Kuna hiki kinachoitwa ungamo. Kwamba mtuhumiwa wa wizi, ugaidi, mauaji nk; kwamba kwa hiari yake aliungama. Kutokea hapo mtu au watu wakahukumiwa kunyongwa au hata kufungwa.
Kesi hii:
Maelezo kukiri kosa yalivyowaunganisha washtakiwa-11
Ni mwendelezo wa maungamo uchwara kama hayo kupewa umuhimu.
Hivi ni kwa kumdanganya nani vile?
Tuliwasikia akina Adamoo walivyolazimishwa kuweka sahihi zao kwenye yaliyoitwa maungamo. Bila shaka huku ndiko walikopotelea kina Lijenje
Kwanini haya maungamo viini macho yanaendekezwa tu na hata kuwa sasa ndiyo haswa ulio uthipitisho wa tuhuma zenyewe?
Kulikoni kutokutumika ushahidi wenye kuaminika kama ule wa ma CCTV, mienendo ya simu yenye kutumia teknolojia nk, zenye kueleweka hata kwao mabeberu? Kwanini ni nia ya serikali kuona kuwa haki za watu zinapotea tu pasipo na kujali?
Kwani ufwedhuli maana yake nini?
Kulikuwa na maslahi gani kwenye kuwabambikizia akina Adamoo maelezo ya uongo Ili kupata kuwatia hatiani kiharamu? Kuna maslahi gani kwenye kuwabambikizia watuhumiwa wowote maungamo yasiyokuwa ya kweli?
Tunahitaji nchi ambapo sekta zote za utawala zitakuwa ni wezeshi. Tunahitaji haki. Hatuhitaji sekta kandamizi.
Mifano iko mingi. Fikiria pia Polisi, TRA, LATRA, EWURA, NIDA, TANROADS, Uhamiaji, nk nk.
Ni wapi kuna nafuu?