Mkoba wa Mama
JF-Expert Member
- May 5, 2021
- 208
- 91
Kumekuwa na utaratibu usio rasmi wa walimu hasa wa shule zilizopo maeneo ya vijijini kuvunja ratiba za masomo na kupeleka wanafunzi kulimia mashamba yao.
Mfano shule ya msingi Nyamagana na shule ya sekondari Ngasamo zilizopo halmashauli ya wilaya ya Busega, mkoani Simiyu, hizi ni baadhi tu ya shule nyingi sana zenye utaratibu huu mbovu.
Cha ajabu zaidi ukifuatilia mpaka sasa unaelekea mwisho wa mwaka, walimu katika shule hizi bado hawajamaliza mada zinazotakiwa kufundishwa, lakini bado vipindi vinavyunjwa karibia kila siku na siku nyingine, siku nzima watoto wanashinda mashambani. Kama hizi shule nizamchepuo wa kilimo basi ieleweke na iwekwe wazi na kuwe na shamba maalum la shule na sio kugeuza wanafunzi kuwa vibarua wa mashamba ya walimu.
Mbaya zaidi matokeo ya shule hizi ni mabaya sana. Mfano ni matokeo ya darasa la saba shule ya msingi Nyamagana karibia nusu ya wanafunzi wamefeli (wana daraja D) lakini bado watoto hawafundishwi wanashinda mashambani.
Serikali itoe tamko kuhusu hili maana sasa ni kero kubwa.