BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Mfano huku mitaa ya kwetu huku Dodoma kumekuwa na ongezeko la mbwa wanaozunguka wakionekana kutokuwa na wamiliki kwa baadhi ya mitaa ikiwemo Mtaa wa Relini.
Ni mbwa ambao wamekuwa na tabia ya kukaa kwenye njia wanazopita mitaani muda mwingi, na wakati mwingine wamekuwa na tabia ya kukimbiza Watu wanaopita kwenye njia hizo.
Wiki iliyopita majira ya saa moja asubuhi, nikiwa ndani nilisikia sauti mtoto akilia sana, baada ya kutoka nje na kuzunguka nje ya nyumba nilimkuta mtoto wa jirani ndiye anayelia baada ya kukimbizwa na mbwa wawili, hali iliyosababisha kudondoka na kuumia mgongo, huku watu wakiwakimbiza mbwa wale.
Si huyu tu, mmoja wa madereva bodaboda anasema mbwa hao wamekuwa na tabia hiyo kwa Watu wanaopita, naye ni miongoni mwa waliopitia adha hiyo wakati fulani. Kuna kipindi hapa waliwapiga risasi mbwa, ila kuna mbwa jike alibaki ndiye aliwazaa hawa mbwa.
Ni zaidi ya mbwa Watano hupenda kukaa njia majira ya asubuhi na jioni. Nitoe wito kwa Mamlaka mbalimbali zinazohusika zichukue hatua mapema kabla ya madhara hayajatokea kwa Watu.
Ni jambo la nadra kuona katika Nchi za wenzetu zilizoendelea kuona Mbwa wakiwa mitaani hawana muongozo kwa kuwa, inapotokea hawana chanjo wakimng'ata mtu wanaweza kusababisha magonjwa lakini pia uwepo wao sehemu mbalimbali kama wana vijidudu au magonjwa wanaweza kuwa na athari kubwa.