyotarajiwa tumeondoka saa 10.55 jioni baada ya kupigwa na joto kali hatqri huku watoto wakipiga kelele kwa maumivu ya joto hilo.
Cha kushangaza saa, kabla ya chombo hicho kuondoka alikuja mmoja kati ya watumishi wa kampuni hiyo akiwa ndani ya uniform ya tshirt na kutangaza yafuatayo "naomba niwaeleza kwamba madust ya taka yapo mbele hiyo ni vema kuacha boti ikiwa hali ya usafi" Mpaka hapo nilimuona jamaa ana akili kweli hadi alipokuja na tangazo la pili "mnajui boti ya Kilimanjaro imetangulia kuondoka ila siyo tatizo, japo tuchelewa kidogo ndani ya dakika 15 tutakua tumeipita" hapa kwa kweli kanipoteza.
Badala ya kuomba msamaha kwa kutuchelewesha kwa takriban dakika 40 anakuja kusema "japokua tumechelewa kidog" halafu angalau angekua na lengo la kuomba radhi kama ilivyo kwa waungwana anakuja anasema " hakuna shida Kilimanjaro tutaipita ndani dakika 15" abiria wote tuliomsikia tukaanza minongono kama kwamba hakuna aliyemwelewa kabisa.
Kwa kitendo cha kuchelewa sina tatizo nacho yaweza kuwa xilikuwepo sababu za msingi japo wao hawakuzisema. Tatizo ni zile kauli za kushindana wakati hatukua ktk mashindano. Leo tumefika salama ila naamini iko siku Mungu aepushie mbali tutakuja alaumiana km vile hakuna aliyekua akijua ama akiona kinachoendelea.
Nqshauri, km ilivyo kwa mamlaka ya Latra kuweka time table ya kutoka na kuingia mabasi kwenye vituo mbali mbali, ni Vyema pia mamlaka husika ziweke ratiba ya kuondoka na kufika kuliko kutegemea uwexo wa chombo husika kuamua muda wa kufika.