Mamlaka ziwajibike juu ya usalama wa maeneo hatari kukumbwa Majanga ya Misimu yanayosababisha maafa

Mamlaka ziwajibike juu ya usalama wa maeneo hatari kukumbwa Majanga ya Misimu yanayosababisha maafa

Ghost MVP

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2022
Posts
439
Reaction score
736
Serikali ichukue hatua madhubuti kupitia viongozi wake katika mazingira mbalimbali waliyopo, tusisubiri maafa yatokee ndio tushtuke kuwa tunapaswa kuchukua hatua, inaumiza sana.

Kuwe na mipango mikakati juu ya kuweka usalama katika maeneo yalio na hatari za kukumbwa na mabalaa katika msimu fulani, tusitoe tu kauli ya 'HAMENI', waende wapi? Je, wewe unaweza muondoa mwanao nyumbani umwambie tu ondoka hapa? Tunapaswa jali wenzetu kama tunavyojali nyumba zetu.

Serikali za mitaa na vijiji ziwe active katika usalama wa mitaa yao, na kufatilia matatizo na kuyafanyia kazi.

Ikitoka kero mahala pa barabara fulan kuna shimo, au barabara mbovu tunapuuza ila zikishatokea ajali kadhaa tunaanza laumu wakandarasi na madereva. Nadhani ni muda sasa wa kuchukua hatua za usalama katika mitaa na vijiji ili kupunguza mabala ya maafa.
 
Back
Top Bottom